Vijana Warusi wameapa kujijeruhi ili kuepuka kuburuzwa kwenda vitani

Kungekuwa kuna kitu cha maana cha kupiganiwa wangeenda vinginevyo ni upuuzi..

Yaani watu wanaoitwa wanajeshi wamekuwa wanalipwa mapesa miaka na miaka sasa imefika mda wa kutukima hawataki bali wanataka watu wengine ndio wakapigane..

Ule pesa wewe afu nikapigane mimi? Upuuzi
 
Wanakimbia kwa sababu hawaelewi Putin anapigania nini huko Ukraine..

Putin si ana watoto awapeleke sasa vitani mbona anataka kulazimisha watoto wa wenzie?

Mwisho Kuna watu wamefundishwa kwa Kazi za jeshi na wanalipwa salary kwa Kazi hiyo Sasa kwa nini wachukue wasiolipwa?

Mda wa kufanya kazi wanayokula salary ndio huu sasa.
 
Tofautisha jeshi la ulinzi na amani na jeshi la frontline, kwenda frontline hata wakitangaziwa wabongo huwezi ona kuna boya anajitokeza.
 
Huku si wanajua wanaishia kula mshahara bila mabomu
 
Hata humu Tz ikitokea hali kama hiyo ya Urusi watakimbia. Hii ni kwa sababu kipindi cha bata wanapata nafasi za kuingia jeshini kwa mbinde, kipindi cha vita ndo wanapelekwa kwa amri.
Amani ni kitu cha maana sana Watanzania tuitunze
 
Siku vita ikitokea kwetu ndipo utajua kuwa watz hawaendi kupigana. Tutawaachia viongozi wakapigane.

Leo ajira zikitoka wanawapa watoto wao.

Vita ikija wanataka watoto wetu wawe frontline bila mafunzo.

Adui atashinda asubuhi.

Hakuna atakayekuwa mzalendo kwenye mauti.
 
Haha bongo vijana wengi hutaka kujiunga na jeshi sababu ya ugumu wa maisha tu na vile wakisikia jeshini mishahara na posho bwerere na nchi yetu ina amani ndiyo kabisaaa
 
Watu humu jf utakuta wanaishabikia Russia wakati Russia wenyewe wote hawana imani tena na Rais wao kwa mkenge aliowaingiza, kawaingiza raia wake choo cha kike, sasa tafran imeanza namtazamia Putin kusababisha fujo Urusi na mambo kuanza kwenda mrama zaidi kwake kuweza ku-stabilize hii situation. Huenda ndio mwisho dikteta putin,

One Man started the War and one Man have to go, Urusi wenyewe watam target maamae
 
Uko hakuna kushobokea kwenda jeshi kama bongo😂😂
 
Hali ni tofauti sana katika nchi mbili ulizotaja za Urusi na Tanzania. Kuwa mwanajeshi Urusi siyo fursa wala ajira, ni msala! Kwa hapa Tanzania, jeshi ni ajira moja ya uhakika sana, ukiingia unajihakikishia ajira salama, kwa kazi ambayo katika maisha yako yote ya kupanda vyeo na kulipwa vizuri wala hutaifanya kazi hiyo na utastaafu kwa heshima. Imagine watu walioingia jeshini 1992 leo hii wametimiza miaka 30 ya ajira bila kuhusika katika vita yoyote, na wengine wamestaafu bila kufyatua risasi yoyote nje ya viwanja vya mazoezi, zile za kulenga picha iliyochorwa kwenye karatasi ngumu umbali wa mita 100.
Hali ya usalama ndiyo inayotofautisha mazingira hayo, na kufanya huku kwetu jeshi ionekane ni ajira ama fursa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…