sos_10
Member
- Jun 23, 2024
- 7
- 21
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zinazokabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wasomi wanaohitimu katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu.
Utafiti uliofanyika mwaka 2019 na Taasisi ya utafiti wa kupunguza umasikini (REPOA) ilionyesha takribani vijana milioni moja huitimu kila mwaka vyuoni ilhali idadi ya ajira zinazozalishwa na serikali na sekta binafsi zikifikia 250,000, kwa maana hiyo kwa wastani kila muhitimu hutumia hadi miaka mitano kupata ajira.
Hali ilivyo sasa ni tofauti na miongo mitatu iliyopita ambapo nafasi za ajira zilikuwa nyingi kutokana na nchi kuwa na wasomi wachache kiasi kwamba vijana walipomaliza chuo hawakuchukua muda mrefu kuajiriwa na kuna ambao walipohitimu masomo yao tu moja kwa moja walipangiwa vituo vya kazi.
Hali ilikuwa hivyo katika soko la ajira miaka thelathini iliyopita ila kwa sasa mambo yamebadilika baada ya idadi ya wasomi kuongezeka.
Kwa mantiki hiyo sasa hata zile ajira ambazo awali zilichukuliwa za kawaida na za watu wenye ufaulu mdogo nazo zimekuwa ngumu kupatikana na zinagombaniwa hata na wasomi waliohitimu vyuo vikuu.
Sasa imefikia wakati serikali, wadau wa elimu, wazazi na vijana kwa ujumla kutambua kuwa nyakati zimebadilika hivyo ni vyema kuendana na mabadiliko hayo.
Yafuatayo ni mambo kadhaa ambayo yakizingatiwa yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira nchini kuanzia miaka kumi hadi ishirini na tano ijayo.
WAZAZI KUTAMBUA VIPAJI VYA WATOTO WAO NA KUVIENDELEZA:
Miaka ya nyuma sanaa na michezo kwa ujumla ilichukuliwa kuwa ni uhuni na vijana walioshiriki walionekana kama wasiofaa, walioshindwa na wanaopoteza muda kwa kufanya mambo yasiyo ya msingi.
Ukilinganisha na sasa ambapo sanaa kama muziki, filamu na mpira wa miguu imekuwa chanzo cha ajira inayowaingizia vijana fedha nyingi na kutoa ajira kwa vijana wengi huku ikichangia kuongeza pato la taifa kwani baadhi ya wasanii wamekuwa walipaji wa kodi na tozo mbalimbali za serikali.
Kwa mantiki hiyo mzazi anapaswa kutambua kipaji alichonacho kijana wake na kukiendeleza kwa kumpa nafasi ya kukitumia.
Sanaa si muziki, kabumbu na uigizaji wa filamu pekee, zipo fani nyingi ambazo zinaweza kugeuzwa kuwa ajira kwa vijana.
Kila mtoto amezaliwa na kalama yake na akiendelezwa ipasavyo ana uwezo wa kuwa bora kwa kufanya kile anachokimudu na kukipenda. Hatuwezi wote kuwa madaktari, walimu, wakandarasi na wanasheria hivyo mzazi anatakiwa aangalie ni kipaji gani alichonacho mtoto na kumsaidia kwa kumpatia maarifa na nyezo zitakazomwezesha kuja kugeuza kipaji alichonacho kuwa ajira yake.
SEKTA YA ELIMU KUBORESHA MITAALA NA SERIKALI KUWEKA SAWA MAZINGIRA YATAKAYOWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI:
Baada ya mzazi kutimiza wajibu wake kwa kutambua na kuwa tayari kuendeleza kipaji cha mtoto, linabaki jukumu la serikali na wadau wa elimu kama vile wamiliki wa shule binafsi na vyuo kutengeneza mazingira yatakayomwezesha kijana kukuza kipaji chake.
Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) iweke sawa mitaala iliyopo na kuongeza palipopelea. Ijapokuwa masomo ya sanaa na stadi za kazi yapo kwa sasa katika shule za msingi lakini yanapaswa kuboreshwa kwa kufanywa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia.
Kwenye mitaala ya shule za msingi kuongezwe masomo ya ufundi stadi yatakayohusisha kazi za mikono kama vile ushonaji, ujenzi, upishi na kadhalika na kwa shule za sekondari na vyuoni kuwe na somo la ujasiriamali ili kuwandaa vijana kuwa na dhana ya kujiajiri kwenye vichwa vyao pindi watakapohitimu masomo.
Serikali iajiri walimu wa sanaa waliosomea taaluma hiyo kutoka vyuo sanaa na wanafunzi wafundishwe somo hilo kwa vitendo. Kwa mfano wanafunzi wafundishwe matumizi ya ala za muziki kama vile gitaa, ngoma, kinanda na nyinginezo.
Kwa upande wa michezo kuwepo na walimu wa michezo mbalimbali shuleni na wanafunzi watengewe muda wa kushiriki. Pia shule za serikali zirejeshe viwanja vya michezo ambavyo asilimia kubwa vilitwaliwa kwa matumizi mengine na hivyo kusababisha watoto kukosa maeneo ya kuchezea.
Kuratibu na kutoa udhamini kwa vijana wanaofanya vizuri kwenye sanaa, michezo na ubunifu mbalimbali kwa kuwalipia ada na kuwaendeleza ili wakifanikiwa waje kutoa fursa kwa wengine.
Serikali iwape kipaumbele wawekezaji wazawa kwa kutoa ushirikiano kwa vikundi vya vijana wenye ubunifu na mawazo mazuri ya biashara kwa kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na kutoa msamaha wa kodi angalau wa mwaka mmoja kwa vikundi vitavyoanzisha biashara ili kuvipa muda kujiimarisha kabla ya kuanza kulipa kodi. Pia kipaumbele kitolewe kwa wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika sekta ya viwanda kwa kutoa masharti nafuu ya uanzishwaji na uendeshwaji wa viwanda nchini kwani sekta hiyo ina uwezo wa kutoa ajira kwa idadi kubwa zaidi.
Mikopo inayotolewa na Halmashari isiwe kwa ajili ya vikundi tu bali hata kwa kijana mmoja mmoja wenye ubunifu na mawazo ya biashara yanayoweza kutoa ajira kwa watu wengi.
Kuwe na utoaji wa elimu wa mara kwa mara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wapya kwani takwimu zinaonyesha 80% ya biashara zinazoanzishwa hufa ndani ya mwaka mmoja na kati ya 20% zilizobaki 10% hufa ndani ya miaka mitano na hii ni kutokana na wafanyabiashara wengi wanaoanza kukosa maarifa ya uendeshaji wa biashara.
VIJANA WABADILIKE NA KUWA NA FIKRA CHANYA ZA KUWA WAZALISHAJI WA AJIRA:
Kijana anapofikia umri wa kujitambua anatakiwa kutafakari na kufanya maamuzi ya nini kitakachomkwamua kiuchumi na kumletea maendeleo.
Taasisi za elimu ya juu ni sehemu zinazokutanisha idadi kubwa ya vijana toka mikoa mbalimbali nchini, vijana wenye uwezo na mawazo yanayotofautiana, wanaweza kutumia muda wanapokuwa chuo kutengeneza mtandao kwa kuunda vikundi vidogo na vikubwa na baada ya kuhitimu masomo, kupitia ujuzi walioupata kushirikiana kubuni fursa zitakazowasaidia kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wengine mtaani badala ya kutegemea kuajiriwa serikalini.
Mitandao ya kijamii isitumike tu kujiburudisha, kuperuzi udaku na vibonzo bali itumike kama nyenzo ya kuongeza maarifa na kugundua fursa zinazopatikana ndani na nje ya nchi. Pia itumike kama sehemu ya kutafuta masoko, kutangaza biashara na kuongeza idadi ya wateja ili kuendana na ushindani wa soko huria ambapo matumizi ya mitandao yameshamiri kwa kasi kubwa.
Vijana waitumie fursa ya fedha za mikopo zinazotolewa na Halmashari, kukopa na kufanya biashara zenye tija na zinazotoa ajira kwa watu wengi. Utoaji wa fedha hizo ambao awali ulisitishwa na waziri mkuu kwa ajili ya maboresho unatarajiwa kuanza kutolewa tena Julai 1, 2024 ambapo zimetengwa sh.227.96 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Vijana waitumie fursa ya fedha za mikopo zinazotolewa na Halmashari,
Upvote
2