Vijana, wekeni nadhiri ya kuzeeka mkiwa na heshima Kama Prof. Assad

Vijana, wekeni nadhiri ya kuzeeka mkiwa na heshima Kama Prof. Assad

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wazee wengi wameshindwa kutunza heshima yao, wameshindwa kuridhika na umri waliopewa na Mungu, wameshindwa kuwa kioo cha jamii, wamekuwa ndumilakuwili, hawana msimamo na awaridhiki na kile walichokwisha chuma.wapo tayari kuishi kwa unafiki ila wasitolewe kwenye nafasi zao.

Kwa sifa hizi wazee wanaoongoza Taifa letu wametengeneza kizazi kisichojiamini na kinachoishi kwa kubebwa na upepo kulingana na unavyovuma.

Vijana amjachelewa, chagueni Leo kuzeeka kwa heshima au kuzeeka kwa fedhea na kutukanwa mbele za watoto wenu pamoja mitandaoni.

Ningependa muamue Sasa kuishi maisha yakumpendeza Mungu, mkiwa na hofu ya Mungu mtawajali Watanzania. Mkiwajali Watanzania mtakuwa tayari kuwatetea hata Kama itagharimu kupoteza nafasi uliyo nayo. Wekeni dhamira yakustaafu Kama wazee wetu akina Assad, Ulimwengu, Samatta nk

Mkidhamiria na kuamini Mali za Dunia zinapita na Jambo kubwa lakuridhisha familia ni uadilifu basi Tanzania ya kesho itakuwa na matumaini.
 
Kama inawezekana hii thread angepelekewa Job Ndugai aisome ili imfumbue ubongo wake.
 
Tungekuwa na utaratubu wa kutoa Tuzo kwa Watanzania mahiri kama hawa.
 
Back
Top Bottom