Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 7,755
- 11,737
Habari wanaJF,
Niende moja kwa moja kwenye mada hapo juu. Mimi kwa Sasa nina umri wa miaka Hamsini na tatu(53). Niliajiriwa kwenye kampuni moja wakati huo nikiwa na miaka Ishirini na sita (26). Tukiwa vijana na rafiki zangu tulifurahia sana maisha na kampuni yenyewe ilikuwa inalipa vizuri sana.
Wenye ufahamu mzuri walijiwekeza kwenye ardhi, biashara, mifugo, nyumba, nk. Sasa umri umesonga nayo magonjwa nyemelezi yamekuwa tatizo. Ukimpigia simu mwenzako, utasikia naumwa kisukari mara huyu, kansa, mara, huyu viungo vimechemka, mara pressure nk.
Shida inakuja pale hukuwekeza gharama za matibabu ziko juu hata marafiki huwaoni na hata ukiwaona nao wanachangamoto zao. Tulikuwa na msemo wa kijinga wa ''Uza Nyumba Jenga Heshima Bar. Nisiwachoshe, Ahsanteni kwa kunisikiliza.