Vijana wengi CCM ni wanafki,wenye tamaa na wasio na Uzalendo

Vijana wengi CCM ni wanafki,wenye tamaa na wasio na Uzalendo

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
Ni vile tu ni kwa sababu ni vijana ni sehemu ya Chama, lakini naamini Mama hana jinsi lakini sote tunafahamu kuwa asilimia 90 ya vijana wa CCM ni wanafki, wamejawa na tamaa ya maisha huku wakiwa wameweka maslahi binafsi kuliko Uzalendo.

Tukichukulia mfano wa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa miaka mitano iliyopota vijana ndio wamekuwa mfano mbaya wa viongozi waliokosa heshima na hekima. Wamekuwa ni watu wanaosemwa, kulalamikiwa na kushutumiwa kuanzia kuonea watu, kuvunja sheria na kujibambikia mali. Watu kama Hapi, Makonda, Kihongosi, Sabaya ni mfano mizuri kabisa. Hawa hawakuwa na ajenda ya kuleta maendeleo kwao kupambana na upinzani ndio walioma ndio majukumu yao. Walifikia hatua kuwadharau na kuwatukana Wazee

Mama yetu alivyoingia, humu mitandaoni alikuwa akitetewa na vijana wasio na vyama na hata baadhi ya wale walio katika upinzani. Kwao waliona Taifa mbele na wakatamani utulivu na ustawi wa amani kwanza kama Taifa kisha mengine tayakuja baadae.

Leo baada ya Mama kuahidi Mkeka uliosheheni vijana ndio unaona vijana wa CCM kama wakina Mwakibinga wanaanzisha nyuzi za kumsifia Mama

Vijana wa CCM mmekiangusha sana Chama na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom