Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,833
- 8,777
Usipende sana kujiona wa zamani kuliko wote humu,maana hujui watu kawa sura zao,Sasa wengine sisi tumeanza kushangilia Simba tokea enzi za Akina Athuman Mambosasa,Daudi salum (Bruce Lee),Mohamed Kajole (Machela),Mohamed Bakari (Tall),Aluu Ali, Ezekiel Greyson (Jujuman),Abdala kibaden,...Leo baada ya ushindi kiduchu tunaanza kudanganyana kuwa mechi za nusu fainali hazina magoli mengi, pumbavu kabisa.
Hazina magoli mengi wakati RS Berkane anaongoza bao 2 huko hadi sasa half time halafu wewe unaleta uchawa wako wa kijinga jinga.
Wengine sisi tumeanza kwenda kuishangilia Simba enzi za akina Riziki Shawa, Mosses Mkandawile, Aston Pardon, Adam Selaman, marehemu Rafael Paul, enzi hizo uwanja wa shamba la bibi.
Leo tusiongopeane wala kuwatuma chawa kutetea ujinga, ukweli ni kuwa tumejimaliza wenyewe, leo Stellenbosch alikuwa anakufa hapa hapa nyumbani ila kocha kwa mapenzi yake kwa Ahoua ametuua.
Hakuna maneno yoyote ya kuambiana hapa ila Fahdu ametukwamisha sana leo, wachezaji wazuri aina ya Okajepha hawachezi mnatuwekea wachezaji wazito kama Ngoma, Chamou ambao hawana mchango wowote wa kuifikisha Simba mbele, sikatai ni wachezaji wazuri lakini sio kwa Simba.
Kwanini tuzidiwe wachezaji wazuri na Singida halafu sisi tujivunie Mukwala?
Viongozi wangu wa Simba sikusudii kuwaponda ila kiukweli kocha ameniumiza sana moyo wangu leo, maneno ya kiuongozi kuwa leo tumeshinda na tutakwenda kupambana ni kuondoana kwenye reli tu lakn ukweli ni kuwa wale wasauzi kule kwao wana privilege kubwa sana.
Anyway, hii imekwisha hata tukilalamika haisaidii maana ndio ishatokea tena, tupambane twende tukapasuane nao huko huko na inshaallah mm pia nitaenda huko bila kuomba nauli ya mtu au kujikomba kwa uongozi.
Nimeumia mnoooooooooo hamjui tu
RS Balkane kupata goli zaid ya mbili hakuzifanyi na timu nyingine zipate goli nyingi.
Kwa Simba kupata goli moja nao ni ushindi,kumbuka Kila timu ilitaka ushindi,acha uzuzu wewe Mzee.
Kwa hiyo Zamalek alipotolewa na Stellenbosch alikua Mjinga?
Mbona hao Stellenbosch hawakumshinda Zamalek SA?
Kwanza unapata wapi ujasiri wa kumkosoa kocha kua katukwamisha,wewe hata kufundisha timu ya watoto wa checkechea TU huwezi,unataka kushindana na kocha mwenye vyeti vyake?
Kati ya wewe na kocha Fadlu nani anahamu zaidi na matokeo ya timu?
Hebu acheni ujuaji nyinyi waswahili.
Timu IPO nusu fainali, na timu Iko mbele kwa goli moja,Tena imeshinda nyumbani,je ingekua imefungwa ama imetoa droo ungesemaje wewe Mzee?
Hakuna ushahidi kua tumu ikicheza nyumbani ni lazima ishinde goli nyingi.