Vijana wengi walioingia kushabikia Simba miaka ya hivi karibuni ndio wanaiua timu yetu kwa sababu ya mambo ya kijinga

Usipende sana kujiona wa zamani kuliko wote humu,maana hujui watu kawa sura zao,Sasa wengine sisi tumeanza kushangilia Simba tokea enzi za Akina Athuman Mambosasa,Daudi salum (Bruce Lee),Mohamed Kajole (Machela),Mohamed Bakari (Tall),Aluu Ali, Ezekiel Greyson (Jujuman),Abdala kibaden,...
RS Balkane kupata goli zaid ya mbili hakuzifanyi na timu nyingine zipate goli nyingi.
Kwa Simba kupata goli moja nao ni ushindi,kumbuka Kila timu ilitaka ushindi,acha uzuzu wewe Mzee.
Kwa hiyo Zamalek alipotolewa na Stellenbosch alikua Mjinga?
Mbona hao Stellenbosch hawakumshinda Zamalek SA?
Kwanza unapata wapi ujasiri wa kumkosoa kocha kua katukwamisha,wewe hata kufundisha timu ya watoto wa checkechea TU huwezi,unataka kushindana na kocha mwenye vyeti vyake?
Kati ya wewe na kocha Fadlu nani anahamu zaidi na matokeo ya timu?
Hebu acheni ujuaji nyinyi waswahili.
Timu IPO nusu fainali, na timu Iko mbele kwa goli moja,Tena imeshinda nyumbani,je ingekua imefungwa ama imetoa droo ungesemaje wewe Mzee?
Hakuna ushahidi kua tumu ikicheza nyumbani ni lazima ishinde goli nyingi.
 
hakika. UtopwiX walishindwa kufunga hata hako kamoja dhidi ya MC Alger
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Watu wa Simba mnajua mno kuchambua mpira aiseee
 
Nilipofika kwenye kundi la Yanga hakuna timu hata moja iliyofika nusu fainal nikajua ww ni zuzu!!, Unajua kundi la Yanga limekutana na timu zipi robo fainal?, Hizo timu mizania yake ni Sawa na Al masry au hawa stellen?.
Bado haujachelewa utapona tu mkuu utaahira wako,milembe sio mbali mbona
 
lakn ukweli ni kuwa wale wasauzi kule kwao wana privilege kubwa sana.
Marhaba mwanagu hujambo? Nilishasema na nasema tena Simba kwa South anaenda kukamilisha ratiba tu ila anaenda kuchapwa vizuri tu na mtarudi na kikapu kimejaa magoli ya kufungwa
 
Kwa Simba kupata goli moja
Ongezea goli moja la kupewa na refa maana ile ni clear Offside ila refa kawapa kwa mbeleko maana anajua kinachoenda kuwapata South sasa huku mkitoka kapa South mtapata nini?
 
Mkuu unaweza ukajiona umeandika Fact Kwa upande wako lakini zikawa pumba Kwa upande mwingine.

Usiwalazimishe watu wakubaliane na hoja zako maana nao Wana hoja zao na wanaziona ni Bora kuliko za kwako hata tufanye vipi.
Inaonekana una hoja za kulazimisha.
Unapowaambia hushabikii upambavu nali unaongea Fact nao wanaona hizo fact zako ni upumbavu,kwa sababu katika mijadala kama hii Kila mtu ana mtazamo wake.

Mfano unaposema Simba Inazidiwa Quality na Singida ndipo unapoonesha udhaifu wako ulipo.

Kwa sababu :

Simba hii hii unayoisema imezidiwa quality na Singida,ni ya pili katika Msimamo wa ligi Ya NBC ikizidiwa na Yanga kwa pinti mbili TU,
Singida ni ya ngapi?

Simba hii hii unayoisema imezidiwa quality na Singida ,sio kwamba Iko nusu fainali TU ya kombe la CAF Bali katika hiyo nusu fainali Ina goli moja katika mchezo wa kwanza ,
Singida inako nafasi ya ngapi kwa kombe lolote la CAF?

Simba hii hii unayoisema imezidiwa ubora na Singida Iko nafasi ya nne kwa ubora Afrika,Singida Yako Iko nafasi ya ngapi?

Simba hii hii unayoisema imezidiwa quality na Singida imefuzu kufika hapa kimataifa kwa kuzifunga timu zifuztazo kwa uchache:
Al Ahly Tripoli
CS Faxien
Constantine
Bravos
Al Masry
Na Stellenbosch mechi ya kwanza,
Singida Yako ingeweza haya?

Ok tufanye wachezaji wengi wa Simba wako chini ya viwango je Simba wangefanyaje kuwapata na kiwasajili wachezaji wa viwango?
Unajua gharama zao?
Unafikiri Simba hawataki kuwa na wachezaji ambao wewe uanwaona wanaviwango.
Kumbuka wachezaji wenye ubora mkubwa ni gharama,je umeisaidiaje Simba kupata Hela za usajiri wa wachezaji Bora.
Tuache ubora wa wachezaji wa Singida tuangalie ubora wa wachezaji wa Yanga inayoongoza ligi je mbona walishindwa hata kupata goli moja Kwa Mkapa na kupelekea kutolewa hatua ya makundi?

Wewe hata kama ni mtu wa mpira ila Kuna vitu vya mpira huvioni.
Kuifanaisha Simba iliyoingia nusu fainali Leo hii baada ya miaka mingi na Singida BS umenitisha sana Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…