Vijana wengi wanafungwa na kuteseka magerezani kwa kubambikiwa mimba na wanafunzi. Je, ushahidi wa mhanga unatosha kumtia hatiani mtuhumiwa?

Vijana wengi wanafungwa na kuteseka magerezani kwa kubambikiwa mimba na wanafunzi. Je, ushahidi wa mhanga unatosha kumtia hatiani mtuhumiwa?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Wanabodi hili suala ni changamoto kubwa sana katika jamii.

Utakuta binti anaanza mapenzi bado mdogo, tena yupo primary school au secondary school. Wazazi wanajua nini kinaendelea. Maana binti kama analiwa huwa hajifichi. Mara ghafla anapata mimba. Ili kuondoa aibu wazazi wanajifanya kwenda polisi.

Education Act, section 60A(3) ipo wazi, ukimpa mimba mwanafunzi unapigwa mvua 30.

Mabinti wengi wanaopewa mimba huwa tayari wameshatembea na wanaume zaidi ya mmoja. Hivyo hutafuta wa kumbambikia mimba. Na mara nyingi hukumu hutegemea ushshidi wa binti aliyepigwa kitofa kwa kumtaja mtu aliyempa mimba mahakamani. Labda itokee aliyempa mimba alikuwa anaishi na mwanafunzi hapo huwa ushahidi unakuwa rahisi. Ila wengi wanaofungwa huwa ni wanaotajwa na wahanga.

Je, ni sawa kwa mahakama kuridhika na ushahidi wa mhanga kisha kumfunga mtuhumiwa?
 
Katika pitapita mitandaoni niliwahi kukutana na kisa cha msichana anajuta kwa kusababisha kijana wa kiume kufungwa gerezani kwa kosa la kusingiziwa kama siyo kutembea nae nasi ni kumpa mimba.

Kesi nyingi za wanafunzi kupewa ujazito zina matege. Unaweza kukuta msichana ameshinikizwa na wenye pesa au mamlaka kumtaja mvulana au mwanaume ili kulipiza kisasi au kumkomoa kutokana na mzozo fulani. Wakati mwingine ni ile mwenye pesa anaamua kumtesa tu mtu.

Kwa kifupi kauli ya msichana haifanyiwi uchunguzi wa kina kwa sababu hata hao wanaohukumu kesi hizi huandaliwa na wenye pesa au huendesha kesi kwa hisia na maslahi ya mlalamikaji zaidi kuliko kuzingatia upelelezi.

Wapelelezi nao wakinyimwa pesa na mlalamikiwa hukomaa kutengeneza ushahidi ili kumkomoa mlalamikiwa kwa kuwa hakuwapa pesa.

Baadhi ya vijana wanafungwa kwa kuwa hawana kipato cha kuwapa askari wanaopeleleza kesi. Na hapa ndiyo wengi huonewa. Askari haangalii kuwa mlalamikiwa ni maskni au la, ni kudai tu pesa.

Fimbo hasa ya mimba za wanafunzi imewaumiza wengi wasiohusika katika tukio na kuwaacha wenye makosa wakila raha. Kuna haja ya mamlaka kupitia upya sheria na kanuni husika ili kupunguza uonevu.
 
Dawa ya yote hayo ni kuacha dhambi ya uasherati/uzinzi.

YESU NI MWOKOZI
 
Katika pitapita mitandaoni niliwahi kukutana na kisa cha msichana anajuta kwa kusababisha kijana wa kiume kufungwa gerezani kwa kosa la kusingiziwa kama siyo kutembea nae nasi ni kumpa mimba...
Upo sawa
 
Sidhani kama wanawazidi walioko ndani kwasababu za kisiasa
 
Wanabodi hili suala ni changamoto kubwa sana katika jamii.

Utakuta binti anaanza mapenzi bado mdogo, tena yupo primary school au secondary school. Wazazi wanajua nini kinaendelea. Maana binti kama analiwa huwa hajifichi. Mara ghafla anapata mimba. Ili kuondoa aibu wazazi wanajifanya kwenda polisi.

Education Act, section 60A(3) ipo wazi, ukimpa mimba mwanafunzi unapigwa mvua 30.

Mabinti wengi wanaopewa mimba huwa tayari wameshatembea na wanaume zaidi ya mmoja. Hivyo hutafuta wa kumbambikia mimba. Na mara nyingi hukumu hutegemea ushshidi wa binti aliyepigwa kitofa kwa kumtaja mtu aliyempa mimba mahakamani. Labda itokee aliyempa mimba alikuwa anaishi na mwanafunzi hapo huwa ushahidi unakuwa rahisi. Ila wengi wanaofungwa huwa ni wanaotajwa na wahanga.

Je, ni sawa kwa mahakama kuridhika na ushahidi wa mhanga kisha kumfunga mtuhumiwa?
Sheria ipo wazi linapokuja suala uzito wa ushahidi ili kumtia hatiani mtuhumiwa inapaswa kuthibitishwa, "pasi kuacha shaka" yaani beyond reasonable doubt...

Sasa suala ni uzito wa ushahidi kama je, waweza kidhi matakwa ya sheria yaani kuthibitisha pasi kuacha shaka? Kila kesi na mazingira yake...
 
Back
Top Bottom