Nitakujibu
1.nimeajiriwa kwenye Taasisi ya mabonde ya maji nchini yapo tisa so moja wapo mimi nipo Ilikuwa 2021 Kiukweli maisha ya utumishi mambo ni mengi
Kuhusu pesa sisi mshahara hakuna kitu nilijiingiza kwenye mikopo na wengi na ninapofanyia kazi Wana hio mikopo unaijua ya bank na Taasisi so wengi wamefika level ya kukopa mshahara ni ndogo.. Kwa sisi huwa tuna activities ambazo tunalipwa per diem yaani posho ambapo Kwa siku ni 150000 so ukipata kazi labda ya siku 20 ujue una million tatu ambazo ni kama mshahara wako wa miezi Sita..
Hizo kazi hazipo mara kwa Mara au niseme inategemeana na bonde uliopo Kwa mimi niko ambalo linajitafuta so kusubiri hela ya wizara ni kipengele at least hela kubwa hio utapata mara chache ila most of time naona wengi tukiwa site wanalalamika kuishiwa hela hata ikiwa nyingi ni matumizi tu wengine hawanywi pombe kama sisi ila wanaishiwa pia pengine wanafanya ya muhimu miradi.. Kiufupi hakuna jipya unapata hela ila inaisha
Nb:sio kila hela unayopata utatue shida nyingine kula raha kidogo si ni hela yako
Mengine ni ya kawaida si unajua hela ni vita so hata makazini majungu na kubaniana na ubinafsi wa baadhi hupelekea wewe kukandamizwa au kunyimwa Haki zako all in all ajira na Hela zake yafaa iwe backup tu ya wewe kupata mtaji ila kujiajir unakuwa busy zaidi.. Binafsi bila hela za posho katikati hapa Kwa mshahara nisingeweza huenda kazi ingenishinda so huwa najaribu kuwaza kazi ambazo hupati posho au over time wanaishi vipi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.