Nitakujibu
1.nimeajiriwa kwenye Taasisi ya mabonde ya maji nchini yapo tisa so moja wapo mimi nipo Ilikuwa 2021 Kiukweli maisha ya utumishi mambo ni mengi
Kuhusu pesa sisi mshahara hakuna kitu nilijiingiza kwenye mikopo na wengi na ninapofanyia kazi Wana hio mikopo unaijua ya bank na Taasisi so wengi wamefika level ya kukopa mshahara ni ndogo.. Kwa sisi huwa tuna activities ambazo tunalipwa per diem yaani posho ambapo Kwa siku ni 150000 so ukipata kazi labda ya siku 20 ujue una million tatu ambazo ni kama mshahara wako wa miezi Sita..
Hizo kazi hazipo mara kwa Mara au niseme inategemeana na bonde uliopo Kwa mimi niko ambalo linajitafuta so kusubiri hela ya wizara ni kipengele at least hela kubwa hio utapata mara chache ila most of time naona wengi tukiwa site wanalalamika kuishiwa hela hata ikiwa nyingi ni matumizi tu wengine hawanywi pombe kama sisi ila wanaishiwa pia pengine wanafanya ya muhimu miradi.. Kiufupi hakuna jipya unapata hela ila inaisha
Nb:sio kila hela unayopata utatue shida nyingine kula raha kidogo si ni hela yako