Vijiji vingi vilivyopo nje ya Africa ni vizuri sana

Unaweza tag Location tujue ni wapi hapa
 
Chai
 
Picha kwa msaada wa AI, yaan AI siku hizi anafanya vitu sio kawaida
Kuna vitu vingine tukubali tu tupo nyuma. Hili la vijiji halina ubishi. Kwanza serikali zetu huwa hazijali sana kuhusu kupeleka miundombinu vijijini
Kama hizo picha unaona hivyo vimerembeshwa na AI basi angalia vijiji vingine hivi.
 
Mkuu uzuri wa Ulaya sio kwamba tunauona kwenye TV, huwa tunafuatilia page za Traveling, na accounts za travellers wanazunguka maeneo mengi Ulaya, sio yale ya utalii pekee. Asilimia kubwa ya maeneo ya Ulaya ni mazuri
Hiyo picha uliyoituma ni ya Serbia kama Google lens haijakosea, lakini hata wewe unajua ni nadra sana kukuta vijiji kama hivyo Ulaya. Hata wao ni binadamu hawawezi kuwa perfect lakini at least asilimia kubwa ya maeneo yao ni mazuri

Sisi hata our biggest cities unakuta hakuna mpangilio, michanga imejaa barabarani na uswazi unachukua eneo kubwa ukicompare na miji ya Ulaya

Niliona account inayojitahidi kuonesha maeneo mabaya tu ya USA ili watu waone USA ni pabaya ila binafsi niliona ni useless account. Hayo maeneo hata kama yapo USA, huwezi kuignore zaidi ya 90% ya USA ambayo ina mwonekano mzuri kuliko miji yetu Africa

We mwenyewe unaona hata baadhi ya nchi za mambele zilivyo, unakuta nchi ina watu milioni 10 lakini ina miji na vijiji vizuri vingi.
Hapa Africa, especially Sub Saharan Africa kupata vijiji hata 10 tu kama hivi ni kazi ngumu sana. Kwanza vijiji vingi huku nyumba ni duni sana, barabara ni za vumbi tu, huduma za kijamii za hovyo. Kuna kijiji mwaka jana nilienda kipo wilaya ya Ludewa huko, aisee kule hali ni mbaya. Kwanza barabara imejaa mashimo, na kutoka Njombe hadi hiko kijiji (Manda) ni km 217 tu ila ilikuwa safari ya masaa 8, na huko Manda kuna mazingira mazuri sana ya asili, milima ya Livingstone, ziwa Nyasa, mto Ruhuhu nk lakini hakuna barabara nzuri, hakuna zahanati nzuri, shule zimechoka na kupo disconnected sana na maeneo mengine
Sasa unakuta nchi ya Ulaya ya watu milioni 10 ila ina vijiji kama hivi vya kutosha kila kona ya nchi
 
Jaribu vijiji vya Moshi...au Kilimanjaro kwa ujumla
 
Jaribu vijiji vya Moshi...au Kilimanjaro kwa ujumla
Huko nasikia kuna vijiji vizuri, itabidi nipatembelee
Ingependeza kama Tanzania nzima ingesifika kuwa na vijiji vizuri kama vya Kilimanjaro. Huwa naona watu wanasema vijiji vingi Kilimanjaro vina nyumba nzuri, barabara za lami, shule za kutosha, zahanati, maji, umeme wa uhakika, ukijani wa kutosha na maisha rahisi. Yani mtu una enjoy kukaa kijijini
 
Pia waweza kupata jumba...self ukakaa buree
 
Sikatai kama wametuzidi Ila sio kama picha zako za Google zinavyoonesha, hata Mimi naweza pick sehemu mbalimbali Africa kuonesha vijiji vizuri ila haitamaanisha Sisi hatuna slums na vijiji vilivyochoka.

Kuanzia Lesotho




Bo kaap south Africa


Sidi bou said Tunisia etc


Kote Ulaya huko kuna maeneo mabovu, unless upo nchi zinazotoa welfare kubwa kama za Scandinavia vile.

Mpaka Nchi kubwa kubwa kama Italy kuna sehemu zina umasikini wa kutupwa, Slums zisitamanika, miuchafu kila sehemu. Usidanganyike na picha nzuri nzuri.
 
Mkuu nahisi hatuelewani nikisema vijiji namaanisha nini
Hiyo first photo sawa ni kijiji ila

Hapa ni Maseru, Lesotho. Ipo kwenye mji mkubwa zaidi nchini humo

.
Hii Boo kap ni neighborhood kwenye jiji la Cape Town, sio kijiji
 
Labda iangalie vijiji vya Moshi hasa milimani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…