Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MUSOMA VIJIJINI - VIJIJI VYETU VYOTE 68 VINA MIRADI YA MAJI SAFI NA SALAMA
Miradi hiyo ya maji iko kwenye hatua mbalimbali kama ifuatavyo:
*Vijiji 2 vinatumia maji ya visima virefu
*Vijiji 32 tayari vinatumia maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Usambazaji unaendelea ndani ya vijiji hivyo.
*Vijiji 15 tayari vimepewa fedha za miradi, na ujenzi wa miundombibu ya usambazi maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria unaendelea
*Vijiji 12 (RUWASA) na Vijiji 7 (MUWASA) vinakamilishiwa usanifu na viko kwenye Bajeti ya Mwaka 2023/2024 inayoanza tarehe 1.7.2023.
SHUKRANI nyingi na za kipekee ziende kwa Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Tafadhali sikiliza CLIP ya RADIO iliyowekwa hapa - furaha ya Vijiji 6 kuanza kujengewa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.
Vilevile, CLIP/VIDEO ya Kwaya ya Musoma Vijijini nayo ina ujumbe mzuri.
MAJI NI UCHUMI & MAENDELEO
MAJI NI AFYA & UHAI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 20.4.2023