Vijimaneno vya kwenye JF

Vijimaneno vya kwenye JF

Wakuu kuna misamiati na Maneno yanatumika sana hapa JF lkn baadhi hatuyaelewi maana yake...mfano Mimi cjui maana ya baadhi ya maneno humu JF ..Naombeni kujuzwa kwa faida yangu na member wengine
........
1/Nyumbu
2/POPOMA
https://www.jamiiforums.com/index.php?posts/15688399

3/ Mkuu
4/Mbebez
5/BTW
6/ Ngabu
7/Usengerema
8/Jipu
9/Dushe
10/Papuchi
11/KUTUKUKA
12/Kibamia
13/Jukwaa la wakubwa
14/Makapuku

Superstar wa kitaa
The Bitoz
-Mtera/Bwawa
-Gegeda
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Vipi Umeshapata Jibu Lake Tayari? Kwa USAHIHI Kamili POPOMA Ni Neno Langu Nililolibuni Baada Ya Kulitohoa Ktk Lugha Ya KINDENGEREKO Na KIZARAMO Ambapo Linamaanisha Ni MTU MPUMBAVU WA KUTUKUKA AMBAYE HATA HASTAHILI KUISHI TENA DUNIANI KWANI HATOKUWA NA FAIDA KWA WENGINE KWA NAMNA YOYOTE ILE NA NI MZIGO PIA KWA JAMII HUSIKA. Ni Matumaini Yangu Kuwa Baada Ya UFAFANUZI Huu MURUA Wa Leo SITOSUMBULIWA TENA KUULIZWA NA MEMBER YOYOTE HUMU JF NINI MAANA YA NENO LANGU PENDWA LA " POPOMA " Naomba UWAFAHAMISHE NA WENGINE Pia Japo Najua Akina Nifah, Mussolin5 Na UncleBen Wanalijua Ila Nashangaa Wamekwepa Kukuambia au Sijui Yawezekana Labda Na Wao Hilo NENO Linawahusu!

Copied from@GENTAMYCINE

popoma [emoji15]
 
Nyumbu ni mnyama anayependa kufuata tu nyuma ya yule anayeongoza msafara hata kama atapita katikati ya moto. Ukitaka kufaidi vizuri ujinga wa nyumbu angalia wakati wanavuka mto hata kama kuna maji yenye kina kirefu na yenye nguvu wao watapita kwa mstari kwa kumfuata aliyetangulia. Hawawezi kuangalia labda kuna sehemu nyingine ambayo inaweza ikawa suluhisho.

Hivyo mtu akiitwa nyumbu maana yake yeye ni mtu wa kukubali/kufuata/kuunga mkono lolote linaongelewa na mtu/kiongozi fulani bila kupinga/ kuhoji/kutafakari hata kama kuna ukakasi. Anakuwa ni mtu wa kuunga mstari na safari inaendelea. Ndio wale wanosema ....... amekwisha sema
 
Poyoyo ni sawa na Popoma?
2: Popos ( mapopo)?
 
Back
Top Bottom