Vijiwe nongwa wameanza, kweli Chivayo amekata au ameingia mitini na Vibunda vya watu?

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Wakuu, nadhani mmeiona hii habari inayotrend mitandaoni kuhusu taarifa za kifo cha mfanyabishara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo. Taarifa za awali zinasema helikopta yake imeanguka maeneo ya Marondera. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, kabla hata mwili haujapoa, tayari minong'ono na nadharia za kijasusi zimeshaanza kusambaa kwa kasi.
825353307_1641543027331931_386910596146694608_n.jpg
Swali kubwa vijiwe nongwa ni moja: Je, jamaa amefariki kweli, au huu ni mchezo mwingine wakufake ajali ili aingia mitini na vitita vya watu?

Wasiwasi wa watu haukutokei tu bila ya sababu, Chivayo ana historia ndefu ya kashfa zinazotia shaka na kuibua maswali juu uaminifu wake:
  • Rekodi ya Jela (2004): Aliwahi kutumikia kifungo Afrika Kusini kwa makosa ya wizi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
  • Skendo ya Umeme wa nguvu za Jua (Gwanda): Jamaa alipiga zaidi ya dola milioni 5 kama malipo ya awali kwa ajili ya mradi wa umeme wa jua wa Gwanda, lakini hadi leo mradi haujakamilika.
  • Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC): Alikumbwa na tuhuma nzito za ulaghai wa zaidi ya dola milioni 100 za ZEC.
  • Kashfa ya Pasipoti za Kenya: Kuna nyaraka zilizovuja zikimhusisha na kashfa ya utengenezaji wa pasipoti zenye utata nchini Kenya.
Miaka ya hivi karibuni, huyu jamaa amekuwa akijipendekeza na kujipenyeza karibu sana na viongozi wakuu wa mataifa mbali mbali ya Afrika, huku akionesha maisha ya kifahari na kutoa zawadi zenye utata kiasi kwamba imewafanya wengi wahoji chanzo halisi cha ukwasi wake.

Hapa ndipo mzizi wa nadharia za minong'ono ya vijiwe nongwa inapoanzia: Vipi kama Chivayo alikuwa akikusanya na kushikilia mabilioni ya viongozi hawa kwa mtego wa kuwekeza viinua mgongo vyao vya uzeeni? Na baada ya kuona mzigo umekuwa mrefu kupiliza, akaona njia rahisi ya kucashout kisha kuandaa ajali ya uongo ili watu wamsahau ale bata zake kimya kimya na kukimbia na hiyo mipango ya watu ya kustaafu?
 
Wakuu, nadhani mmeiona hii habari inayotrend mitandaoni kuhusu taarifa za kifo cha mfanyabishara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo. Taarifa za awali zinasema helikopta yake imeanguka maeneo ya Marondera. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, kabla hata mwili haujapoa, tayari minong'ono na nadharia za kijasusi zimeshaanza kusambaa kwa kasi.
View attachment 3681396Swali kubwa vijiwe nongwa ni moja: Je, jamaa amefariki kweli, au huu ni mchezo mwingine wakufake ajali ili aingia mitini na vitita vya watu?

Amekufa.
 
Wakati wa Sekeseke na purukushani za Rubani kuituliza Helikopta.

Usikute jamaa alipomuona Rubani ngoma imemshinda gia zinagoma alipatwa na pressure akakata moto.

Helikopta inakuja kuanguka, yeye tayari kitambo mwili ushakuwa wabaridi.

Ule mwili nyie wenyewe si mnauona, unadhani atakosa pressure yule?
 
Wakuu, nadhani mmeiona hii habari inayotrend mitandaoni kuhusu taarifa za kifo cha mfanyabishara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo. Taarifa za awali zinasema helikopta yake imeanguka maeneo ya Marondera. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, kabla hata mwili haujapoa, tayari minong'ono na nadharia za kijasusi zimeshaanza kusambaa kwa kasi.
View attachment 3681396Swali kubwa vijiwe nongwa ni moja: Je, jamaa amefariki kweli, au huu ni mchezo mwingine wakufake ajali ili aingia mitini na vitita vya watu?

Wasiwasi wa watu haukutokei tu bila ya sababu, Chivayo ana historia ndefu ya kashfa zinazotia shaka na kuibua maswali juu uaminifu wake:
  • Rekodi ya Jela (2004): Aliwahi kutumikia kifungo Afrika Kusini kwa makosa ya wizi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
  • Skendo ya Umeme wa nguvu za Jua (Gwanda): Jamaa alipiga zaidi ya dola milioni 5 kama malipo ya awali kwa ajili ya mradi wa umeme wa jua wa Gwanda, lakini hadi leo mradi haujakamilika.
  • Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC): Alikumbwa na tuhuma nzito za ulaghai wa zaidi ya dola milioni 100 za ZEC.
  • Kashfa ya Pasipoti za Kenya: Kuna nyaraka zilizovuja zikimhusisha na kashfa ya utengenezaji wa pasipoti zenye utata nchini Kenya.
Miaka ya hivi karibuni, huyu jamaa amekuwa akijipendekeza na kujipenyeza karibu sana na viongozi wakuu wa mataifa mbali mbali ya Afrika, huku akionesha maisha ya kifahari na kutoa zawadi zenye utata kiasi kwamba imewafanya wengi wahoji chanzo halisi cha ukwasi wake.

Hapa ndipo mzizi wa nadharia za minong'ono ya vijiwe nongwa inapoanzia: Vipi kama Chivayo alikuwa akikusanya na kushikilia mabilioni ya viongozi hawa kwa mtego wa kuwekeza viinua mgongo vyao vya uzeeni? Na baada ya kuona mzigo umekuwa mrefu kupiliza, akaona njia rahisi ya kucashout kisha kuandaa ajali ya uongo ili watu wamsahau ale bata zake kimya kimya na kukimbia na hiyo mipango ya watu ya kustaafu?
Si kwa dunia hii yenye uwazi mkubwa kiasi hiki,atajificha wapi
 
Back
Top Bottom