ANAITWA Daudi Issa Masasi. Ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha upinzani cha ADC akitaja vipaumbele 10 vyake endapo atapata ridhaa ya chama chake na wapiga kura wa jimbo hilo.
Daudi Masasi ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Jarida maarufu la Tabasamu anasema:
"Mimi Daudi Issa Masasi Kamishina wa ADC Nyanda za Juu Kusini. Natangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini, Oktoba 2025, Mungu akipenda. Ninawaomba wana Iringa tuje pamoja kufanya mabadiliko kwenye jimbo letu na Halmashauri yetu. Tunawakaribisha wote wenye nia na sifa ya kushinda udiwani kwenye kata zao tuache ushabiki wa vyama vyetu.
Fursa zilizopotezwa na watangulizi wetu; tutazitaja na kueleza namna ya kuzirejesha na tutataja fursa mpya ya kuleta uchumi na kuongeza mzunguko wa pesa kwenye jimbo letu.
Jimbo litakalowanufaisha watu wote, kuanzia Halmashauri yenyewe, wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo. Wajasirimali wote mama lishe, bodaboda, bajaji, daladala, wapigadebe, taksi, (Alphad, Noah), guta, Toyo, Pick-up na hadi wenye nyumba za kupangisha vyumba, watu wa saluni, (vinyozi), wamachinga, mafundi nguo, mafundi ujenzi, watengeneza sofa, (seremara), wauza viungo, wauza mboga, wauza vitafunwa na kila mtu pato lake litakuwa maradufu.
Yatawezekana vipi mambo haya? Naam yatawezekana kwa vipaumbele vya moto ambavyo baadhi vimeanza kutimia. Niliwahi kugombea Ubunge Jimbo hili la Iringa Mjini mwaka 2005, 2015, 2020 na nikijaaliwa kugombea 2025 itakuwa ni mara ya nne. Kwa hiyo huko nyuma nilieleza vipaumbele vyangu. Hapa leo nataja vipaumbele ambavyo vimefanikiwa japo kwa kuchelewa sana kwa sababu mtoa hoja sikuwepo kwenye nafasi ya utekelezaji.
1. Kipaumbele cha kwanza;
Taa za kuongoza magari barabarani kwenye Manispaa ya Iringa. Kipaumbele hiki kilikuwemo kwenye vipaumbele 2015 na 2020 sasa zimewekwa. Mwandishi wa habari wa Azam, Joseph Mpangala alinihoji na kurusha Azam TV. Wana Iringa ni mashahidi.
Rafiki yangu anaitwa Jamhuri Kikoti akanipigia simu kutoka Mbeya, akaniambia; naona unataka kutuwekea taa za kuongoza magari kwenye mji.
2. Kipaumbele cha pili;
Soko Kuu la Kisasa. Hili pia nilizungumza 2015 na 2020, na watu wa Iringa, hususan wauza soko kuu Iringa ni mashahidi. Nilisema soko kuu la kisasa Iringa, kwa vile Iringa ni mji wa kilimo, tukajenge pale sabasaba, soko kubwa kama soko la Kariakoo au zaidi. Maana litakuwa la kimataifa.
Na hapa lilipo la sasa pajengwe maegesho ya magari ya kisasa (ghorofa 4-5) kwa sababu jiografia ya mji wa Iringa, huduma muhimu zote zipo katikati ya mji. Soko la Mjerumani, polisi wilaya, hospitali ya rufaa ya mkoa, hospitali ya AghaKhan, magereza bomani, mahakama ya wilaya, mahakama kuu, maduka (Kariakoo ya Iringa), ofisi ya polisi mkoa, TRA na ofisi zote zipo katikati ya mji. Na wafanyabiashara wa maduka, maofisini nk. Wana vyombo vya usafiri na hakuna maegesho.
Sasa hili ni kipaumbele changu kimetimia vipi? Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2025, Ismail Ally Ussi, Mwenge wa Uhuru ulipofika sokoni hapo alisema:
"Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa pesa za soko kuu Iringa mjini. Wahusika ni kuchora ramani na lijengwe."
Pamoja na kuwa ni vipaumbele vyangu, mimi nilimwandikia Mh. Rais barua ya wazi na nikaongea na waandishi wa habari Isimila Hotel na Mtandao wa Matukio Daima wakaiweka mtandaoni.
Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha ingia Youtube, sachi Matukio Daima , Kamishna wa ADC Mkoa wa Iringa ataona jambo hilo na mengine niliyowahi kuhojiwa na TV hiyo.
Kwa hiyo kwa kutupatia pesa hiyo, Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya watu wa Iringa mjini (kwa vile mimi ndiye mtoa hoja) kwa dhati kabisa na kwa heshima na taadhima nasema asante sana.
3. Kipaumbele cha tatu kilichotimia;
Soko la Kisasa la Kihesa. Hili lilikuwepo kwenye vipaumbele
vyangu mwaka 2005 nilipogombea ubunge kwa mara ya kwanza.
Na kipaumbele hiki nilisoma kwenye mdahalo uliofanyika Radio Cantri. Na ninacho kipeperushi hicho. Kipaumbele hiki kimetimia kwa mjibu wa kikao cha madiwani, ambacho mimi nilialikwa na Mkurugenzi Kijazi amethibitisha kuwa pesa yake tayari imetolewa na wafanyabiashara wote wa Soko la Kihesa wanahamishiwa Ngome kwa muda ili kupisha ujenzi.
4. Kipaumbele cha nne kilichotimia;
Shule za awali kwenye shule za msingi za serikali.
Hili kama Soko la Kihesa. Lilikuwepo kwenye vipaumbele vya 2005 na sasa
kimetimia.
Shule zote nilizofanya utafiti nimeona kuna madarasa ya awali.
5. Kipaumbele cha tano kilichotimia;
Umoja wa wana Iringa.
Naam umoja wa wana Iringa ilikuwa ni kipaumbele changu 2015 na ndivyo moyo wangu unavyopenda siku
zote.
Kipaumbele hiki kimetimia vipi? Ni vile vikundi mbalimbali
vya wana Iringa. Ni vikundi vingi mno ambavyo vimewafanya wana
Iringa kupata maendeleo ya aina tofauti kama vile kuwawezesha
wanavikundi, kujenga, kuimarisha biashara, kwa maana ya kukuza mitaji, kufanya sherehe za harusi, kuzikana (ushirikiano kwenye
misiba) kwenye maradhi n.k.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kuwa maono yangu ni ya
hali ya juu sana. Na hii si kwa Iringa tu, bali ni mimi niliyeshauri kwa
maandishi kupitia gazeti la Majira, wakati huo foleni la Jiji la Dar es
Salaam zilifikia kuwa kero na watu kutumia muda mwingi barabarani. Mijadala ilipoanza kwamba tufanye nini ili kulitatua tatizo hilo?
Ndipo niliposhika kalamu na kutiririka madini tupu, na kweli leo kumepatikana Kituo Kikuu cha Mabasi Kariakoo (Gerezani) Kituo cha Kivukoni.
Na kubwa kuliko yote Bandari ya Nchi Kavu katikati ya Vigwaza na
Chalinze (ndivyo nilivyo shauri) na vyote vinetimia.
Hizo Terminal za Kariakoo na Kivukoni na Bandari ya Nchi
Kavu ya Kwala. (Mimi ndiye mtoa hoja), na kijana wa kwanza kutoka Iringa kusajili chombo cha habari serikalini (Idara ya Habari - Maelezo) Gazeti la Tabasamu 'Chombezo la Burudani' kiboko cha vijarida. Ukitazama kwa makini utaona maono haya ni ya viwango vya kuleta sura nzuri kwenye mji wetu, lakini na kukuza uchumi na kuongeza mzunguko wa fedha kwa watu wake. Ni maneno ambayo ndiyo sifa ya mtu anayestahili katika uongozi hasa nbunge.
Sasa nidokeze vipaumbele vipya.
Vipaumbele vipya vitaendelea...