Haya ni matokeo au kisababishi chake ni mambo kadhaa kama ifauatavyo:
1. Mwaswala ya haki sawa. Ulimwengu wa haki sawa umewapumbaza sana watoto wakike kuamini kuwa Mwanaume ni adui yake na anatakiwa kujitafutia maisha pembeni au nje ya maisha yake na mwanaume. Mwanaume amtumie tu kama daraja kuyafikia maisha.
2. Kufuata mikumbo ya marafiki bila malengo ya kueleweka. Wanawake wengi huamini wanachofanya wanawake wenzao ni sahihi zaidi kuliko atakachoelekezwa na mume wake, mchumba wake au familia yake. Mabinti wengi hujiunga vikoba kwa ushawishi wa rafiki zao especially wale ambao wamezaa nje ya ndoa na hawana mume wabidi kuingia kwenye vicoba ili kujikimu kimaisha ila wao huingia na huku hawajui ni sababu ipi wanaingia. Shida ni wakishika hizo pesa hakuna la maana wanakuwa nalo la kufanya zaidi ya kutumia katika vitu ambavyo hawajui vitawapa mrejesho gani kifedha au kuwanufaisha vipi kifedha.
3. Tamaa ya pesa. Wengi wa wanawake wanakwenda kujiunga na vicoba kwa malengo ya kujipatia fedha za kujikimu shida zao ndogo ndogo na wanakopa bila kujua pesa ya kulipa inatokea wapi matokeo yake muda ukifika hana hata buku ya kurudisha anajikuta matatani hapo anakuwa hana namna ila kukopa hovyo ili alipe madeni ya kikoba. Upuuzi kabisa yaani.
4. Viburi kwa wanaume wao. Mwanaume anajua kuwa anawajabu na jukumu la kuhudumia mke wake ili washirikiane kujenga familia. Ila changamoto iliyopo kwa sasa hawa mabinti ni 2 katika kumi ndio wanajua wajibu wao wa kuwa mke kwa mwanaume na kuwa na disciplined enough kujua mwanamke na mwanaume si sawa na hawawezi kuwa sawa hata iwe sayari gani.
Kiburi cha mashindano na kutaka kumuonyesha mwanaume kuwa na yeye anaweza kujisimamia huwapeleka kujiunga na vikoba wakiwa na malengo ya kufungua biashara na kufanikiwa as if ni rahisi namna hiyo katika maisha haya ya tozo kutoboa ukiwa pekee yako kama mchawi. [emoji23][emoji23][emoji23] Matokeo yake wanadanganyana na marafiki zao micharuko wanajikuta katika madeni mazito na biashara zilivyongumu miaka hii wanajikuta hawana namna ila kurudisha majeshi nyuma wakiwa na madeni kibao.
Kuna dada alitofautiana na baba watoto wake jamaa m'moja mpole sana na hana makuu, aliondoka kwa dharau sana na ngembe za usinibabaishe hata mimi naweza kupambana na maisha. Kwa kushawishiana na marafiki zake wasiojua maana ya ndoa ni nini akaondoka na watoto.
Akaenda kwenye mishe mishe zake huko akapambana akapata kiwanja maeneo ya chanika. Akaanza ujenzi na akamaliza na kuhamia nyumba ikiwa katika hali ya finishing. Huku na kule akahamia.
Sasa muda wote huu jamaa alijitahidi kusuluhisha mwanamke kiburi jamaa akakata tamaa akahama. Nasikia yupo geita huko anapambania huko.
Bi dada amehamia kule nje ya mji maisha ni magumu kuishi nje ya mji watoto walikuwa wanamuelemea jamaa akaenda kuwachukua na kuwaleta kwa bibi yao tegeta maana walitakiwa kuanza shule. Mama yao alitaka kukomaa ila akikumbuka balaa lake anaona bora waende kwa bibi yao.
Kwa bahati nzuri kuna mjomba wake hapo kifuru ananyumba so akamwambia akaishi pale ili iwe rahisi kufanya biashara. So alirudi town nyumba kule ikabidi aweke sokoni ili apate mtaji. Ameanza biashara ameingia katika vicoba madeni sasa na huu ugumu wa maisha ikabidi ampigie simu baba watoto amsapoti kidogo kidogo madeni.
Nikajifunza somo juu ya wanawake kuwa inapokuja swala la kufanya maisha na mafanikio wao huwa wanakuwa very selfish wanajifikiria wao tu na wanataka waonekane wao ndio wamepambana bila msaada as if kuna sehemu watapewa tuzo ya upambanaji.
Sent using
Jamii Forums mobile app