Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 11,462
- 21,124
Mimi Mdau wa JamiiForums ninasema hivi, vikundi vingi katika jamii ni changamoto.
Vikundi vingi vimejikita katika:
1. Kusaidiana katika shida na raha, yaani hivi havina malengo zaidi ya kuchangishana pesa za misiba na sherehe mbalimbali ikiwemo harusi, sendoffs na birthdays. Changamoto kwenye aina hii ya vikundi ni pamoja na kama mtu huchangi basi huchangiwi. Mchango wa msiba ni iwapo mwanakikundi kafiwa na kati ya mke, mume, mtoto, baba au mama. Ukifiwa na ndugu mwingine, mbali na hao, basi unapewa tu pole yanaisha. Hapa utakuta vikundi vina majina kama vile "KUFA NA KUZIKANA GROUP" n.k.
2. Pia kuna vile ambavyo malengo yake ni kuweka akiba, yaani kila mwezi wamewekeana kiwango mfano, kila mwanachama achange elfu 10 ili kuweka akiba kwenye akaunti ya kikundi. Changamoto ya hapa ni pale ambapo wanakikundi wachache wanachanga kwa sababu mbalimbali. Pia fedha kukaa benki huku ikikatwa. Lakini pia, wanakikundi wengine huona wivu pale fedha inatolewa kwa wenzao waliopata matatizo, na hili huweza kuibua migogoro na kufifisha uchangiaji.
3. Kuna vile ambavyo malengo yake ni kuweka na kukopa. Hawa ni maarufu zaidi kama 'KIKOBA'. Hawa kidogo wapo 'smart' na wanatambulika kisheria na wanajaribu kufanya kazi zao kitaalamu, japo kuna vingine vinajiita 'KIKOBA' ila havipo kisheria.
4. Kuna vikundi vimeenda mbali zaidi kwa kufanya uwekezaji kwenye viwanda, biashara au kilimo na ufugaji. Hivi vipo serious kidogo na baadhi vinakopesheka na wadau mbalimbali.
Sasa mimi sina tatizo vikundi ambavyo vina miradi endelevu, isipokuwa vile vya kusaidiana katika shida na raha, kuweka, na vile vya kuweka na kukopa.
1. Vikundi vya kusaidiana katika shida na raha. Mimi sikatai kusaidiana katika shida na raha, ila wasiwasi wangu, ni kwanini watu wajiunge kwa pamoja kwa minajili ya kusaidiana kwenye shida na raha? Mimi kwa maoni yangu, watu waunde vikundi vyenye malengo ya kutatua changamoto zilizopo katika jamii mfano ajira, kipato n.k, halafu mambo ya shida na raha yatatatuliwa tu ilimradi wanakikundi wana miradi endelevu na uwezo wa kifedha. Na hivyo basi kipindi cha majanga au sherehe, fedha za kusaidiana zitatoka kwenye akaunti ya kikundi badala ya kuanza kukimbizana na michango na kupigiana simu.
Na isitoshe, mkishakuwa na kikundi chenye miradi, mnaweza mkaamua kuwa na kamati ya kushughulikia masuala ya majanga na sherehe. Sasa ukisema unaunda umoja wa kujishughulisha na shida, maana yake tunajiaminisha kwamba tatizo tulilonalo ni shida za misiba na magonjwa, kwa hiyo tuungane wakati wa misiba na magonjwa tu, na baada ya hapo kila mtu kivyake.
Halafu suala la kumchangia yule anayechangia, kwangu halijakaa vyema kwa sababu kanuni hii inamfanya mtu achangie msiba ili aje achangiwe, na siyo kwamba anachanga kwa kuwa ameguswa na msiba. Wengine wanadiriki kusema 'mkeka' wa mchango uhifadhiwe ili pindi ikitokea msiba au sherehe, basi wanachama warejee kwenye record waangalie je, mwenzao mwenye msiba alikuwa mchangiaji?