Vikundi/ vyama vya KUFA na KUZIKANA vinaleta ustawi gani katika jamii?

Vikundi/ vyama vya KUFA na KUZIKANA vinaleta ustawi gani katika jamii?

jozee jose

Senior Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
147
Reaction score
360
Utamaduni ni jambo ambalo linanguvu saana, Hata wataalamu wa mambo ya kijamii wanasema ili uweze kubadilisha utamaduni wa sehemu fulani inaweza kuchukua hata miaka 50.

Katika jamii zetu kumekuwa na desturi au kaida za kuisaidiana katika Sherehe mbalimbali kama harusi, birthday, vipaimara, ubatizo na n.k vile vile hata kwenye majanga mbalimbali kama misiba

Sasa nataka kuzungumzia vyama hivi ambavyo huenda vinakusudia mazuri katika kusaidiana, vyama vya KUFA na KUZIKANA ambavyo wao husaidiana kwenye Misiba tuuu.

Ngoja nikupe mfano huu
Kikundi kinaweza kuwa na wanachama 21 ambapo kila mmoja wakati mwenzao amepatwa na maafa itabidi mchango utolewe kuanzia 50 000 hadi 100 000 na wengine zaidi.
Tukichukua mchango wa 100 000@ 20 baada ya kutoa 1 kwa mpata maafa utapata around Tsh 2000 000.
Sasa kama vile tujuavyo binadamu na PESA , Yeye anakuwa ni mtu wa kuchangia wenzake mwaka wa kwanza, wa pili , wa tatu, wa sita😁😁😁

Je mtu wa Namna hii itakuwa kwenye hali gani?
Je hatajaribiwa atamani nduguze wafe ili naye mkeka utiki?
Sasa mdau unasemaje kwa ustawi wetu katika hili?

Jitahidi kuwa positive , mwagikaaa
 
Kila kitu kinachoanzishwa na watu ujue wameona umuhumu wakee mkuu,,,kuwa na vikundi ni muhimuu ilaaa kuwa na pesaa n muhimu zaidiiii
 
Yani utamani kufiwa kwa.ajilia ya pesa kweli?kwa pesa ipi hiyo isiyoisha?hivi kweli utakuwa timamu kumuonea wivu mtu aliyefiwa utakuwa timamu kweli?
Vikundi hivyo ni muhimu sana sana . .unaweza kuwa uanaishi mbali na ndugu zako lakini ukiwa na umoja huo incase ukapata majanga hao watajitokeza wa kwanza na kutoa ushirikiano kabla ya ndugu zako kufika.
 
Mbona mwizi anaweza kukuua kwa hela ndogo tu?...
 
vinasaidia sana niliona nilipofiwa na wazee wangu kwa nyakati tofauti, ukiachana na michango ya rambirambi lakini wanakikundi ambako mke wangu ni mwanachama walifanya almost kazi zote kwa kujitolea sana.
Mkiwa mnaambiwa vikao vya vikoba na wake zenu muwe mnatoa michango ya kila mwisho wa mwezi ..mshikamano huo sio burebure si uliona umuhimu wake mkuu
 
Back
Top Bottom