Utamaduni ni jambo ambalo linanguvu saana, Hata wataalamu wa mambo ya kijamii wanasema ili uweze kubadilisha utamaduni wa sehemu fulani inaweza kuchukua hata miaka 50.
Katika jamii zetu kumekuwa na desturi au kaida za kuisaidiana katika Sherehe mbalimbali kama harusi, birthday, vipaimara, ubatizo na n.k vile vile hata kwenye majanga mbalimbali kama misiba
Sasa nataka kuzungumzia vyama hivi ambavyo huenda vinakusudia mazuri katika kusaidiana, vyama vya KUFA na KUZIKANA ambavyo wao husaidiana kwenye Misiba tuuu.
Ngoja nikupe mfano huu
Kikundi kinaweza kuwa na wanachama 21 ambapo kila mmoja wakati mwenzao amepatwa na maafa itabidi mchango utolewe kuanzia 50 000 hadi 100 000 na wengine zaidi.
Tukichukua mchango wa 100 000@ 20 baada ya kutoa 1 kwa mpata maafa utapata around Tsh 2000 000.
Sasa kama vile tujuavyo binadamu na PESA , Yeye anakuwa ni mtu wa kuchangia wenzake mwaka wa kwanza, wa pili , wa tatu, wa sita😁😁😁
Je mtu wa Namna hii itakuwa kwenye hali gani?
Je hatajaribiwa atamani nduguze wafe ili naye mkeka utiki?
Sasa mdau unasemaje kwa ustawi wetu katika hili?
Jitahidi kuwa positive , mwagikaaa