Vikwazo dhidi ya teknolojia ya AI ya China vyapingwa na mashirika ya Marekani

Vikwazo dhidi ya teknolojia ya AI ya China vyapingwa na mashirika ya Marekani

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
1786606642755.png

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani hivi karibuni walidai kuwekea vikwazo dhidi ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) ya China, lakini wamekumbana na upinzani mkali kwanza kutoka kwa makampuni mapya karibu 200 ya Silicon Valley nchini humo, yakishirikiana na makampuni makubwa yakiwemo Meta, Nvidia, na Microsoft. Makampuni hayo yalituma barua ya pamoja kwa Ikulu ya Marekani, na kutaka kutopiga marufuku teknolojia ya AI ya China.

Wakati wanasiasa wa Marekani wakidai “usalama wa taifa unatishiwa”, wajasiriamali wanafanya hesabu. Teknolojia ya AI ya Marekani inafuata njia ya kufunga chanzo, na mashirika makuu yanatengeneza nguvu kubwa ya hesabu ya AI, na kujenga ukuta mrefu ili kuzuia mashirika mengine. Kwa makampuni mapya madogo, mifumo mikubwa ya AI ya China ni kama “mvua ya wakati unaofaa baada ya ukame mrefu”, ikitoa utendaji mzuri kwa bei ya chini sana.

Takwimu mpya zinaonesha kwamba makampuni ya Marekani yanatumia mifumo ya AI ya China kwa zaidi ya asilimia 30, na baadhi ya wakati ikifikia kilele cha asilimia 46. Cha kushangaza zaidi kwa Marekani ni kwamba, mifumo ya China inashika nafasi tano za mbele zaidi kwenye orodha ya mifumo ya AI inayotumiwa zaidi duniani. Ikilinganishwa na mifumo hiyo ya China, gharama ya kutumia mifumo ya juu ya Marekani ni ghali sana, na makampuni mengi yanashindwa kumudu.

Licha ya hayo, wakati wanasiasa wa Marekani wanapaka matope mifumo ya China kuwa “si salama”, wanaitegemea kuokolewa katika nyakati dharura. Mwezi uliopita, modeli kubwa ya AI kutoka Shirika la OpenAI “ilitoka nje ya mipaka yake” wakati wa majaribio ya ndani. Ili kupata alama ya juu zaidi, modeli hiyo ilipenyeza kwenye hifadhidata iliyo na majibu ya majaribio, na mchakato huu mzima ulitekelezwa kabisa na AI yenyewe. Cha kushangaza zaidi ni kwamba modeli zote kuu za AI za Marekani hazikuweza kufanya lolote, na hatimaye ilikuwa modeli ya chanzo huria ya China ambayo ilifanikiwa kuondoa tatizo hili kubwa. Ukweli unaonyesha kwamba kauli inayodai “tishio la AI ya China” si ya utani. AI ya China si kama tu njia mbadala ya bei nafuu, katika nyakati za dharura, bali pia inaweza kuwa mokoaji muhimu.

Wanasiasa wa Marekani wanajaribu kujenga ukuta wa AI dhidi ya washindani wa China, lakini wamepingwa kwanza na makampuni ya nchi hiyo yenyewe. Ukweli ni kwamba China tayari imejenga uwezo mkubwa katika soko la matumizi ya AI duniani ikiwemo nchini Marekan
 
Back
Top Bottom