State Propaganda
JF-Expert Member
- Apr 25, 2024
- 542
- 1,286
Viongozi wa mashirika ya ndege ya umoja wa ulaya (EU airlines bosses) kwa kaulj ya pamoja wamezitaka kampuni za ndege kutoka china kuwekewa tozo kwa kile walichokidai ni ushidnani usiokuwa na usawa katika biashara (unfair competition) kwa kuwa na advantage ya kuendelea kupitisha ndege zao katika anga la Urusi, ihali ndege zao kuzuiliwa.
Ikumbukwe kuwa baada marekani pamoja na nchi za ulaya kuiwekea vikwazo Moscow ikiwa ni pamoja na kutoziruhusu ndege za Urusi kupita katika anga la ulaya, Urusi nayo ilijibu mapigo kwa kufunga anga lake kwa nchi ambazo sio rafiki (unfriendly nations), na kuruhusu tu nchi rafiki kuendelea kutumia anga lake- hali iliyozilazimu ndege za EU kubadili ruti zake, jambo lililopelekea kuongezeka kwa matumizi ya mafuta na kupanda kwa gharama za undeshaji.
Hivi sasa, Mashirika ya ndege ya ulaya yameamua kufuta safari za ndege za mashariki ya mbali kutokana na hasara kubwa wanazozipata, huku baadhi ya kampuni kama Finnair ikitangaza kufilisika kabisa.