SoC01 Vikwazo kwa Wanasoka Vijana wa Tanzania katika kucheza soka la kulipwa nchi za nje

SoC01 Vikwazo kwa Wanasoka Vijana wa Tanzania katika kucheza soka la kulipwa nchi za nje

Stories of Change - 2021 Competition

strong star

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
36
Reaction score
42
Soka ( ama mpila wa miguu ) ni moja kati ya michezo inayopendwa na kufuatiliwa sana ulimwenguni kote, Mchezo huu una wafuasi wengi zaidi ya michezo mingine duniani, Vijana mbali mbali duniani wamekuwa wakifaidika, kuwa maarufu na kujipatia maendeleo kupitia soka, vivo hivyo , Ndizo ndoto za vijana wengi wa kitanzania.

Pamoja na juhudi zao nyingi katika kukuwa na kujipatia mafanikio kupitia soka ,vijana wengi wamekuwa wanakumbwa na changamoto hizi katika safari hiyo,

Uelewa mdogo juu ya soka.

Moja kwa wazazi au walezi


Bado wazazi au walezi hawana elimu ya kutosha juu ya soka kwani uutazama mchezo huu kama uhuni na utaueletea matatizo na migogoro kati yao na wanajamii hivyo kumkataza mtoto wao kushiliki kikamilifu au kumnunulia vifaa na kumuandikisha katika vituo mbalimbali na kutimiza ndoto.

Uelewa wa Jamii

Jamii zetu za kitanzania bado hazina uelewa wa kitosha juu ya mpira wa miguu kwa mfano inakuwa ni vigumu sana kumpa moyo na kumjenga kijana kupitia soka hasa hasa vijana wa kike.

Tatu kwa vijana wenyewe

Bado vijana hatuutazami mpira kama kazi na kuweka nguvu na ari zote huko na kufanikiwa kupitia soka, Hivyo inakuwa ni vigumu zaidi kufanikiwa na kucheza nchi za nje katika soka la kulipwa.

Uhaba wa vituo vya kulelea vipaji vya soka ( shule za vipaji maalum )

Upungufu wa shule hizi maarufu kama "academy" inakuwa vigumu zaidi kwa vijana kufahamu mpira vizuri na kupata malezi bora ya kisoka kufikia ndoto zao za kucheza soka la kulipwa nje ya inchi.

Ubora wa viwanja vyetu vya ndani

Hii inakuwa changamoto kubwa katika kutimia kwa ndoto za vijana wengi kwani viwanja vyetu vingi havina nyasi bora ( iwe bandia au asili ) na miundombinu nyingine kama taa,viti ,nakadhalika, Hivyo inawawia vigumu sana vijana kutoboa kwani hata timu za nje zinapotaka kuwasajili zinaona bora kuwaacha.

Nafasi ya timu yetu ya taifa katika msimamo wa kidunia

Timu nyingi hasa kutoka ukanda wa maghalibi ( Ulaya na Asia ) hupenda sana kuangalia kigezo hiki na kuamua kuwaacha vijana wengi wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kwani nafasi yetu huko hairidhishi sana.

Pamoja na changamoto hizi bado kuna vijana wachache wanatoboa na kucheza huko kwa juhudi zao na kutokata tamaa kama vile Mbwana Samata, Simoni Msuva ,Kinda Kelvin John, na wengineo.
 
Upvote 2
kweli ndugu ndoto za kina Ronaldo na Lionel messi wetu zinaishiaga kwenye tafakali zetu tu .
 
Back
Top Bottom