Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,833
- 8,777
Vikwazo maana yake ni kutengwa na mataifa katika nyanja mbalimbali
Vikwazo ni hatari sana,ni janga na vinatesa sana.
Kuna aina nyingi sana za vikwazo lkn vikwazo kwa kiuchumi na kisiasa ni hatari kuliko vyote.
-Kuna vikwazo vya nchi moja kuiwekea vikwazo nchi nyingine,mfano Marekani kuiwekea nchi moja
Ndugu zangu vikwazo vinatesa sana.
Nchi ikiwekewa vikwazo vya kiuchumi ni balaa kuliko vikwazo yote.
Maana nchi hairuhusiwi kuuza wala kununua bidhaa kwa ajili ya maendeleo kwa mfano huruhusiwi kuuza bidhaa za kiwandani,mashambani na madini na bidhaa kama mafuta.
Vikwazo hivi huua uchumi wa nchi kwa haraka sana
Maana nchi moja inahitaji kuuza bidhaa ili iweze kununua bidhaa za mahitaji ya nchi.
mfano inahitaji kuuza:
madini,mazao yatokanayo na kilimo,bidhaa za viwandani n.k
Ili kupata fedha,hususan fedha za kigeni kwa ajili ya kununua bidhaa isizozalisha,kama baadhi ya vyakula,madawa ya binadamu na wanyama, mitambo,mashine,vifaa vya hospitali,silaha na vitu vingine vyote muhimu kwa Matumizi ya serikali na raia.
Ukiwekewa vikwazo vya kiuchumi hutoboi.
Nchi kubwa wenye historia kubwa,ujuzi mkubwa,elimu,uzalendo,sayansi, teknolojia,utajiri wa rasiliamali na Kila aina,utalii, tunu muhimu za Taifa kushinda mataifa mengine zilizowekewa vikwazo vya kiuchumi ziliyumba vibaya sana.
Sasa tuangalia mfano.
Cuba,Iran,Korea kaskazini, south Afrika, Zimbabwe, Russia n.k
Nchi hizi niliwekewa vikwazo kwa nyakati tofauti.
Sasa tuangalie akili,uwezo na maarifa waliyonayo nchi hizi,tuangalie nani kati Yao vikwazo havijamuathiri,ana uwezo wa kuvikabili,anauwezo wa kujitegemea tulinganishe na sisi Tanzania kama tukiwekewa vikwazo kama walivyiwekewa wenzetu je tutaweza kutoboa?
Tuangalie viongozi wetu,kama wanaweza kutuvusha,kwa kuangalia uwezo wao wa kubuni mbinu za kiuchumi za kutuvusha,kwa kuangalia akili zao,maarifa Yao,ubunifu wao,uzalendo wao na utashi wao.
Kumbuka hata kama nchi inauwezo wa kuzalisha namna Gani haitaruhusiwa kuuza bidhaa Nje ya nchi.
Na hata kama ina pesa kiasi Gani haitaruhusiwa kununua bidhaa kutoka Nje ya nchi.
Itanyimwa misaada ya kijamii na kimaendeleo.
Hakuna ujenzi wa Barbara,shule, hospital n.k kutokana na pesa ya wafadhiri.
Vikwazo vya kidiplomasia.
Viongozi wetu na hata familia zao hawataruhusiwa kuingia katika nchi au jumuiya zilzotuwekea vikwazo,
Mabalozi wao wataondoka,yaanibwatafunga Balozi zao na sisi wa kwetu watafukuzwa kwao.
Vikwazo ni kama vile mtu alieshikwa na nyoka mkubwa kama vile Anakonda au chatu.
Nyoka hawa akikuzunguka kadri unavyotaka kujitoa ndivyo anavyozidi kukubana,ukiwa mpole nae anatulia,ukipambana anaongeza mwisho wa siku unakufa haraka.
Kwa Nini nimetoa mfano huu.
Kwa kadri nchi iliyowekewa vikwazo ikiongeza kiburi na vikwazo vikali vinaongezwa.
Kwa mfano ukiwekewa vikwazo vya kutosafiri kwao,ukijifanya hujali,wanaweka vikwazo vya kiuchumi,ukijifanya hujali wanaweka vikwazo vya raia wako kutokwenda kwao,ukikaidi,wanazuia,Mali na fedha za nchi na viongozi,zilizoko kwao.
Kwa hiyo wanakua wanaongeza mbinyo hatua kwa hatua Hadi utakapokosa pumzi na hatinae kufa.
Nchi zilizowekewa vikwazo Zina maisha magumu sana ndugu zangu,uchumi unaanguka kabisa,maisha ya raia yanakua ya shida ,machafuko yanaanza, vurugu,mizozo na Kila aina ya taharuki inaikumba nchi.
Vitu vinaoanda bei,biashara za watu zianaanguka,maendelea yanasimama,nchi inafilisiaka na Kila aina ya shida.
Je sisi tuna viongozi kama akiana Fidel Castro, Vladimir Putin,Kim I'll sung,Kim jong UN, Ayatollah khomenei, Ayatollah khamenei,
Kumbukeni South Afrika maji yaliwafika shingoni akaja Fredrick De Clerk kuokoa jahazi,
Robert Mugabe maji yalimshinda akalala mbele.
Je ni sababu Gani nchi yetu iwekewe vikwazo?
Je Sababu inayopelekea tuwekewe vikwazo Ina umuhimu Gani kwa nchi?
Je kama nchi tuna maslahi Gani tunayalinda yanayopolekea kukubali hata tukiwekewa vikwazo ni sawa TU?
Je ni kwa sababu za uzalendo wetu tuko radhi ukiwekewa vikwazo?
Tuangalie nchi zilizowekewa vikwazo hapo juu sababu zao za kuwekewa vikwazo, zinalingana na sababu ambazo zitapelekea sisi kuwekewa vikwazo?
Tutafakari!?!?!

- Kuna vikwazo vya nchi kadhaa kuiwekea nchi moja,mfano EU + USA kuiwekea nchi moja
- Kuna vikwazo jumuiya za kimataifa kuiwekea vikwazo nchi moja,mfano UN, AU, Commonwealth,SADEC n.k