VIKWAZO: Piga nikupige ni mchezo wa haki

VIKWAZO: Piga nikupige ni mchezo wa haki

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111334315970.jpg
Inasemekana kuwa, hata paka mpole anaweza kupambana kwa nguvu anaposukumwa kwenye kona. Hilo pia ni sahihi kwa binadamu, kwani hata wale wanaoonekana kuwa ni waoga, wanaweza kushambulia katika njia zisizotegemewa ili kulinda maslahi yao na uhai wao.

Katika miaka kadhaa iliyopita, nchi za Magharibi zimekuwa zikitoa lawama za kila aina dhidi ya China katika mkakati unaolenga kuvuruga utulivu wa kisiasa na kijamii nchini humo. Ilimchukua aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump kutimiza mipango hiyo, akianza na kuchochea vita ya kibiashara kutokana na madai ya kodi za juu zisizo za haki zinazodaiwa na China kwa bidhaa zinazotengenezwa Marekani.

Trump aliondoka madarakani Januari mwaka huu, akicha njama ya kuvuja kwa virusi katika Maabara ya Virusi ya Wuhan ambayo inalaumiwa kuwa chanzo ya virusi vya Corona. Pia alianzisha tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu katika mkoa wa Xinjiang, na kudai kuwa serikali ya China inafanya mauaji ya kimbari ya jamii ndogo ya waislamu wa kabila la Uyghur.

Ni juhudi za pamoja zinazoratibiwa vizuri, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zimejitenga na kampuni za China na kuweka adhabu ya vikwazo katika maeneo kadhaa ya kidiplomasia na maslahi ya kibiashara kama njia ya kuadhibu makossa ya kufikirika. Wakati wote huo, China imechukulia masuala hayo kinidhamu, ikijitahidi kufafanua nafasi yake wakati mvutano na uchochezi vikiongezeka kutoka upande mwingine.

Inaonekana kwamba China haiwezi kuvumilia zaidi, na imechoshwa na daima kuwekwa kwenye nafasi ya kujitetea. Wakati wa Mikutano Miwili iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu, washiriki kutoka sehemu mbalimbali walipendekeza kuwa China iunde sheria maalum ya kujibu vikwazo vya kigeni ili kutoa uungaji mkono wa kisheria ili kujibu hatua zozote za adhabu zinazotolewa na nchi za kigeni.

Vilevile, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) hivi karibuni ilipitisha sheria ya kujibu vikwazo vinavyowekwa na nchi za kigeni. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Li Zhanshu, lengo la sheria hiyo ni kutoa uungaji mkno wa kisheria ili kujibu vitendo vya nchi moja kuwa juu ya nchi nyingine na siasa za kimabavu, pia kulinda maslahi ya China na watu wake.

Pamoja na hatua nyingine muhimu zinazoonekana kufaa, sheria hiyo mpya inaelekeza aina tatu za majibu. Kwanza ni kukataa kutoa visa, kuzuia kuingia China, kufuta visa, na kufukuzwa nchini. Aina ya pili ni kuzuia, kufunga na kushikilia vitu vinavyohamishika na visivyohamishika na aina nyingine za mali zilizoko nchini China. Na aina ya mwisho, ni kuzuia kufanya mabadilishano ya aina yoyote na mashirika au watu binafsi.

Kimsingi, sheria hiyo inaelekeza kuwa, mashirika ama watu binafsi wanaohusika na utekelezaji wa hatua za kinidhamu dhidi ya wananchi wa China au taasisi, wanaweza kuwekwa kwenye orodha ya vikwazo inayotolewa na idara ya serikali ya China, na hii inaweza kuwafikia mameneja na wasaidizi wa, ikiwemo wanafamilia.

Zaidi ya hayo, wale walioko kwenye orodha nyeusi wanaweza kukataliwa kuingia China au kufukuzwa nchini humo, mali zao ndani ya China zinaweza kuzuiwa, na wanaweza kuzuia kufanya biashara nchini China.

Kampuni za kigeni zikizoko nchini China zinapaswa kufanya marekebisho ama kuondoka nchini humo, kwani si rahisi kung’ata mkono unaokulisha na kutarajia mkono huohuo uendelee kukulisha! Kuunga mkono vikwazo ni kitendo cha njama ambacho hakuna nchi inaweza kuvumilia.

Haipendezi kabisa kuharibu uchumi uliojengwa kwa maumivu makubwa kwa miaka 40, ambao ni muda tangu China ilipotangaza “Sera ya Mageuzi na Kufungua Mlango”.

Sheria hii inapaswa kuzishawishi nchi nyingine zinazohisi zinalengwa isivyo halali na vikwazo kusimama na kutetea haki zao. Hakuna nchi yenye mamlaka ya kimaadili kutoa hukumu dhidi ya nchi nyingine katika masuala yanayogusa mambo ya ndani ya nchi husika. Wale wanaotoa vikwazo wanapaswa pia kuhukumiwa kwa vigezo vivyo hivyo wanavyotumia kuhukumu wengine.

Akijibu kama sera hiyo haitakuwa kikwazo kwa mageuzi na ufunguaji mlango wa China, ofisa mmoja kutoka Tume ya Masuala ya Sheria iliyo chini ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China amesema, kihalisi, sheria hiyo itakuwa nafuu kwa juhudi za China. Amesema dhamira ya China na utayari wake wa kufanya mageuzi ya kina, kufungua mlango zaidi na kulinda mamlaka yake, usalama na maslahi ya kimaendeleo bado iko imara.
 
Back
Top Bottom