Kuanzia Januari 1, 2026 saa 6:01 usiku kwa saa za Marekani Mashariki (EST), kufuatia Tamko la Rais namba 10998 kuhusu “Kuzuia na Kudhibiti Uingiaji wa Raia wa Kigeni kwa Lengo la Kulinda Usalama wa Marekani,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasitisha kwa sehemu utoaji wa visa kwa raia wa nchi 19 – ambazo ni: Angola, Antigua na Barbuda, Benin, Burundi, Cote D’Ivoire, Cuba, Dominica, Gabon, Gambia, Malawi, Mauritania, Nigeria, Senegal, Tanzania, Togo, Tonga, Venezuela, Zambia, na Zimbabwe.
Usitishaji huu unahusu visa za wageni wa muda mfupi za aina ya B-1/B-2 (ziara na biashara), pamoja na visa za wanafunzi na wanaobadilishana kielimu (F, M, J), pamoja na visa zote za uhamiaji – isipokuwa kwa wachache waliotajwa hapa chini:
- Visa za uhamiaji kwa wachache wa kikabila na kidini wanaokumbwa na mateso nchini Iran
- Raia wenye uraia wa nchi mbili wanaotuma maombi kwa kutumia pasi ya kusafiria ya nchi isiyohusika na marufuku
- Visa Maalum za Uhamiaji (SIVs) kwa wafanyakazi wa serikali ya Marekani chini ya kifungu 8 U.S.C. 1101(a)(27)(D)
- Washiriki wa baadhi ya mashindano makubwa ya michezo
- Wakazi wa Kudumu wa Kisheria (Green Card holders)