Vikwazo vya Marekani: Huawei yatangaza kuacha kutengeneza simu za viwango vya juu, flagship phones

Hii ni habari mbaya sana kwa wapenda technology, maana huawei alikuwa anatoa simu kali sana kuanzia muonekano mpaka camera. Nimesikitisha sana hata ulipokuwa ukitazama reviews ilikuwa mara nyingi wana compare samsung huawei na iphone na huawei alikuwa kwenye specifics nyingi anaibuka kidedea
 
Kwamba wewe mjuaji kuliko Huawei?
 
Usihofu mkuu, Marekani kakumbuka shuka wakati kumekucha, mchina ameshakuwa mjanja tayari, tofauti na miaka ile, huawei itayumba kwa muda, lakini haitakufa...

Kwa dunia ya sasa Marekani ni ngumu yeye peke yake kutawala masoko makubwa yote, kwenye silaha za kivita anapata upinzani kwa urusi, technolojia licha ya mchina nchi nyingi zimepiga hatua sana,, ndege za abiria kuna AIR BUS, kwa dunia ya sasa anachofanya USA, ni kwamba anawafanya adui zake wabuni njia mbadala, sasa hivi kuna nchi zinafikiria kuachana na matumizi ya us dollar, OS za computer hawatumii windows, RUSSIA ana internet yake kama backup iwapi Ulaya/USA watamzingua..
 
Marekani anachezewa akili, muda wowote atashangazwa na Hauwei. Ogopa sana adui anaposema wazi kwamba ameshindwa huku bado kuna walakini.
 
Kama mtu amegundua 5g atashindwaje kutengeneza hizo chipset? Au unadhani huawei ni kama serikali ya viwonder?
 
Unajua kwamba ZTE ni kampuni ya china iliokufa kwasababu ya kuwekewa vikwazo??
 
Taarifa yako inasema Huawei anaacha kutengeneza flagship phones. Ila link uliyoweka inasema kwamba Huaweji anaacha kutengeneza flagship chipsets

Tumuamini nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…