Vikwazo vya Marekani: Huawei yatangaza kuacha kutengeneza simu za viwango vya juu, flagship phones

Vikwazo vya Marekani: Huawei yatangaza kuacha kutengeneza simu za viwango vya juu, flagship phones

Mleta mada tofautisha flagship chipset na flagship smartphone.

Huawei walikuwa wanapata flagship chipset kutoka kwa Taiwanese Semiconductors Manufacturing Corporation (TSMC) ambao ndio the best duniani. Pia walikuwa wanapata baadhi ya components ili watengeneze processors zao za Kirin lakini TSMC watasitisha kuiuzia Huawei kwa kuwa Marekani imetaka kampuni zinazotumia tech yake zisifanye kazi na Huawei labda kwa ruhusa. Hapa hata US hana teknolojia ya maana ya foundry, kina Samsung na TSMC ndo wababe. Kina Qualcomm na Intel Wamarekani ndo wanakuja nyuma.

Huawei kuona hivyo walifanya order ya chipset za kutosha simu millioni 15 tena hizi Huawei Mate 40 ambazo ndo simu za kwanza kutumia 5nm processor. Hata iPhone 12 itazikuta zishatangulia kuwa nayo. Simu nyingine zisizo high end watatumia technology yao kutenegeneza, hawashindwi kutengeneza 16nm. Pia wako bize mno kwenye maabara zao kuibuka na breakthrough. Kwangu mimi teknolojia ya Mchina nasubiri kuipima hapa.

Huawei hafi leo wala kesho. Kwenye soko la China labda serikali inaweza fanya kina Xiaomi, Oppo, OnePlus wauze sana nje kisha waiachie Huawei ijipange upya uku inapokea order za ndani. Baada ya kujipanga itoe product nje.

Huawei ana patents nyingi zaidi za 5G kuliko kampuni yoyote. Akifungiwa kutoa huduma makampuni yatakayotoa yatalipia patent yake. Hapa wanaweza pata kiasi cha kawaida cha pesa.
Tech ya chipset inabadilika Kila Siku , huwezi ku stock chipset kwa ajili ya matumizi ya baadaye .
Umeongea kishabiki Hadi unasahau facts
 
Kwahiyo wewe hili unalifurahia et.
Afurahie au anunie, tuwe na desturi ya kuongea facts, ndio maana ya forum na tutaitendea haki hii forum kwa vizazi vijavyo

Tukianza kuongea vitu kwa kupendelea upande, forum hii haitakuwa na maana kwa vizazi vijavyo.
 
Marekani ni ngumu kuua kampuni ya kichina kwenye soko la China. Huawei ametishia soko la dunia kwa kuwekeza kwenye teknolojia nyingi, anagusagusa tu. Sioni kama Huawei atatoa Harmony OS hata mwakani kwa kuwa Nokia, Samsung na Microsoft walishindwa. Lakini sioni kwa vipi Huawei ataondoka sokoni kiurahisi hivi.

Makampuni kama kina Siemens na Ericcson yalijikita kwenye sehemu tu ya teknolojia ya mawasiliano. Tatizo Huawei anagusa kotekote. Hili ni tatizo kwa Marekani ambao waliifanya Toshiba ya Japan ilitolewa kwenye soko sembuse kampuni ya adui Mchina. Bombardier ya Canada wametolewa kwenye soko la ndege kwa kutishia mauzo ya Boeing.
Bombardia haikuwahi kutishia Boeing kwenye masoko ,
Airbus aliona fursa kwa bombardia c series , ndo akanunua program hiyo ili atrngeneze ndege hizo kwenye kiwanda chake Alabama states (.A220)

C series isingeweza kupenya kwenye soko la marekani Kama ingeendelea kutengenezwa Canada , sababu ya Kodi kubwa.
 
Taarifa yako inasema Huawei anaacha kutengeneza flagship phones. Ila link uliyoweka inasema kwamba Huaweji anaacha kutengeneza flagship chipsets

Tumuamini nani?
Kama unafatilia vizuri flagship phones hutengenezwa na flagship chipset, kwa hiyo Kama anaacha kutengeneza chipset maana yake ni kuwa simu za flagship nazo zinakufa
 
Tech ya chipset inabadilika Kila Siku , huwezi ku stock chipset kwa ajili ya matumizi ya baadaye .
Umeongea kishabiki Hadi unasahau facts
Tuliza akili ukileta ubishi. Simu hutumia chipset ya aina moja unless kama ina version tofauti. Na penyewe si kawaida makampuni kutengeneza version zenye chipset tofauti. Mfano utakuta iPhone 12, 12 Pro au 12 Pro Max zinatofautiana storage, camera, screen to body ratio, battery, etc lakini chipset ni moja.

Huawei waliagiza chipset around 15M kwa kutoshea simu za Mate 40. Production ya high end flagship always huwa ni mwaka mmoja. Baada ya hapa watatakiwa watengeneze nyingine.

Unabisha nini, na ushabiki uko wapi nilipoandika?
IMG_20200811_123208.jpg
 
Bombardia haikuwahi kutishia Boeing kwenye masoko ,
Airbus aliona fursa kwa bombardia c series , ndo akanunua program hiyo ili atrngeneze ndege hizo kwenye kiwanda chake Alabama states (.A220)

C series isingeweza kupenya kwenye soko la marekani Kama ingeendelea kutengenezwa Canada , sababu ya Kodi kubwa.
Bishana na Boeing wenyewe sasa. Unasema Bombardier alitozwa tarrifs kubwa. Kwani chanzo cha hizo tarrifs kuwa za juu ni nini?

Boeing aliona soko lake linapotea, for your information Delta Airlines ni mojawapo ya wateja watiifu sana wa Boeing. Tena wapo Marekani kwenyewe sasa imagine hao wameopt Bombardier, wengine itakuwaje?

Boeing alifika mamlaka za US kulalamika na ndipo tarrifs zikaongezwa. Baada ya hapo Bombardier akashindwa uza ndege ndipo akauza program kwa Airbus. Airbus haiwezi wekewa tarrifs kwa kuwa tiyari ni giant. Hata hawa kina Embrael wanavutiwa muda.
IMG_20200811_124545.jpg
 
Bishana na Boeing wenyewe sasa. Unasema Bombardier alitozwa tarrifs kubwa. Kwani chanzo cha hizo tarrifs kuwa za juu ni nini?

Boeing aliona soko lake linapotea, for your information Delta Airlines ni mojawapo ya wateja watiifu sana wa Boeing. Tena wapo Marekani kwenyewe sasa imagine hao wameopt Bombardier, wengine itakuwaje?

Boeing alifika mamlaka za US kulalamika na ndipo tarrifs zikaongezwa. Baada ya hapo Bombardier akashindwa uza ndege ndipo akauza program kwa Airbus. Airbus haiwezi wekewa tarrifs kwa kuwa tiyari ni giant. Hata hawa kina Embrael wanavutiwa muda.View attachment 1533939
Na hili ndo soko huria wanalotuhubiria kila siku wanalotaka na waafrica nao walifate.
 
Mungu anaisamehe ila nawachukia wachina sanaaaa...! Acha tu wapate tabu sana,Hawana Utu

Wachina ni watu wazuri sana kuliko marekani

Marekani ni killers hivyo sioni wema wao, waliuwa innocent people zaidi ya laki mbili huko japan, haikutosha akasababisha mataifa mawili yapigane Iraq na Iran na kupelekea kupoteza maisha zaidi ya milioni 3, haikutosha huko huko iraq, afghanistana, yemen, syria n.k. sasa wanachokipata sasaiv kwa covid ni haki yao, na itaendelea kuwapukutisha mpaka basi.
 
Back
Top Bottom