Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

"katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.”

Kipindi kirefu ni muda gani? Inahitajika specific estimates kwa ajili ya kupima usahihi.
Ukiachana na biashara yakimataifa
Hem fafanua hio sentena yako MKUU kama hutojali

Sent using Jamii Forums mobile app
 

your sound is Loudly and Clear
 
Halafu hawa propagandalist ndo wapo mstari wa mbele kujitekenya wakifikiri dunia nzima ni matahila
 
Kwa yoyote aliyesoma Marketing, Economics n.k atakubaliana na hii ripot, kuanzia mwanzo w Ripot mpaka mwisho unaona kabisa waandishi walivyoandaa kisomi na kujenga hoja zenye nguvu.
 
Russia imefika ngapi?

Data za Nchi za magharibi si kila siku unazisoma mtandaoni, kuhusu uchumi wa Russia unapata taafifa zake kutoka ktk sources mbalimbali kama hao wa Ulaya na Magharibi?
 
Nakubaliana na wewe, kwa pini alopigwa Russia sio rahisi uchumi wake kubaki imara kama ambavyo wanavyotudanganya.

Kampuni za Ulaya zilikuwa na ajira laki mbili kwa Warusi. Kampuni zaidi elfu moja zimeondolewa, bado nchi imepunguza mapato yake kupitia chanzo kikuu cha mapato ambayo ni Gas na Mafuta, na bado mtu anakwambia jamaa hawajatetereka.

Fikiria tu Tz hapa tuambiwe Utalii upigwe pini pamoja na sekta ya madini au Bandari, unafikiri tuna nini tena hapo?

Narudia tena, tunasema Ulaya inataabika kwa mfumuko wa bei kutokana na wao kuachilia huru vyombo vya habari, laiti Russia wakifungua vyombo vha habari viwe huru hapatashikika.
 
Utafika wakati tutaanza kuuona moshi, hapo ndipo tutaona moto unaofukuta chini ktk nchi ya Urusi. Ukiondoa ushabiki, kwa vikwazo vya Russia, hawezi kubaki salama kiuchumi.

Na atakuwa anapita ktk hali ngumu mno, tusisahau kuwa fedha za wafanyabiashara wa Urusi, mali zao n.k ambazo vipo Ulaya na America, vyote vimepigwa pini.
 
Inasemekana imepungua kwa zaidi ya 80% huo utengenezaji wa magari.

Hii ya ruble kupanda dhidi ya dollar waliizungumza mno kipindi cha mwezi wa tatu hivi.
 
Hiki ndicho kipindi ambacho Russia anatafuta mno washirika. Mbaya zaidi US yupo macho kila eneo.
Russia anatafuta ushirika na nchi kama Uganda [emoji848] hii Hali inafikirisha sana , maana urusi Kwa kipindi kirefu hanaga mda na mataifa ya Africa.., wanaweza kutuficha takwimu, lakini matendo yenyewe ni ushindi tosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…