Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

"katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.”

Kipindi kirefu ni muda gani? Inahitajika specific estimates kwa ajili ya kupima usahihi.
Ukiachana na biashara yakimataifa
Hem fafanua hio sentena yako MKUU kama hutojali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vikwazo alivyowekewa urusi hawezi kufanya vizuri kiuchumi asilani , kabla ya vikwazo russia alikuwa anapitwa na nchi kama india . Uchumi wa urusi uko hoi long time kitambo na ni sababu mojawapo iliyopelekea ussr kuvunjika na ashukuru Mungu kaijaalia gesi na mafuta vinginevyo ingekuwa tunaongea mengine na ndiyo maana urusi haina ushawishi wa maana kwa wenzake wa ulaya mashariki maana haina hela. Hata russians wenyewe hutaman waende west. Angalia hata waliosoma russia wengi lazima utakuta wa mahangaiko fulani hivi kwenye maisha sasa angalia waliosema western wengi hawana hayo mahangaiko e.g. rip Dr. Mengi vs rip Dr. Shika. Putin kaenda omba msaada wa drones iran na kupata uzoef wa kuuza bidhaa na huduma kimagendo kukwepa vikwazo vya western sasa ka nchi imefikia hatua hii kwa nini kiuchumi wasiwe hoi bin taaban?

your sound is Loudly and Clear
 
Wanajitekenya na kicheka wenyewe,ukweli duniani kote unafahamika kuwa Urusi amesababisha mdororo wa kiuchumi duniani note.Nchi zilizoathirika zaidi ni EU na USA kuliko hata Urusi yenyewe,mfano USA inflation rate imefika 9.1% kiwango ambacho hakijawahi kutokea toka miaka 40 iloyopita.

Huko Uingereza na Germany inflation zimetoka 1.2% hadi 8%,kiwango ambacho hakijawai kufikiwa kwa miaka mingi.koifupi Urusi amewashika korodani.
Halafu hawa propagandalist ndo wapo mstari wa mbele kujitekenya wakifikiri dunia nzima ni matahila
 
Kwa yoyote aliyesoma Marketing, Economics n.k atakubaliana na hii ripot, kuanzia mwanzo w Ripot mpaka mwisho unaona kabisa waandishi walivyoandaa kisomi na kujenga hoja zenye nguvu.
 
Wanajitekenya na kicheka wenyewe,ukweli duniani kote unafahamika kuwa Urusi amesababisha mdororo wa kiuchumi duniani note.Nchi zilizoathirika zaidi ni EU na USA kuliko hata Urusi yenyewe,mfano USA inflation rate imefika 9.1% kiwango ambacho hakijawahi kutokea toka miaka 40 iloyopita.

Huko Uingereza na Germany inflation zimetoka 1.2% hadi 8%,kiwango ambacho hakijawai kufikiwa kwa miaka mingi.koifupi Urusi amewashika korodani.
Russia imefika ngapi?

Data za Nchi za magharibi si kila siku unazisoma mtandaoni, kuhusu uchumi wa Russia unapata taafifa zake kutoka ktk sources mbalimbali kama hao wa Ulaya na Magharibi?
 
Urusi
Kwa vikwazo alivyowekewa urusi hawezi kufanya vizuri kiuchumi asilani , kabla ya vikwazo russia alikuwa anapitwa na nchi kama india . Uchumi wa urusi uko hoi long time kitambo na ni sababu mojawapo iliyopelekea ussr kuvunjika na ashukuru Mungu kaijaalia gesi na mafuta vinginevyo ingekuwa tunaongea mengine na ndiyo maana urusi haina ushawishi wa maana kwa wenzake wa ulaya mashariki maana haina hela. Hata russians wenyewe hutaman waende west.

Angalia hata waliosoma russia wengi lazima utakuta wa mahangaiko fulani hivi kwenye maisha sasa angalia waliosema western wengi hawana hayo mahangaiko e.g. rip Dr. Mengi vs rip Dr. Shika. Putin kaenda omba msaada wa drones iran na kupata uzoef wa kuuza bidhaa na huduma kimagendo kukwepa vikwazo vya western sasa ka nchi imefikia hatua hii kwa nini kiuchumi wasiwe hoi bin taaban?
Nakubaliana na wewe, kwa pini alopigwa Russia sio rahisi uchumi wake kubaki imara kama ambavyo wanavyotudanganya.

Kampuni za Ulaya zilikuwa na ajira laki mbili kwa Warusi. Kampuni zaidi elfu moja zimeondolewa, bado nchi imepunguza mapato yake kupitia chanzo kikuu cha mapato ambayo ni Gas na Mafuta, na bado mtu anakwambia jamaa hawajatetereka.

Fikiria tu Tz hapa tuambiwe Utalii upigwe pini pamoja na sekta ya madini au Bandari, unafikiri tuna nini tena hapo?

Narudia tena, tunasema Ulaya inataabika kwa mfumuko wa bei kutokana na wao kuachilia huru vyombo vya habari, laiti Russia wakifungua vyombo vha habari viwe huru hapatashikika.
 
Hili liko wazi sana, hata kama bahadhi ya members humu kila siku wanatuletea riport ndefundefu kila siku kuonnyesha kuwa urusi mambo yako shwari.., huwezi ukatengwa na mataifa makubwa yenye nguvu kiuchumi alafu eti usipate madhara yoyote,Hilo haliwezekani hata ikitokea washirika wa marekani wakaungana kwa dhati bila kujari madhara yatakoyowapata,na wakaamua kumtenga marekani, usitegemee kumuona Amerika akiendelea kuwa super pawer
Ninachokiona hapa ni serikali ya urusi kuendelea kupika takwimu huku ikifunga mlango kwa yeyote mwenye mawazo tofauti na klemlin!
Utafika wakati tutaanza kuuona moshi, hapo ndipo tutaona moto unaofukuta chini ktk nchi ya Urusi. Ukiondoa ushabiki, kwa vikwazo vya Russia, hawezi kubaki salama kiuchumi.

Na atakuwa anapita ktk hali ngumu mno, tusisahau kuwa fedha za wafanyabiashara wa Urusi, mali zao n.k ambazo vipo Ulaya na America, vyote vimepigwa pini.
 
Russian ruble is the worst performing currency of the emerging economies against USD. Imeshuka 16% mwezi huu baada ya kupanda ghafla mwezi May. Ruble ina fluctuations kali na haiko stable, haitabiriki kabisa.

Utengenezaji wa magari nchini Russia umepungua capacity zaidi ya nusu, components muhimu from European countries hazipatikani
Inasemekana imepungua kwa zaidi ya 80% huo utengenezaji wa magari.

Hii ya ruble kupanda dhidi ya dollar waliizungumza mno kipindi cha mwezi wa tatu hivi.
 
Hiki ndicho kipindi ambacho Russia anatafuta mno washirika. Mbaya zaidi US yupo macho kila eneo.
Russia anatafuta ushirika na nchi kama Uganda [emoji848] hii Hali inafikirisha sana , maana urusi Kwa kipindi kirefu hanaga mda na mataifa ya Africa.., wanaweza kutuficha takwimu, lakini matendo yenyewe ni ushindi tosha
 
Back
Top Bottom