Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Vikwazo vyaathiri uchumi wa Urusi

Kupanda mchongoma Kushuka ndio Ngoma. Wachinjaji walienda Machinjioni kuchinja Ngombe walipo fika wakakuta Ngombe wameshika Visu na Kuwasubiri wachinjaji.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha YALE nchini Marekani wanasema uchumi wa Urusi unakabiliwa na uharibu mkubwa kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi, licha ya Moscow kupuuzia athari hizo.

Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa kazi yao inatilia mashaka madai ya Moscow kuwa uchumi wake bado uko imara na kuwa nchi za Magharibi zinaumia Zaidi kupitia kile kinatajiwa kuwa ni "vita vya kuzorota uchumi.”

Utafiti huo wasemaje?

Timu ya watalaamu wa Yale ilitumia data ya watumiaji bidhaa na takwimu kutoka washirika wa kimataifa wa kibiashara na usafirishaji bidhaa wa Urusi, kupima shughuli za kiuchumi miezi mitano baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini UKRAINE [emoji1255]

Waligundua kuwa msimamo wa Urusi kama muuzaji wa bidhaa ng'ambo umeyeyushwa kabisa, baada ya kulazimika kugeuka kutoka kwa masoko yake makuu barani Ulaya kuelekea Asia..

Utafiti huo unasema uingizaji wa bidhaa nchini Urusi umeporomoka tangu vita vilipoanza, na nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za kununua pembejeo, vipuri na teknolojia.

Timu hiyo iligundua kuwa uzalishaji wa ndani wa Urusi umekwama kabisa na haina uwezo wa kujaza nafasi za biashara zilizoanguka. Watayarishaji wa ripoti hiyo wanasema hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa na hasira ya watumiaji.

Nchi zaMagharibi zimeiwekea Urusi vikwazo. Huku kukiwa na karibu kampuni 1,000 za kimataifa zilizofunga milango yao nchini humo, Urusi imepoteza kampuni ambazo zinawakilisha karibu asilimia 40 ya patojumla la ndani kwa mujibu wa utafiti huo.

Ripoti hiyo imesema Putin anaingilia kati kwa kutumia njia isiyo endelevu ya kifedha ili kuficha mapungufu ya muundo wa kiuchumi.

Iliongeza kuwa bajeti ya serikali ya Urusi imetumbukia katika nakisi kwa mara ya kwanza na fedha za Kremlin zipo katika hali ngumu mno kuliko inavyoeleweka kawaida.

Wakati huo huo, watafiti hao wamesema masoko ya kifedha ya Urusi – wakiweka jicho kwa utabiri wa usoni – ndio yanayofanya vibaya Zaidi ulimwenguni, hali inayopunguza uwezo wa kuvutia uwekezaji mpya wa kuufufua uchumi.

"Tangu uvamizi huo, takwimu za kiuchumi za Kremil zimekuwa za kuchaguliwa, kwa kutoa maeneo ambayo hayaonekana kuwa mazuri kwao na kuchapisha tu yanayowafaa” unasema utafiti huo.

Urusi imewekewa vikwazo vya mafuta
Takwimu mpya za uzalishaji wa viwanda wa Urusi kwa mwezi Juni zinaonyesha kuwa iliathirika pakubwa katika sekta nyingi ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa magari, uzalishaji ulipungua kwa asilimia 89 wakati kwa nyaya za mawasiliano ulishuka kwa karibu asilimia 80. Nini kinachofuata kwa uchumi wa Urusi?

Waandishi wa utafiti wa Yale walisema Urusi haina mbinu ya kujiondoa katika janga hilo la kiuchumi kama washirika wa Magharibi wataendelea kuungana kuhusu vikwazo.

Utafiti tofauti wa Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama uliochapishwa Juni pia unaashiria kuwa uchumi wa Urusi upo kwenye misukosuko mingi, licha ya kustahimili siki za mwanzo za kutangazwa vikwazo.
"Athari za vikwazo ndio zimeanza tu kushuhudiwa: matatizo ya uzalishaji na usambazaji yanaongezeka na mahitaji yanapungua kwa kasi.” "katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.” Ilisema ripoti hiyo.

Source DW. Aljazeera

=========

NB: Russia kuomba msaaada wa kijeshi IRAN ni ishara tosha.

by the way tutauamini huu utafiti hadi tutakapo pata utafiti mbadala toka russia [emoji635]
Report ya IMF inasema kwamba, uchumi wa Urusi umefanya vizuri tofauti na ilivyotegemewa.
Uchumi wa marekani ndio unapata tabu makampuni yamepoteza billions kwasababu ya kushuka wa dola.
 
Inasemekana imepungua kwa zaidi ya 80% huo utengenezaji wa magari.

Hii ya ruble kupanda dhidi ya dollar waliizungumza mno kipindi cha mwezi wa tatu hivi.
Sio inasemekana. Taarifa za ndani ya Urusi data muda fulani mwezi huu mwanzoni zilionesha uzalishaji wa magari umeshuka kwa 86%, wiki hii kuna data zao zilionesha uzalishaji umeshuka kwa zaidi ya 90% ila chanzo cha ndani ya Urusi kilichoandika sijui credibility yake na sikuona data walizipataje.

Sasa kama hata Lada ambazo ndio gari pendwa nchini Urusi zilikuwa zinatengenezwa chini ya Renault ya Ufaransa unategemea nini. Russian automobile industry ilishakufa zamani hawana innovation wala uwekezaji kwenye new technology, civilian market haitaki uzembe. Ndio maana hakuna ndege za kiraia zilizotengenezwa na Urusi kwenye soko la dunia.

Uzuri wa magari sio magumu sana makampuni ya Ulaya yakiondoka makampuni ya China yanaweza kushika nafasi, changamoto ndogo itabaki kwenye kuhamisha umiliki. Mfano umwambie Renault auze shares zake za AvtoVaz kwa Chinese company. Wakati huo Chinese company ifanye hivyo inajua kuna uwezekano wa sanctions. Kazi ipo
 
Report ya IMF inasema kwamba, uchumi wa Urusi umefanya vizuri tofauti na ilivyotegemewa.
Uchumi wa marekani ndio unapata tabu makampuni yamepoteza billions kwasababu ya kushuka wa dola.
Report ya IMF ya lini. Uchumi wa Urusi hauaminiki kwa wawekezaji, ukishaona sarafu ya nchi inapanda thamani 20% within 2 months na kushuka 20% within 2 months ujue hakuna kampuni serious itaenda kule.

Marekani hata ufanyeje, huwezi fanya USD ikue kwa asilimia zote hizo. Iko stable hata ulete vitisho gani, uchumi wa Marekani hauna tishio walau kufikia lililokuwepo 2020 kwenye peak ya COVID-19
 
Russia anatafuta ushirika na nchi kama Uganda [emoji848] hii Hali inafikirisha sana , maana urusi Kwa kipindi kirefu hanaga mda na mataifa ya Africa.., wanaweza kutuficha takwimu, lakini matendo yenyewe ni ushindi tosha
Kweli bhaana, jamaa wameenda mpaka Uganda, kweli huko hapakaliki. Nahisi mpaka sasa viongozi na wale vibopa wa Russia wanakamua fedha zao mfukoni badala ya hazina ya Taifa. Hawawezi gusa hazina ya Taifa sababu wanajua watauporomosha uchumi kwa kasi sana.
 
Report ya IMF ya lini. Uchumi wa Urusi hauaminiki kwa wawekezaji, ukishaona sarafu ya nchi inapanda thamani 20% within 2 months na kushuka 20% within 2 months ujue hakuna kampuni serious itaenda kule.

Marekani hata ufanyeje, huwezi fanya USD ikue kwa asilimia zote hizo. Iko stable hata ulete vitisho gani, uchumi wa Marekani hauna tishio walau kufikia lililokuwepo 2020 kwenye peak ya COVID-19
Hii france 24 habari ya siku 5 zilizopita, utaipata hata sources nyngne Russia doing better than expected despite sanctions: IMF
 
Hii france 24 habari ya siku 5 zilizopita, utaipata hata sources nyngne Russia doing better than expected despite sanctions: IMF
France24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.

IMF imetabiri uchumi kukua kwa 2.5% mwaka huu ila bado kuna contraction ya 6%. Generally hakuna performance nzuri ya ukuaji, ila kupambana na vikwazo wahusika wanastahili tuzo
 
Lakini Bwana Jo huko US watu hawamwelewi uchumi na inflation imewachanganya
 
Lakini Bwana Jo huko US watu hawamwelewi uchumi na inflation imewachanganya
Hakuna first world country yeyote ambayo wananchi hawalalamiki, they are too much demanding. Mfano kichomuondoa Waziri Mkuu wa Italy ni nini hasa, kinachomuondoa Boris Johson pale UK ni kufanya party kipindi cha COVID-19 wakati kuna sanctions. Sababu ambazo ungekuwa Russia ukazisema unafariki bahati mbaya baada ya kuteleza na kudondoka kutoka dirisha la apartment yako huku mkeo akifariki bahati mbaya hapohapo baada ya kujikaba
 
Kwa hiyo wewe umeona wa kuwaamini ni Wamarekani waliosema Saddam ana silaha za maangamizi...wakakuta hewa tu??
 
Kwa hiyo wewe umeona wa kuwaamini ni Wamarekani waliosema Saddam ana silaha za maangamizi...wakakuta hewa tu??

leta habari unazo ziamini wewe toka kwenye source yako Tuzichambue. si umeona apo wanaume wamejipinda wametoa kitu kimechambuliwa hakina makandokando. leta na wewe this is jamiiforum sio facebook.
 
France24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.

IMF imetabiri uchumi kukua kwa 2.5% mwaka huu ila bado kuna contraction ya 6%. Generally hakuna performance nzuri ya ukuaji, ila kupambana na vikwazo wahusika wanastahili tuzo

source ya hizi data pls
 
Bwana Ewura mbona hueleweki... Huko juu umedai uchumi wa Russia ni mmbaya mno na hakuna kinachoeleweka hapo juu umekuja na hilo la kuwasifia wachumi wa Russia kwa kazi nzuri,. Swali je hizo sifa unazotaka wapewe hao wachumi za kazi nzuri ipi!!!?? Kwa kuufanya uchumi uwe imara au kwa kuudondosha!!!!!????
 
Kuhimili vikwazo tofauti na ilivyotarajiwa na kufanya vizuri kiuchumi hujui tofauti yake? Unashindwa kuelewa context nyepesi.

Ukiwa mahututi ukawekewa hadi mashine ya kupumua, ukakaa wiki mbili ukipambana. Mtu akisema una afya nzuri atakuwa na akili sawasawa? Mtu akisema unaendelea vizuri tofauti na ulivyokuwa na hali mbaya na walivyoogopa kukupoteza hapo haieleweki anamaanisha nini?
 
Uchumi WA Rusia utayumba lakini hautaporomoka kama west walivyotarajia Kwa vikwazo walivyowekewa Rusia ulaya na Marekani walijua Kuwa Rusia hii vita hata kwenda nayo miezi ata mitatu haitafika ata Rudi nyuma ili kulinda uchumi wake Ila matarajio yamekuwa tofautii na Hali ikiendelea ivi kuna hatihati wakalamba matapishi Yao Kwa kuondoa vikwazo walivyoweka wao wenyewe hasa upande WA gesi, mafuta, mbolea,chakula, makaa ya mawe na vipuri hatari za kiuchumi mbeleni ni kubwa snaa Kwa ulaya kuliko Rusia utulivu WA Rusia kwenye kushughulikia ivi vikwazo limekuwa Jambo la faida sana kwao hawakurupuki wanafanya kama hawataki
Ulaya walikuwa wanaiona Rusia kama nchi ambayo walikuwa hawahiitaji kwenye uchumi wao Ila Kwa yanayotokea saivi kwenye chumi zao naisi ni ngumu kuitenganisha ulaya na Rusia
 
Bado naiona CIA fikra zake zipo sawasawa, Russia atavumilia hii hali kwa muda tu. Utafika wakati hatoweza kuvumilia, kuna muda atasitisha ama kupunguza kabisa vita yake huko Ukraine.
 
Bado naiona CIA fikra zake zipo sawasawa, Russia atavumilia hii hali kwa muda tu. Utafika wakati hatoweza kuvumilia, kuna muda atasitisha ama kupunguza kabisa vita yake huko Ukraine.
Malengo yake yakifikiwa wala hatajiweka kwenye hii vita sana akikamilisha eneo ya donesk kulimiliki atapunguza hii operations Kwa asilimia kubwa naona vita kubwa ikienda kupiganwa pale Odessa na inaweza kuchukua ata miezi miwili kama wakiimiliki basi itabaki kuzuia mashambulizi ya Ukrein wengi wanaichukulia Rusia kama pilipili hoho Ila bado ana uchumi imara pamoja na vikwazo vyote walivyopigwa
 
Utafika wakati tutaanza kuuona moshi, hapo ndipo tutaona moto unaofukuta chini ktk nchi ya Urusi. Ukiondoa ushabiki, kwa vikwazo vya Russia, hawezi kubaki salama kiuchumi.

Na atakuwa anapita ktk hali ngumu mno, tusisahau kuwa fedha za wafanyabiashara wa Urusi, mali zao n.k ambazo vipo Ulaya na America, vyote vimepigwa pini.
Wacha na mimi nitie neno hapo mkuu, Vikwazo vya kiuchumi vina mbio mbili.
i, Mbio fupi[ short run ] na
ii, Mbio ndefu[ long run ]

- Kwenye mbio fupi{ short run }, mwanzoni kabisa mwa operation ya kivita ya Urusi nchi Ukraine baada ya Vikwazo kuanza Urusi ilitaka kushindwa Ila baada ya kukaa kwa wachumi wa ndani ya Urusi na kuweka mipango bomba wakaweza kushinda mpaka Sasa mfano kutoka kushuka kwa rubble na kupanda kwake haraka Sana mwezi wa tatu na hii kutokana na rubble Kutumika Sana kwa manunuzi baada ya Bank kuu ya Urusi kuamrisha malipo yote ya ununuzi wa rasilimali kutoka Urusi ni lazima rubble itumike Kama fedha kuu ya manunuzi na hapa umoja wa ulaya uliweza kushindwa na Urusi. Mpaka Sasa tunaona Urusi bado anasimama lakini si kwamba anasimama kwa nguvu Kama awali kabla ya Operation yake ya kijeshi kuanza huko Ukraine la hasha . Ana simama sawa lakini si kwa ubora Kama wa awali.

- Kwenye mbio ndefu{ long run } hapa inahitajika akili nyingi zaidi za wachumi wa Urusi kuliko hata mbio fupi hapa ni mbio za kuweza kuishi na vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu na huku ukivishinda kimoja baada ya vingine . Hapa ndipo unapaswa kujifunza kwa mataifa yaliyowekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu mfano Iran, North Korea walioishi na vikwazo kwa zaidi ya miaka 40+ ujifunze ni wapi wanashinda hivyo vikwazo na ni wapi hivyo vikwazo vinawaumiza vibaya Sana . Ili wewe usifanye makosa Kama ambavyo wanafanya wao kupelekea vikwazo kuwaumiza. Urusi anahitaji wasomi wake wakiuchumi kuumiza vichwa vyao kadiri wawezavyo ili mbio ndefu za kupambana na vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mingi waweze kuvishinda Kama ambavyo Sasa umoja wa ulaya Wana tafuta na kusaini mikataba mbalimbali ya kuuziana rasilimali [ gas, mafuta, makaa ya mawe ] na mataifa mengine ya mashariki ya Kati na Afrika ili kupunguza na Kama ikiwezekana ni kuondokana kabisa na kuitegemea Urusi kwa rasilimali hapa Urusi ni lazima atake asitake lazima azidishe ushirikiano na China, India, Brazil na anapaswa kuongeza washirika kwa mataifa mbalimbali ya Asia yaliyo bora kiuchumi n
ili kuweza kuuokoa uchumi wake na kuweza kushinda vikwazo vya kiuchumi kwa mbio ndefu pasipo kuwaathiri kwa kiwango kikubwa au kutowaathiri kabisa.

* Mwisho wa siku Kama tunakubaliana kuwa vikwazo vya kiuchumi vinawaumiza wao wenyewe ulaya walio viweka pia tunapaswa tuwe tayari kuyakubali matokeo hasi yatayo ikumba Urusi kutokana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa . Iwe ni matokeo hasi ya muda mfupi [ short run ] au matokeo hasi ya muda mrefu [ long run ] maana vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi ni vingi{ rundo } na vikali Sana.

-Ni hayo tu mkuu niliyonayo labda Kama na wewe utaweza kuongeza mengine.
 
Back
Top Bottom