Tetesi: Vikwazo vyanukia kumshinikiza Magufuli aingilie kati ili mshindi atangazwe Zanzibar

Status
Not open for further replies.

afsa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
1,986
Reaction score
1,585
Ni hatareeeeee
 
Attachments

  • 1454220496874.jpg
    1454220496874.jpg
    23.9 KB · Views: 112
  • 1454220581678.jpg
    1454220581678.jpg
    22.4 KB · Views: 128
  • 1454220635971.jpg
    1454220635971.jpg
    29.9 KB · Views: 124
Ikiwa vikwazo vyenyewe ni vya kutokusafiri kwenda ulaya na marekani, wala wasihangaike maana keshajipiga ban mwenyewe.
 
Kwa kawaida uchaguzi huwa unarudiwa sehemu zilizothibitika kuwa na matatizo na sio kufuta uchaguzi wote.
Hii ni kuchezea demokrasia, fedha na muda
 
Ulitaka urudiwe pemba nzima na baadhi ya maeneo ya unguja....ndio uridhike!!
 
Inauma sana kwa vile watakaosota na maisha ni sisi Watanzania wenye kipato cha chini. Siku zote naombea muungano uvunjike tu kwani ukiangalia udogo wa kisiwa cha Zanzibar na athari zitakazotupata wabara hadi nakereka.
 
Unadhani CUF kukataa kushiriki uchaguzi ikitaka matokeo ya zamani yatangazwe inaashiria nini?halafu msidhani kwa kupeleka wana usalama wetu visiwani Zanzibar ndio mtafanikisha azma zenu za kisiasa,mgogoro Zanzibar ukilipuka kwasababu ya ujeuri na tamaa zenu za madaraka ujue na huku Bara hatutanusurika,tutaingia ktk matatizo yale yale wanayopitia Wakenya.Usidhani huu mgogoro ukilipuka utakuwa kama wa Burundi na kuzimwa kwa kutumia Nkurunzinza style. It will be a more catastrophic conflict than you think. Power is nothing compared to the lives of Tanzanians. Msije kutuharibia amani yetu jamani,chonde chonde.
Damu ipi imemwagika na maisha yapi unataka yaokolewe???
 
Mkuu wa majeshi ameongezewa muda mwa mwaka mmoja kwa ajili ya usalama wa zanzibar na si kwa lingine lolote. Marekani na Uk awawezi kuweka vikwanzo vya kiuchumi kwa serekali ya Tanzania kwani CCM ndio wamewapa Uranium na GAS. CUF watabaki kupiga kelele tu.
 
Kwa kawaida uchaguzi huwa unarudiwa sehemu zilizothibitika kuwa na matatizo na sio kufuta uchaguzi wote.
Hii ni kuchezea demokrasia, fedha na muda
Nilitegemea baada ya miezi 2 kupita, Mwenyekiti wa ZEC angeibuka na ushahidi wa kuharibika uchaguzi katika majimbo yote ya Zanzibar.
Kama hakuwa na ushahidi wa kutosha, ilimpasa kuuridhisha umma wa watanzania, dunia na wapiga kura wa Zanzibar japo kwa ushahidi wa kasoro za uchaguzi katika majimbo au vituo vya kupigia kura. Alitakiwa kuweka orodha ya majimbo na vituo vya kupigia kura ambavyo vinakidhi kutamkwa kuwa uchaguzi uliharibika,ulichafuliwa au ulikuwa na kasoro,matatizo ambayo yanaondoa uhalali wa kuitwa uchaguzi huru. Mpaka muda huu ,si Mwenyekiti wa ZEC wala CCM ambao wametoa orodha ya vituo au majimbo husika.

Ni muda sasa, tokea niliposoma habari kuwa uchunguzi wa waliohusika na kuvuruga uchaguzi umekamilika. Hii ina maana ushahidi umekusanywa tayari. Ni kwa nini DPP hajafungua mashitaka ili mahakama nayo iondoe utata na kuridhia au kuupa uhalali "uchaguzi wa marudio"?

Kesi hii ingesikilizwa kwa daharura na kutolewa hukumu "fasta". Au zilikuwa ni mbwembwe tu za Polisi na DPP kusema uchunguzi umekamilika?

Nimemsikia Mwenyekiti wa ZEC akiwaomba waandishi wa habari waandike ukweli kuhusu kilichotokea wakati wa Uchaguzi huko Zanzibar. Swali la kujiuliza waandishi watapata wapi taarifa sahihi kama Mwenyekiti wa ZEC anajificha au anafichwa? Kwa nini Mwenyekiti wa ZEC haitishi mkutano na vyombo vya habari ili aoneshe vielelezo ambavyo waandishi watavitumia kuueleza huo ukweli? Pia wanahabari watapata nafasi ya kumuuliza Mwenyekiti maswali magumu ambayo bado hayajapatiwa maelezo.

La kushangaza zaidi ni kwa nini Mwenyekiti wa ZEC ameitisha/ ametangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio bila kuondoa utata uliotanda wa uhalali wa tamko alilolitoa la kufuta uchaguzi uliokamilika wa tarehe 25.10.2015 na matokeo yake yote.

Hakuna viashiria vyovyote vinavyoonesha kuwa uchaguzi wa tarehe 25.10.2015 uliharibika au ulivurugika. Mvurugaji pekee ni Mwenyekiti wa ZEC aliyetangaza "kuvurugika/kuvurugwa" kwa uchaguzi huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na ikiwa inasubiri kutangaza matokeo ya majimbo 9 ambayo ZEC ilikwishayahakiki.

Kwa waliofatilia matangazo ya matokeo ya uchaguzi ambayo ZEC ilikuwa inayatangaza kitaifa wakiwa Bwawani, wanaweza kujiridhisha kuwa utangazaji wa matokeo ulikwamishwa/ilivurugwa na vyombo vya ulinzi kwa "lock down" na baadae kumchukua Makamu wa Mwenyekiti wa ZEC ambaye alikuwa anaendelea na kazi ya kutangaza matokeo baada ya Mwenyekiti kulalamika kuwa ni mgonjwa na siku iliyofuata Mwenyekiti wa ZEC hakufika kituo cha kutangazia matokeo lakini aliibukia kwenye runinga na kutoa tamko la kufuta uchaguzi. Wanahabari wanahitaji kupewa nafasi na muda wa kumhoji Mwenyekiti wa ZEC ili wanahabari hawa wapate kuueleza umma ukweli.

Bado Mwenyekiti wa ZEC anasikika akisema uchafuzi wa uchaguzi ulifanyika zaidi majimboni Pemba. Kwa nini amefuta uchaguzi wote? Kweli bado Mwenyekiti wa ZEC amejitathmini na kujiona ni mtu sahihi na makini wa kusimamia uchaguzi wa marudio?

Mwenyekiti wa ZEC itisha mkutano na wanahabari ukiwa na wajume wa Tume yako ili wanahabari wapate nafasi ya kuwahoji ili wawasaidie kazi ya kueleza ukweli. Kwa sababu mpaka muda huu, kiashiria ni kuwa wewe mwanyekiti unatumikia maslahi ya chama fulani, chama kinachonufaika na kufutwa kwa uchaguzi.
 
Nilitegemea baada ya miezi 2 kupita, Mwenyekiti wa ZEC angeibuka na ushahidi wa kuharibika uchaguzi katika majimbo yote ya Zanzibar.
Kama hakuwa na ushahidi wa kutosha, alimpasa kuuridhisha umma wa watanzania, dunia na wapiga kura wa Zanzibar japo kwa ushahidi wa kasoro za uchaguzi katika majimbo au vituo vya kupigia kura. Alitakiwa kuweka orodha ya majimbo na vituo ambao vinakidhi kutamkwa kuwa uchaguzi uliharibika,ulichafuliwa au ulikuwa na kasoro,matatizo ambayo yanaondoa uhalali wa kuitwa uchaguzi huru. Mpaka muda huu ,si Mwenyekiti wa ZEC wala CCM ambao wametoa orodha ya vituo au majimbo husika.

Ni muda sasa, tokea niliposoma habari kuwa uchunguzi wa waliohusika na kuvuruga uchaguzi umekamilika. Hii ina maana ushahidi umekusanywa tayari. Ni kwa nini DPP hajafungua mashitaka ili mahakama nayo iondoe utata na kuridhia au kuupa uhalali "uchaguzi wa marudio"?

Kesi hii ingesikilizwa kwa daharura na kutolewa hukumu "fasta". Au zilikuwa ni mbwembwe tu za Polisi na DPP kusema uchunguzi umekamilika?

Nimemsikia Mwenyekiti wa ZEC akiwaomba waandishi wa habari waandike ukweli kuhusu kilichotokea wakati wa Uchaguzi huko Zanzibar. Swali la kujiuliza waandishi watapata wapi taarifa sahihi kama Mwenyekiti wa ZEC anajificha au anafichwa? Kwa nini Mwenyekiti wa ZEC haitishi mkutano na vyombo vya habari ili aoneshe vielelezo ambavyo waandishi watavitumia kuueleza huo ukweli? Pia wanahabari watapata nafasi ya kumuuliza Mwenyekiti maswali magumu ambayo bado hayajapatiwa maelezo.

La kushangaza zaidi ni kwa nini Mwenyekiti wa ZEC ameitisha/ ametangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio bila kuondoa utata uliotanda wa uhalali wa tamko alilolitoa la kufuta uchaguzi uliokamilika wa tarehe 25.10.2015 na matokeo yake yote.

Hakuna viashiria vyovyote vinavyoonesha kuwa uchaguzi wa tarehe 25.10.2015 uliharibika au ulivurugika. Mvurugaji pekee ni Mwenyekiti wa ZEC aliyetangaza "kuvurugika/kuvurugwa" kwa uchaguzi huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na ikiwa inasubiri kutangaza matokeo ya majimbo 9 ambayo ZEC ilikwishayahakiki.

Kwa waliofatilia matangazo ya matokeo ya uchaguzi ambayo ZEC ilikuwa inayatangaza kitaifa wakiwa Bwawani, wanaweza kujiridhisha kuwa utangazaji wa matokeo ulikwamishwa/ilivurugwa na vyombo vya ulinzi kwa "lock down" na baadae kumchukua Makamu wa Mwenyekiti wa ZEC ambaye alikuwa anaendelea na kazi ya kutangaza matokeo baada ya Mwenyekiti kulalamika kuwa ni mgonjwa na siku iliyofuata Mwenyekiti wa ZEC hakufika kituo cha kutangazia matokeo lakini aliibukia kwenye runinga na kutoa tamko la kufuta uchaguzi. Wanahabari wanahitaji kupewa nafasi na muda wa kumhoji Mwenyekiti wa ZEC ili wanahabari hawa wapate kuueleza umma ukweli.

Bado Mwenyekiti wa ZEC anasikika akisema uchafuzi wa uchaguzi ulifanyika zaidi majimboni Pemba. Kwa nini amefuta uchaguzi wote? Kweli bado Mwenyekiti wa ZEC amejitathmini na kujiona ni mtu sahihi na makini wa kusimamia uchaguzi wa marudio?

Mwenyekiti wa ZEC itisha mkutano na wanahabari ukiwa na wajume wa Tume yako ili wanahabari wapate nafasi ya kuwahoji ili wawasaidie kazi ya kueleza ukweli. Kwa sababu mpaka muda huu, kiashiria ni kuwa wewe mwanyekiti unatumikia maslahi ya chama fulani, chama kinachonufaika na kufutwa kwa uchaguzi.
vp maalim seif kujitangaza mshindi co kosa? Kwanin afanye kaz icyo yake
 
Ya kenya usiyaseme huku..... tumuombe ALLAH ya malizike kwao na kwetu yasije kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom