Kadutu Kapya
Senior Member
- Oct 24, 2015
- 122
- 26
Unategemea nini kama nchi hivi sasa ni ya uvccm ndiyo viongozi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera kwa uchambuzi mzuri! Nilifikiri ni Pasco!Nilitegemea baada ya miezi 2 kupita, Mwenyekiti wa ZEC angeibuka na ushahidi wa kuharibika uchaguzi katika majimbo yote ya Zanzibar.
Kama hakuwa na ushahidi wa kutosha, ilimpasa kuuridhisha umma wa watanzania, dunia na wapiga kura wa Zanzibar japo kwa ushahidi wa kasoro za uchaguzi katika majimbo au vituo vya kupigia kura. Alitakiwa kuweka orodha ya majimbo na vituo vya kupigia kura ambavyo vinakidhi kutamkwa kuwa uchaguzi uliharibika,ulichafuliwa au ulikuwa na kasoro,matatizo ambayo yanaondoa uhalali wa kuitwa uchaguzi huru. Mpaka muda huu ,si Mwenyekiti wa ZEC wala CCM ambao wametoa orodha ya vituo au majimbo husika.
Ni muda sasa, tokea niliposoma habari kuwa uchunguzi wa waliohusika na kuvuruga uchaguzi umekamilika. Hii ina maana ushahidi umekusanywa tayari. Ni kwa nini DPP hajafungua mashitaka ili mahakama nayo iondoe utata na kuridhia au kuupa uhalali "uchaguzi wa marudio"?
Kesi hii ingesikilizwa kwa daharura na kutolewa hukumu "fasta". Au zilikuwa ni mbwembwe tu za Polisi na DPP kusema uchunguzi umekamilika?
Nimemsikia Mwenyekiti wa ZEC akiwaomba waandishi wa habari waandike ukweli kuhusu kilichotokea wakati wa Uchaguzi huko Zanzibar. Swali la kujiuliza waandishi watapata wapi taarifa sahihi kama Mwenyekiti wa ZEC anajificha au anafichwa? Kwa nini Mwenyekiti wa ZEC haitishi mkutano na vyombo vya habari ili aoneshe vielelezo ambavyo waandishi watavitumia kuueleza huo ukweli? Pia wanahabari watapata nafasi ya kumuuliza Mwenyekiti maswali magumu ambayo bado hayajapatiwa maelezo.
La kushangaza zaidi ni kwa nini Mwenyekiti wa ZEC ameitisha/ ametangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio bila kuondoa utata uliotanda wa uhalali wa tamko alilolitoa la kufuta uchaguzi uliokamilika wa tarehe 25.10.2015 na matokeo yake yote.
Hakuna viashiria vyovyote vinavyoonesha kuwa uchaguzi wa tarehe 25.10.2015 uliharibika au ulivurugika. Mvurugaji pekee ni Mwenyekiti wa ZEC aliyetangaza "kuvurugika/kuvurugwa" kwa uchaguzi huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na ikiwa inasubiri kutangaza matokeo ya majimbo 9 ambayo ZEC ilikwishayahakiki.
Kwa waliofatilia matangazo ya matokeo ya uchaguzi ambayo ZEC ilikuwa inayatangaza kitaifa wakiwa Bwawani, wanaweza kujiridhisha kuwa utangazaji wa matokeo ulikwamishwa/ilivurugwa na vyombo vya ulinzi kwa "lock down" na baadae kumchukua Makamu wa Mwenyekiti wa ZEC ambaye alikuwa anaendelea na kazi ya kutangaza matokeo baada ya Mwenyekiti kulalamika kuwa ni mgonjwa na siku iliyofuata Mwenyekiti wa ZEC hakufika kituo cha kutangazia matokeo lakini aliibukia kwenye runinga na kutoa tamko la kufuta uchaguzi. Wanahabari wanahitaji kupewa nafasi na muda wa kumhoji Mwenyekiti wa ZEC ili wanahabari hawa wapate kuueleza umma ukweli.
Bado Mwenyekiti wa ZEC anasikika akisema uchafuzi wa uchaguzi ulifanyika zaidi majimboni Pemba. Kwa nini amefuta uchaguzi wote? Kweli bado Mwenyekiti wa ZEC amejitathmini na kujiona ni mtu sahihi na makini wa kusimamia uchaguzi wa marudio?
Mwenyekiti wa ZEC itisha mkutano na wanahabari ukiwa na wajume wa Tume yako ili wanahabari wapate nafasi ya kuwahoji ili wawasaidie kazi ya kueleza ukweli. Kwa sababu mpaka muda huu, kiashiria ni kuwa wewe mwanyekiti unatumikia maslahi ya chama fulani, chama kinachonufaika na kufutwa kwa uchaguzi.
Hao wote waliobeba hayo mabango ukiangalia wengi wao hawana passport za Tanzania na wamejiripua pale kama wasomali au wengine waburundi au warwanda.Sasa kwa akili zao wanafikiria maandamano ya watu 10 yanaweza kulazimisha Canada imuite balozi wake kutoka Tanzania.wanajua magnitude ya kumuuta balozi? Ni watu wenye akili kama zao tu ndiyo wanaoweza kuamini kama hicho kitu kinaweza kutokea. Na Juss anawadanganya nyumbu wake kwa kuweka hayo mabango kwenye wall ayake huku yeye akijua ukweli...angalia aliyoyafanya Mugabe kuna nchi gani ilisitisha uhusiano na Zimbabwe..Ni hatareeeeee
Pasco ni pacha wangu. teh teh, kwi kwiiii, khe khe kheeeeee. ding dong.Hongera kwa uchambuzi mzuri! Nilifikiri ni Pasco!
Ha ha ha haaah ni kweli aisee!!!Mwenye mawazo mafupi ni anayeshabikia vikwazo vya marekani kwa serikali ya Tanzania wakati anshudumiwa na serikali ya Tanzania. Ni sawa na kushabikia mafuriko wakati unaishi bondeni.