Mwenye mawazo mafupi ni anayeshabikia vikwazo vya marekani kwa serikali ya Tanzania wakati anshudumiwa na serikali ya Tanzania. Ni sawa na kushabikia mafuriko wakati unaishi bondeni.
Akili ,akili ,akili,
Elimu,elimu,elimu.
Maarifa,maarifa,maarifa.
Anayeshabikia kwa vitendo kunyimwa misaada ni yupi kati ya aliyefuta matokeo halali aliyoyatangaza kwa wawakilishi na kuwapa hati za ushindi au anayetoa tahadhari ya kuibuka kwa mgogoro mkubwa kwa uroho wa watu walianzisha chama na kusajili chama wakakiita CCM. Wamekifanya kuwa neno CCM ni mungu mwenye nguvu anayetawala milele na milele.
Ni utumwa na ushetani mkubwa kuanzisha chama halafu unakitukuza pasipo kujali usalama,utu,undugu,amani ,furaha ,upendo na umoja wa watu kisa umelenga tu kubaki madaralani milele.
Tutanyimwa misaada kutokana na akili za wanaCCM wengi kulewa madaraka. Ulevi unaondoa busara na hekima.
CCM wamelewa sana. Hawana aibu tena. Wanashabukia ubaguzi wa rangi ili wabaki madarakani kwa mapinduzi yaliyoongozwa na Jecha.
Aibu kubwa kama mtu bado haoni kwa wahisani wako sawa kutunyima misaada.
Wewe unafikiri Dr. Shein,Jecha ,Mwinyi,Mkapa na Kikwete na Makada wengine wanaochochea ubaguzi kule Zenji wataathirika kwa kukosa hiyo misaada?
Hawa hawajali kwani hawana hata harufu ya shida kwani wamefaidi ujinga na uvumilivu wa watanzania kwa muda mrefu ilihali wao sio wavumilivu hata wa kuona Maalim Seif anakua rais wa kakisiwa ka Zanzibar. Hawana huo uvumilivu. Ni bora mamilioni ya watanzania waumie kwa kukosa misaada lakini mwanachama na rafiki yao anayeitwa shein anakalia Ikulu ya Zanzibar.
Wanahubiri amani ,upendo,uvumilivu,na mshikamano wakati wao hawana hata mojawapo ya wanachohubiri.