Vikwazo zaidi vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Russia vyaondoa uwezekano wa suluhisho la amani la mgogoro

Vikwazo zaidi vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Russia vyaondoa uwezekano wa suluhisho la amani la mgogoro

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1679017141011.png


Wataalam wa China wamesema, hatua za karibuni za nchi za Magharibi za kuendelea kuitenga na kuongezea vikwazo Russia zinaondoa uwezekano wa mazungumzo ya amani, na badala yake, zitasababisha umwagaji damu zaidi katika mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Wataalam hao wametoa kauli hiyo baada ya nchi za Magharibi kujaribu kutoa taarifa inayoilaani Russia katika mkutano wa Kundi la Nchi 20 (G20), huku Umoja wa Ulaya ukiweka raundi mpya ya vikwazo dhidi ya Russia.

Ili kutoa suluhisho la mkwamo uliopo sasa, hivi karibuni China ilitoa mpango wa makubaliano ya Amani ili kutatua mgogoro huo. Mpango huo, ambao kwa kwa kiasi kikubwa umekubaliwa na pande husika, ulikataliwa na Marekani kwa madai kuwa “hauna mantiki”. Wataalamu hao wanaamini kuwa, tuhuma hizo zisizo na msingi zinaonyesha matakwa binafsi ya Marekani ya kutaka vita hiyo iendelee, na ni jaribio la kuzima ushawishi wa China katika majadiliano ya masuala ya kimataifa.

Katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa fedha wa G20 uliofanyika Bengaluru, India, baadhi ya nchi wajumbe wa Kundi hilo walikuwa wakipanga kutoa taarifa ya pamoja kuilaani Russia katika mgogoro wake na Ukraine, lakini jaribio hilo lilishindwa kutokana na upinzani kutoka Russia na China.

Kwa mujibu wa waraka uliochapishwa na Umoja wa Ulaya hivi karibuni, Umoja wa Ulaya na baadhi ya nchi za Magharibi, zikiwemo Marekani na Uingereza, zimeweka raundi mpya ya vikwazo dhidi ya Rusia, ikiwemo vizuizi zaidi vya biashara ya nje vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 11, vikwazo kwa raia na kampuni karibu 120 za Russia na matakwa mapya ya ripoti ya lazima ya mali za Benki Kuu ya Russia.

Li Ziguo, mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Elimu ya Kimataifa ya China anaona kuwa, mfululizo wa vikwazo hivyo hautakuwa na athari kubwa kwa Russia, kwani ni ishara za kidiplomasia kutoka nchi za Magharibi zinazotumika kuonyesha hasira zao. Anasema kusitishwa kwa matumizi ya nishati na biashara kati ya Russia na Ulaya na Marekani kulifanyika katika raundi ya kwanza ya vikwazo, na Russia, kwa upande mwingine, inatafuta njia za kukabiliana na athari za vikwazo hivyo kutoka nchi za Magharibi.

Zhang Hong, mchunguzi katika Taasisi Elimu ya Russia, Ulaya Mashariki na Asia Katikati katika Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China, amesema, kuitenga zaidi Russia katika uwanja wa kimataifa na kuiwekea vikwazo kumefanya uwezekano wa mazungumzo ya amani ama kutumia njia za kisiasa kutatua tatizo hilo kupungua kwa kiasi kikubwa. Anasema hatua kama hizo zinaweza kuzisaidia nchi za Magharibi kuondokana na ghadhabu zake na kujisikia vizuri kwa muda, lakini zitasababisha umwagaji damu, na uharibifu mkubwa mali kwani zinachochea zaidi mgogoro huo.

Ili kutatua mgogoro huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitoa waraka kuhusu nafasi ya China katika utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Ukraine, ikiwemo kuheshimu mamlaka halali ya nchi zote na kurejesha mazungumzo ya amani. Russia ilipongeza pendekezo la China lenye vipengele 12. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zarakhova alisema kwenye taarifa yake kuwa, kuhusu mgogoro wa Ukraine, Russia iko tayari kutimiza malengo ya operesheni maalum ya kijeshi kwa njia za kisiasa na kidiplomasia. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelesnky naye amesema yuko tayari kufikiria baadhi ya vipengele vya mpango huo. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron naye pia amepongeza mpango huo, na amenukuliwa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP akisema kuwa, ni jambo zuri kwa China kutoa pendekezo la suluhisho la amani kwa mgogoro huo.

Rais wa Marekani Joe Biden anaonekana kuwa mmoja wa watu wachache wanaopinga mpango huo wa amani wa China. Katika mahojiano na Shirika la Habari la ABC, rais Biden amesema wazo la China kujadili matokeo ya vita ambayo haikuwa ya halali kwa Ukraine halina mantiki.

Lakini Zhang anasema, mpango wa China unatetea amani, huku kile ambacho Marekani inataka ni mgogoro huo kuendelea kwa kuwa unaendana na maslahi ya nchi hiyo, hivyo ni wazi kuwa rais Biden atauchafua mpango wa China. Ametoa sababu nyingine kuwa ni kwamba Marekani inataka kupunguza ushawishi wa China katika majadiliano ya masuala muhimu ya kimataifa.

Ikumbukwe kuwa, mpango wa China ambao hauna upendeleo na sio wa kibinafsi, umetolewa wakati nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani zikiwa katika hatua za kusukuma mgogoro kati ya Russia na Ukraine kuingia kwenye hali mbaya zaidi, na unaleta mwanga wa amani kwa mkwamo ulioko sasa.
 
Nchi za magharibi ni wendawazimu sana, wanaiwekea vikwazo russia ambavyo vinawaathiri wao wenyewe. Halafu kwenye vyombo vya habari wanageuza maneno kwamba russia anapigwa vibaya na ameshindwa vita tayari.

Ukweli ni kwamba, russia kaishaimaliza na kaishaigeuza miji yote ya ukraine kama makaburi, haifai na haitamaniki, na bado anazidi kuiangamiza kabisa. Na hivo vikwazo vyao wala havimkoseshi usingizi urusi.

Nchi za magharibi ni wajinga, ndio maana mashoga.
 
Nchi za magharibi ni wendawazimu sana, wanaiwekea vikwazo russia ambavyo vinawaathiri wao wenyewe. Halafu kwemye vyombo vya habari wanageuza maneno kwamba russia anapigwa vibaya na ameshindwa vita tayari.

Ukweli ni kwamba, russia kaishaimaliza na kaishaigeuza miji yote ya ukraine kama makaburi, haifai na haitamaniki, na bado anazidi kuiangamiza kabisa.

Nchi za magharibi ni wajinga, ndio maana mashoga.
Kwahiyo urusi na China hakuna mashoga msomi.???
 
Nchi za magharibi ni wendawazimu sana, wanaiwekea vikwazo russia ambavyo vinawaathiri wao wenyewe. Halafu kwemye vyombo vya habari wanageuza maneno kwamba russia anapigwa vibaya na ameshindwa vita tayari.

Ukweli ni kwamba, russia kaishaimaliza na kaishaigeuza miji yote ya ukraine kama makaburi, haifai na haitamaniki, na bado anazidi kuiangamiza kabisa. Na hivo vikwazo vyao wala havimkoseshi usingizi urusi.

Nchi za magharibi ni wajinga, ndio maana mashoga.
Hujui kitu wewe, Tulia
 
Kwahiyo urusi na China hakuna mashoga msomi.???
Kule huo upuuzi haupo kwa kiwango unachodhania sababu hakuna mtu ambaye ana muda wa kusapoti. Ule ni upande wa kiumeni.

Mtu yoyote anayeshikamana na siasa na sera za kimagharibi huwa namuona ni mgonjwa wa akili kama hao watu wa huko magharibi. Katika mataifa ambayo yamepoteza uelekeo na yanaishi kama vichaa basi ni mataifa ya magharibi.
 
Huko vita ikiasha inabidi niende nikale watoto wazuri
Ukiwa unaenda unishtue mwamba. Hatubebi condoms wala nini kwanza mademu ya Ukraine naiskia hawanaga magonjwa ambukizi. Ni wasafi na watamu kama karanga za mayai.
 
U
Kule huo upuuzi haupo kwa kiwango unachodhania sababu hakuna mtu ambaye ana muda wa kusapoti. Ule ni upande wa kiumeni.

Mtu yoyote anayeshikamana na siasa na sera za kimagharibi huwa namuona ni mgonjwa wa akili kama hao watu wa huko magharibi. Katika mataifa ambayo yamepoteza uelekeo na yanaishi kama vichaa basi ni mataifa ya magharibi.
Shawahi kukaaoscow au Petersburg au Macau au Beijing msomi???
 
Back
Top Bottom