Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

Je umeusoma huo mkataba kujua majukumu na haki ya kila mdau wa mkataba?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Je, vigezo vili fuatwa kama walivyo kubaliana kimkatabaa? kama hapana basi bodi ya ligi na Tff wna makosa na kama vilifuatwa Gsm ata fidia hyo miezi aliotangazwa na vilabu [emoji848]
GSM kasema amevunja mkata, it means ulimukuwepo mpaka anaamua kuvunja, mwambie aombe JUA liwake Dar magodoro yakauke lasivyo KISUTU inamngoja.
 
Vishabiki vya simba vinaogopa GSM kutwa kuipa Kiki JF. Andamaneni laivu mueleweke
Waandamane Yanga na vilabu vingine 14 kwa kutoingiziwa 2B. Simba waandamane kwani wanamdai nani?
 
GSM kasema amevunja mkata, it means ulimukuwepo mpaka anaamua kuvunja, mwambie aombe JUA liwake Dar magodoro yakauke lasivyo KISUTU inamngoja.
Vipengele vya mkataba wako visipotekelezwa automatically huo mkataba unakuwa umevunjika

NB:Rudi shule ukajifunze kuandika na kusoma vizuri
 
Kama masharti hayakutimia waliaanza vp kuvaa nembo na kuweka matangazo ya GSM
Mkataba una consist timu 16 zote za ligi kuu kuvaa nembo ya GSM kwenye bega la kushoto

Timu 15 tu ndo zikawa zinavaa hizo nembo na timu ikakataa na hata bila kuchukuliwa hatua za kisheria

TFF na bodi ya ligi kufikia hapo mmevunja makubaliano yetu na mdhamini hana haja ya kuweka pesa tena ktk hilo
 
Kwa hiyo mlikuwa mnaitaka Simba hahahaaaaaaa godoro limelowa maji..
GSM wameidhamini ligi kuu na timu zote lazima wavae nembo Ya GSM na kama Simba alikuwa hataki kuvaa nembo hiyo basi automatically mkataba umevunjika hata ingekuwa timu yeyote iliyobaki isingevaa, hali ingekuwa ni hiyohiyo
 
Hiki ndo ambacho kimetengenezwa kwasasa mdhamini yeyote akitokea kuja kudhamini ligi na Yanga akiona ana chembechembe za Usimba basi hakuna litakalokubaliwa

Inshort kupitia hili ligi yetu tunaichimbia kaburi sisi wenyewe kwa ushabiki wa kipumbavu kabisa

Mpira unahitaji pesa za kutosha ktk kuendesha timu, hatuhitaji Simba na yanga pekee ndio ziwe timu zenye uwezo mzuri wa kipesa pekee, hapana.

Kupitia udhamini unaokuja ndio na hizi timu ndogo zinapata nafuu kifedha na kuleta ushindani madhubuti katk ligi yetu na kupelekea kupata wachezaji wazuri watakao wakilisha vzr timu ya Taifa Coz ss hatuna wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi, kwahyo tunategemea ligi ya ndani zaidi
 
Taja embu hata mmoja
Unafahamu kwamba mkataba wa TFF na TBC kurusha matangazo kwa njia ya radio ni Milioni 300 kwa miaka 2?

Kwa mwaka inatoka milioni 150 kwa timu zote 16,na ukigawa hiyo pesa hakuna hata pesa ya maana inayopata timu ili kujiendesha

Je, vipengele vya mkataba huo viliwekwa wapi wazi na vikajulikana, na Je, mliweza kuhoji chochote kuhusu hilo

Jitahidi kutokuwa na akili mgando kama vile unafanya kazi kwa wahindi mkuu
 
masharti yapi?
mbona hawakuvunja mkataba mapema kabla hayo masharti hayajafuatwa kwanini wasubiri hadi mzunguko wa kwanza uishe ndo wavunje mkataba?
Mkataba wa GSM na TFF umeingia wakati ligi tayari imeanza na takribani mechi 7 zimechezwa

Wakati ligi inaendelea na masharti ya mkataba hayatekelezwi, GSM akawa anawaandikia barua TFF kuhusu kutotimizwa kwa masharti yake na TFF wala hakujisumbua kujibu

GSM wasingeweza kusitisha mkataba wakati ligi inaendelea na wakasubiri mzunguko wa kwanza uishe ili wavunje mkataba wao ili tukirudi round ya pili basi kila iwe imetoa nembo ya GSM kwenye mabega yao

Just simple as it
 
π“π€ππ†π€π™πŽ 𝐋𝐀 π”πŠπŽπŒπŽ 𝐖𝐀 πŒπ€πŠπ”ππ€π‹πˆπ€ππŽ π˜π€ π”πƒπ‡π€πŒπˆππˆ

βžͺTunasikitika kuwajulisha kwamba Makubaliano yetu ya Ufadhili ya tarehe 23 Novemba 2021 yatakatishwa.

βžͺBarua hii inatumika kama notisi rasmi ya kutimiza madhumuni yaliyowekwa chini ya kifungu cha 5 cha makubaliano hayo.

βžͺTafadhali fahamu kuwa tunakatisha Mkataba huu kutokana na yafuatayo.

1. Mechi zote za ligi kuu ya nyumbani zinazohusisha Simba SC zimechezwa bila ya kuonyesha nembo ya GSM kwenye mbao za pembeni hii ni kinyume na kifungu cha 4.1 na 4.4 cha Mkataba wa Udhamini.

2. GSM imenyimwa kwa makusudi haki yake ya kuonekana kwenye bango la nyuma kwa habari zote zinazohusu Simba SC kinyume na kifungu cha 4.8 cha Mkataba wa Udhamini.

3. GSM imenyimwa kwa makusudi haki yake ya kuonekana kwenye mabango ya Pre and Post conference conference inayohusisha viongozi wa Simba SC kinyume na kifungu cha 4.9 cha Mkataba wa Udhamini.

4. GSM imenyimwa kwa makusudi haki yake ya kuonekana kwenye mkono wa kushoto wa jezi za Simba SC kinyume na kifungu cha 4.12 cha Mkataba huo wa Udhamini.

5. TFF imeshindwa kujibu barua zetu na kushindwa kurekebisha ukiukwaji kama ilivyoainishwa kwenye notisi ya uvunjaji wa tarehe 14 Desemba 2022. 6. TFF imeshindwa kutekeleza kanuni zake kuhusu Wadhamini.

7. Nembo na chapa za GSM mara kwa mara zimekuwa zikidharauliwa na maofisa wa TFF.

8. TFF imeshindwa kuweka viwanja vya haki kwa mechi za ligi kuu.

βžͺMwisho tunapenda kuitaarifu ofisi yako kuwa Bwana Ghalib Said Mohamed ameamua kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars kwa maslahi ya soka la Tanzania.
 
Hiyo hapo juu ni masharti yaliyovunjwa kwenye mkataba na nimetafsiri kwa Kiswahili ili wajinga wengine muelewe
 
Fact
 
Mkuu kuna vitu ukisikia uwe watulia na kutafakari...

GSM alikuwa anadhamini ligi ya NBC, na jezi anazotumia Simba kwenye ligi ya Bongo sio zile anazotumia kwenye mechi za CAF...

Sasa Simba angemtangaza vipi GSM kimataifa?
Mkuu Kuna watu wengine ni mabongo lala mkuu ishue iko wazi kabisa kwamba gsm ni mdhamini wa ligi kuu hiyo kimataifa anafuata nn kwa mkataba upi na kwa mandate ipi kuwa watu ni wajinga wa akili
 
Sasa vilabu vingepata vipi mgao wakati kulikuwa na mgogoro wa kimkataba?

Simba hakuwa tayari, hadi hapo GSM asingeweza kuendelea na mkataba na TFF...
hivyo aliingia mkataba kwaajili ya simba?
 
u
anacholilia mtu wenu hajatangazwa na Simba kwenye jezi na pre/post match na sio tff
jamaa wenu hana pesa.

 
Mkuu kuna vitu ukisikia uwe watulia na kutafakari... GSM alikuwa anadhamini ligi ya NBC, na jezi anazotumia Simba kwenye ligi ya Bongo sio zile anazotumia kwenye mechi za CAF... Sasa Simba angemtangaza vipi GSM kimataifa?
Sasa iweje avunje mkataba uliotekelezwa na vilabu 15 kati ya 16 sababu ya klabu moja tu aliyoitaja mara nne kwenye malalamiko yake? Kwa nini hazungumzii kuwalipa waliotumikia mkataba ila anazungumzia kuvunja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…