Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

Kwahio hapo anamulaumu nani. Kiki tu raisi wa CAF ulimkuta wapi na uliongea naye Nini wataje na hao wengine wadau wa soka majina yao.hapa naww umekuja tu kwaupande fulani fulani unaonekana tu .Sasa mbona NBC hakujitoa kwenye uwekezaji baada ya logo yao kufanyiwa mabadiliko ya rangi na timu ya yanga kwakisingizio Cha kijinga kua wao wanamiiko yao .bac kwakua sheria inasema vilabu vyote vinatakiwa vivae na visibadilishe nembo NBC angevunja mkataba na tusingekua na mdhamini kwa Sasa ila kwasababu wale lengo lao kukuza soka Hilo waliona la kawaida Mana kwenye kipengele chauzamini Hilo limo kua ikitokea kilabu itagoma kuvaa nembo adhabu itakua hii.kama ni hivo bas sheria badala yake ingekua hivi ikitokea kilabu itagoma kuvaa nembo ya mdhamini bac mdhamini atavunja mkataba hilo lingekua transparent sana ila in favor of GSM only no
 
Akijibu nisitue
 
Bado CCM hawajaja kudai pesa za kubandika matangazo kwenye viwanja vyao. Mwaka huu GSM wanalo. Unawezaje kuambatana na Kirusi Manara na ukafanikiwa.
 
Jitafakari upya kabla ya kuanza Ku QUOTE reply zangu

Pia kajifunze Writing and Reading skills upya
Dare you. Writing skills zipi acha kebehi za laisi laisi namna hio.wewe hapo umetumia skill ipi au unafikili kila mtu na watisha tisha tu jibu hoja kwa hoja sio propaganda
 
Sasa vilabu vingepata vipi mgao wakati kulikuwa na mgogoro wa kimkataba?

Simba hakuwa tayari, hadi hapo GSM asingeweza kuendelea na mkataba na TFF...

Umewahi kusikia Mkataba wenye Mgogoro kutekelezwa? Sasa kwanini Muhuni Gharibu aliruhusu Timu 15 zitekeleze Mkataba wenye mgogoro? Huoni hapo yeye pia atakuwa sehemu ya Mgogoro?
Halafu mgogoro wa Simba kwenye Mkataba unahusianaje na utiifu wa Dodoma Jiji na wengine kwenye Mkataba? Kwanini asipigwe Faini Simba kwa kukiuka Mkataba?
 
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.


Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.


Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.


“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.


“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…