Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

Vilabu 15 NBC havijapata mgawo wowote miezi 3

ANAANDIKA SHAFFIH DAUDA.

Wakati nipo Cameroon kwenye michuano ya CAF, nimebahatika kukutana na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, tumekuwa na vikao rasmi na visivyo rasmi

Nimepata bahati ya kukutana na kuongea na Rais wa CAF Patrice Motsepe, nimeiona dhamira yake ya kuhakikisha tunakuwa na African super cup, ili kufanikiwa inahitaji msuli kutoka kwa wadau wa soka ambao watawezesha super cup

Ila inasisitiza mazingira bora ya uendeshwaji wa soka Afrika ili wadau watakaoingia nao wanufaike na uwepo wa super cup

Ukweli ni kwamba wadau ndio kama NBC, AZAM na GSM, Jana nimesoma sababu zalizotolewa na GSM kuvunja mkataba zipo 8, na hawajazunguka sana wameziorodhesha zote

Kwa walichokiainisha tunahitaji kuanza upya, hakuna kampuni au mdau atakuja kuwekeza kwenye soka letu Tanzania kwa style hii

Hata waliopo pengine wana yao lakini wanavumilia kama ndoa, Ila baada ya waraka wa GSM kutoka jana, image ya uendeshwaji wa soka la Tanzania mbele ya watu ambao wangetamani kuwekeza is not the same anymore, wadau tukae chini tujenge soka letu Tanzania
Kwahio hapo anamulaumu nani. Kiki tu raisi wa CAF ulimkuta wapi na uliongea naye Nini wataje na hao wengine wadau wa soka majina yao.hapa naww umekuja tu kwaupande fulani fulani unaonekana tu .Sasa mbona NBC hakujitoa kwenye uwekezaji baada ya logo yao kufanyiwa mabadiliko ya rangi na timu ya yanga kwakisingizio Cha kijinga kua wao wanamiiko yao .bac kwakua sheria inasema vilabu vyote vinatakiwa vivae na visibadilishe nembo NBC angevunja mkataba na tusingekua na mdhamini kwa Sasa ila kwasababu wale lengo lao kukuza soka Hilo waliona la kawaida Mana kwenye kipengele chauzamini Hilo limo kua ikitokea kilabu itagoma kuvaa nembo adhabu itakua hii.kama ni hivo bas sheria badala yake ingekua hivi ikitokea kilabu itagoma kuvaa nembo ya mdhamini bac mdhamini atavunja mkataba hilo lingekua transparent sana ila in favor of GSM only no
 
Wale waarabu ni wajanja waliotoboa tu maisha kiujanja ujnja

Azam tv wakat anaizamin ligi juu VPL lwa mara ya kwanza alikuwa anatoa fungi lwa vilabu vyotee sim na yanga walitengewa 100 M, yanga chin ya aliyekuwa M/kitu wake muhindi yule wakagomea kuchukua zile pesa na wakagomea mechi zao kurushwa live
Azam.alikuwa anagawa pesa kama kawaida pasipo kujali utopolo imetia mgomo , mpaka baadae muhindi alipo ondoka, viongoz wa mpito wa utopolo wakaenda tff kudai gawio walilokuwawamelisusa swali na wakapatiwa mbona AZAM HAKUSEMA club moja imegomea.basi sitoi pesa ..in reality wale waarabu ni wajanja
Akijibu nisitue
 
Bado CCM hawajaja kudai pesa za kubandika matangazo kwenye viwanja vyao. Mwaka huu GSM wanalo. Unawezaje kuambatana na Kirusi Manara na ukafanikiwa.
 
Jitafakari upya kabla ya kuanza Ku QUOTE reply zangu

Pia kajifunze Writing and Reading skills upya
Dare you. Writing skills zipi acha kebehi za laisi laisi namna hio.wewe hapo umetumia skill ipi au unafikili kila mtu na watisha tisha tu jibu hoja kwa hoja sio propaganda
 
Sasa vilabu vingepata vipi mgao wakati kulikuwa na mgogoro wa kimkataba?

Simba hakuwa tayari, hadi hapo GSM asingeweza kuendelea na mkataba na TFF...

Umewahi kusikia Mkataba wenye Mgogoro kutekelezwa? Sasa kwanini Muhuni Gharibu aliruhusu Timu 15 zitekeleze Mkataba wenye mgogoro? Huoni hapo yeye pia atakuwa sehemu ya Mgogoro?
Halafu mgogoro wa Simba kwenye Mkataba unahusianaje na utiifu wa Dodoma Jiji na wengine kwenye Mkataba? Kwanini asipigwe Faini Simba kwa kukiuka Mkataba?
 
Tangu mkataba usainiwe Kati ya GSM na TFF na kushirikisha vilabu 15 ,vilabu havijapata mgawo ndani ya miezi yote mitatu .

Tulisema mkataba wa GSM ni wa kihuni na hawana huo ubavu kudhamini ligi , vilabu 15 vilijifanya vyote vimekubali na njaa zao na kukebehi Simba kumbe wanafanya matangazo ya GSM bure.

GSM ni genge la kihuni wamejaa chupli chupli tu.


View attachment 2111652
[https://res]

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.


Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.


Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.


Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.


“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.


“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.
 
Back
Top Bottom