Vilabu vya Tanzania havimo kwenye 10 bora Afrika

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
14,885
Reaction score
18,083
Katika orodha mpya iliyotolewa na Opta yenye kuonyesha ubora wa vilabu mbalimbali duniani kwenye vilabu kumi bora Afrika hakuna hata klabu moja ya Tanzania pamoja na tambo nyingi za wanazi wa vilabu vikubwa vya Tanzania lakini vilabu vyao havipo kwenye 10 bora Afrika.

Top 10 teams in Africa [Opta]:

1. Mamelodi Sundowns (164 globally)
2. Al Ahly (173)
3. Wydad AC (189)
4. Pyramids (282)
5. FUS Rabat (312)
6. FAR Rabat (322)
7. Orlando Pirates (351)
8. Petro De Luanda (360)
9. Raja Casablanca (365)
10. Belouizdad (369)

 
Kesho ni fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga ya Tanzania, dhidi ya USM Alger ya Algeria. Jitahidi kuufuatilia huu mtanange.

Achana na hizo siasa za kwenye mpira.
 
Hata kwa kutumia akili ndogo sana ya darasa la awali unaona hiyo orodha ni ya uongo.

Mfano Mamelod ana sifa gani ya kuwa timu bora barani Africa kiasi cha kuwazidi akina Al Ahly wanaojiandaa kucheza hatua ya fainali kwa msimu wa 4 au 5 mfululizo?

Ukiwa na akili timamu ukiambiwa Fus Rabat na Far Rabat ni bora kuliko Esperance de Tunis kwa lipi?.
 
Mimi nikiona cite flani imetoa rank ya vilabu kumi bora Africa, nikiona simba hayupo huwa najawa na hasira na kuona football ni ujinga na hiyo ranking ni ya kitakataka kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…