Villarreal yanyakua Kombe la Ligi ya EUROPA. Yaifunga Man. Utd kwa penati 11-10

Villarreal yanyakua Kombe la Ligi ya EUROPA. Yaifunga Man. Utd kwa penati 11-10


Klabu ya Villarreal imechukua Ubingwa wa Ligi ya Europa baada ya kuifunga Klabu ya Manchester United kwa penati 11-10

Timu hizo zilifungana goli 1-1 katika dakika 120 hatua iliyofanya mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.

Villarreal ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 29 kupitia kwa Gerard Moreno, lakini Manchester iliweza kusawazisha kupitia kwa Edinson Cavani katika dakika ya 55.

Katika upogaji Matuta, Kipa wa Villarreal, Geronimo Rulli aliweza kuokoa penati na kipa mwenzake David De Gea na kuipa timu yake Ubingwa huo.

Kocha wa Villarreal Unai Emery ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kushinda mataji ya UEFA Cup/Europa League kwa mara nne (2013-14, 2014-15, 2015-16 & 2020-21).

That day nilifurahi mno ushindi Villareal/Spain
 
Back
Top Bottom