Vimbwanga ndani ya vyumba vya mtihani.

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Katika vyumba vya mtihani kuna wakati huwa yanatokea mambo ambayo yanaweza kukuacha mdomo wazi. Moja ya matukio ambayo huwa nayakumbuka ni:
1. Tulikuwa katika mtihani wa taifa wa kidato cha pili sasa kuna dada mmoja hivi ambaye pia alikuwa ni sista duu hatari, sasa baada ya kufanya mtihani bwama akalala zake kumbe akajisahau akaachia kitu cha mbuuuuuu.....watu tukacheka, na yeye akastuka akiwa anaona aibu kinoma. Msimamizi akaja kutuuliza tunacheka nini watu tukawa kama hatusikii vile, tunajifanya tuko busy na pepa. Tulipotoka ikawa ndo story kwa kila mtu. Usista duu uliisha kwa muda.
2. Kuna siku na mimi yalikuta, nilifanya mtihani nilipomaliza nikawa nasubiri muda wa kumaliza pepa ufike nikaamua kujiegesha juu ya dawati nikalala, bwana weee kuja kuamka naona karatasi ya majibu imelowa na udenda, wakati wa kukusanya mwalimu alipoiona karatasi yangu ya majibu imeloa alikataa kuichukua eti hadi ikauke na matusi juu. Tulipotoka kwenye chumba cha mtihani nilipata tabu sana aiseeee....
 
Upo kwenye mtihan unakuta mwana anatumia vifaa vyote vya mkebe hafu wewe kapuku hahahaha ... Another booklet please akat wewe ndo kwanza page tatu unahangaika wapi ukondens hata kanyimbo ili umeonekana umeandika sana nyie jaman shule ... Shule achen iitwe shule .. Nawasalimu ndugu zangu pcb popote mlipo ... Phosphoenol pyruvate halet tena pyruvate now days wala atp .. Naye vyuma vimekaza .......
 
[emoji3][emoji16][emoji16][emoji16]kuna majitu yana sifaaa
 
Clouds fm wana" HEKAHEKA" kwenye kipindi chao pedwa cha leo tena

Capital radio wana " KASHIKASHI" kwenye kipindi chao cha lete raha

sijaelewa mantiki ya ku name haya majina kihivyoo

Ngojea nitafute jina ya hiyo kitu yako maana
 
MIE NILIKUWA NA KOPI MASWALI KATIKA question paper NAHAMISHIA KATIKA booklet.. mpaka muda unafika..

alaf MTIHANI wa MATHEMATICS unalala USINGIZI HAUJI.. unakuwa BORED.. alaf masaa ma 3.. unachoka.. unaanza kuhesabu mabati... ukichoka unalalia desk kama MBWA KOKO.. yaan hatari
 
tukiwa chumba cha mtihani CBE enzi hizo ukiona math ngumu unamtengenezea jamaa wa DIT kitambulisho chenye jina lako anenda kupiga paper fresh

sasa masnitch hawakosekani kumbe wakawatonya viongozi siku ya paper tunashangaa wasimamizi wanaingia na polisi venue after venue walipofika venue letu lilikuwa ni T4 bonge la hall wanakuja na mashine kama ya supermarket ile wanamulika kwenye kitambulisho kama kimetengenezwa CBE inapiga beep kama umetengeza nje hailii unapigwa pingu

nakumbuka kuna jamaa wa DIT alitoka mbio akampiga push HOD mmama alivyodondoka akamanyang'anya ile karatasi tuliyosign IN akakikimbia nayo alikimbizwa na polisi akaruka ukuta akadondokea makaburi ya upanga akatokomea πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Raha ya chumba cha mtihani somo liwe limeeleweka sivyo.... Jasho hujaa mikononi hata halieleweki limetoka wapi


Asee i can't imagine gals wengi hii huwanga na hii kitu common sijui ni swala la psychology isuue utakuta leso iko wet mpka anatoka nje
 
Jamaa aliona msala huo haahaa
 
Asee i can't imagine gals wengi hii huwanga na hii kitu common sijui ni swala la psychology isuue utakuta leso iko wet mpka anatoka nje
Humkumba kila mtu ambae somo halijasomeka kichwani ni shida.
 
Hahaha, jamaa alijitoa mhanga. Hakutaka kufa kizembe.
 
aisee, aliponifurahisha ni alivonyang'anya karatasi..,
 
aisee, aliponifurahisha ni alivonyang'anya karatasi..,

alipiga mahesabu makali ..maana asingenyang'anya karatasi wangetulazimisha kusign OUT then ambaye angemiss wangejua ndio aliyekimbia so angekamatwa alafu yy angetaja mtu aliyemleta kufanya paper jamaa alisepa na ushahidi πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

yale majaa ya DIT yapo smart hadi kwenye utapeli
 
Unahesabu na vitobo vya misumari kwenye bati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…