Katika vyumba vya mtihani kuna wakati huwa yanatokea mambo ambayo yanaweza kukuacha mdomo wazi. Moja ya matukio ambayo huwa nayakumbuka ni:
1. Tulikuwa katika mtihani wa taifa wa kidato cha pili sasa kuna dada mmoja hivi ambaye pia alikuwa ni sista duu hatari, sasa baada ya kufanya mtihani bwama akalala zake kumbe akajisahau akaachia kitu cha mbuuuuuu.....watu tukacheka, na yeye akastuka akiwa anaona aibu kinoma. Msimamizi akaja kutuuliza tunacheka nini watu tukawa kama hatusikii vile, tunajifanya tuko busy na pepa. Tulipotoka ikawa ndo story kwa kila mtu. Usista duu uliisha kwa muda.
2. Kuna siku na mimi yalikuta, nilifanya mtihani nilipomaliza nikawa nasubiri muda wa kumaliza pepa ufike nikaamua kujiegesha juu ya dawati nikalala, bwana weee kuja kuamka naona karatasi ya majibu imelowa na udenda, wakati wa kukusanya mwalimu alipoiona karatasi yangu ya majibu imeloa alikataa kuichukua eti hadi ikauke na matusi juu. Tulipotoka kwenye chumba cha mtihani nilipata tabu sana aiseeee....