Vinasaba kwenye nywele, uhai wake na malighafi bora ya wachawi

Vinasaba kwenye nywele, uhai wake na malighafi bora ya wachawi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nywele mojawapo ya 'viungo' vya mwili ama mazao ya mwili ni mojawapo ya malighafi muhimu kiroho na kimwili pia.... Nywele hizi za kichwani huota toka kwenye ngozi ya kichwa ambapo ndani yake ndio kumebeba software ya ufahamu na utambuzi wa kiumbehai... Nywele nyingine zimeota juu ya ngozi ambayo ndani na chini yake kuna njia za mishipa ya damu inayosafirisha damu mwilini mote...
Nywele ni kitu pekee katika mwili ambacho huendelea kuota ama kukua hata baada ya mwili kuachana na roho na kuwa mfu... Na hata baada ya muda mrefu kupita nyama na vingine vitaoza na kupotea lakini sio fuvu la kichwa na nywele zake... Hivyo nywele huishi hata baada ya kifo cha mwili.

Ni kutokana na hayo ndio maana nywele zikapewa nguvu ya pekee kwa upande wa nuru na kwa upande wa giza
Samsomi alipewa nguvu zake kupitia nywele
Yule kahaba alitumia nywele zake kumsafisha Kristo miguu yake....
Kiroho nywele ni kichaka kinachoweza kutumika kufuga roho wachafu na hata washirikina wanapotaka kumtengeneza mtu hutumia nywele zake kumfunga ama kuzima na kufifisha nyota yake....
Kwa wale mnaonyolewa nywele usiku hampaswi kuogopa sana kwakuwa kwa sehemu kubwa michezo hiyo hufanywa na wanga ama huchukuliwa kwenda kutumika kwa wengine na si wewe mwenyewe...
Zamani zile kukiwa hakuna saluni za biashara watu walinyoana nyumbani na kuzifukia nywele zao... Ni hatari kuziacha nywele zako zikisambaa hovyo......

Sasa je nywele zetu saluni ni salama? Maana tunanyoa na kuziacha huko...!
Nywele zako saluni zitakuwa salama tu endapo hakuna mtu mwenye nia ovu nawe, kwakuwa mnyoaji atazichanganya na za watu wengine kitu ambacho kitashindikana kuzisort
Nywele zilizochanganywa ni ngumu kutumika vibaya kwakuwa ni nywele mchanganyiko toka roho na vinasaba tofauti tofauti, hazifai na ni sawa na uchafu mwingine tuu....

Kikubwa na cha muhimu kama wewe ni mwamini wa hizi habari ni kuepuka kunyoa saluni moja kila wakati hasa saluni zile za mtaani kwako... Kama kuna mtu mwenye nia ovu nawe ni rahisi mno kukufanyia timing...
Unaweza kujiuliza kwanini wachawi wanapendelea nywele za kichwani zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote
. zinepatikana kwa wepesi
. zimekaa pazuri
. zina vinasaba vyenye nguvu zaidi
. zinepatikana kwa kiwango cha kutosha kwa haraka
. huchukua muda mrefu kuharibika na kupotea kama zisipokutana na moto ama kemikali kali

Nywele nyingine hatari na za kulinda sana ni nywele za sehemu za siri... Hizi ni spesheli kwenye ishu nzima ya mahusiano na uzazi! Zilinde! Zichunge... Dunia imejaaa wema na wabaya.... Lakini wabaya wana nguvu zaidi! Chukua tahadhari....! Makinika...!
 
Kila sehemu zinapoota nywele zina majina yake kama, kope, ndevu, vinyweleo, mavuuuu n. k, na ila sijawahi kusikia jina la nywele zinazoota kwenye mzunguko wa haja kubwa huitwaje?
 
MKUU ushaanza makeke yako,tupe vigongo Baba.Hii mada ni ya kufungia mwaka.
Alafu ni kwanini baadhi ya makabila wakifiwa wananyoa nywele?Shida ni mini?na wakiacha inakuaje?
 
MKUU ushaanza makeke yako,tupe vigongo Baba.Hii mada ni ya kufungia mwaka.
Alafu ni kwanini baadhi ya makabila wakifiwa wananyoa nywele?Shida ni mini?na wakiacha inakuaje?
Mila na desturi lakini pia kama njia ya kufukuza pepo la kifo katika familia
 
Kwa hiyo hizi nywele zikittumiwa vibaya naweza kuwa jiniazi...?
 
Back
Top Bottom