Vincent van Gogh

Iyegu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
6,276
Reaction score
12,404
Vincent Willem van Gogh (30 Machi 1853 - 29 Julai 1890 ) alikuwa mchoraji kutoka Uholanzi.
Huhesabiwa kati ya waanzilishaji wa uchoraji wa kisasa. Aliacha picha 864 na vichoro zaidi ya elfu moja na zote alichora katika miaka 10 ya mwisho wa maisha yake.

Van Gogh alizaliwa mjini Zundert (Uholanzi) kama mtoto wa mchungaji wa kanisa la Reformed.Baada ya shule alianza kazi katika duka la sanaa la mjomba wake. Kazi hii ilimpeleka pia London na Paris . 1876 aliacha ajira hii akaendelea kujaribu kazi mbalimbali.

Alifundisha katika shule, alikuwa msaidizi wa mchungaji wa kanisa, aliuza vitabu. Wazazi walimshauri kusoma theolojia lakini aliacha masomo haya tena.

=== Some Words Missing ===
 
Mkuu umejitahidi kumuelezea jamaa lakini hujamtendea haki Vincent Van Gogh...kumueelezea huyu genius mgonjwa wa akili aliekuwa na uwezo hadi wa kuchora upepo unaovuma na kuuweka kwenye mchoro na muhasisi wa sketch za kuchora kwa rangi za mafuta na ajabu zaidi alifanya kazi zake zote kubwa akiwa na matatizo ya akili (ukichaa) kwenye asylum home yaani kama Mirembe vile, ambapo Dunia imekiri kwamba anaqualify kuingia Kwenye kundi la magenius watano wa uchoraji Duniani wa muda wote akiwemo Leonardo Da Vinci, Michelangelo, Vincent Van Gogh, Raphael, Pablo Picasso.

Sikia hii kwamba sketch yake ya Dr Gatchet ndio mchoro uliouzwa kwa bei kubwa zaidi Duniani wa zaidi ya dola $149m kwa mchoro mmoja tu na ana michoro kibao mingi ikiwemo ule maarufu zaidi wa Starry starry night ambao Bill gate anaupenda na kuukabili kuubandika pale nyuma ya Laptop yake huku akiacha nembo yake ya kibiashara ikifunikwa na kufichwa na mchoro wa jamaa...hii ni heshima kubwa sana!

Pia Van Gogh aliwahi kuuza picha moja tu katika maisha yake yote kwa dola 80 kama laki na kitu tu...then sasa hivi mchoro wake mmoja ni trillion za pesa? Nadhani akifufuka anaweza kufa tena kwa mshtuko maana hiyo bei hakuwahi labda hata kuiwaza kama kazi zake zinaweza kuwa na thamani hiyo.

Kihualisia maisha yake yanasikitisha sana na kutoa mafunzo mengi kuhusu maisha. Aliishi katika upweke uliotopea na kaka yake waliopendana kwa dhati hadi kufa wakafa siku zikifuatana na kuzikwa karibu kabisa maana waliacha hayo maelekezo.

Mkuu huyu ana mengi sana...ila hongera kwa kujaribu kumuelezea.
 
Wewe Humble African kama sio mwalimu inakubidi uwe mwalimu sasa maana huwa nakuelewa sana
ahsante
"Huwa naamini Kazi ya ualimu ni kuyafanya magumu kuwa mepesi" mara nyingi huwa najitahidi kufanya hivi.

Na watu wengi wananiulizaga Kama Mimi ni mwalimu.. Mkuu Mimi sio mwalimu ila napenda sana kuwa mwalimu.. Huwa nafurahi nikiona nimefanya gumu kuwa jepesi na mtu akanielewa that's my pleasure. Bahati mbaya mimi ni janki tu wa mtaani. Just jobless guy!

Nimefurahi kwa compliment yako mkuu. Shukrani sana.
 
Mkuu Humble African Nikushukuru Kwa Elimu Yako Kuhusu Huyu Mtu.

Maelezo Yote Niliyoyaleta Ni Copy & Paste Kutoka Wikipedia Wala Sijaongeza Chochote.Nimekuwa Nikijitutumua Kusoma Kuhusu Binadamu Maarufu Wa Zama Hizo, Hivi Karibuni Nilisoma Makala Moja Iliyohusu ' Top 5 Artists Of All Time '.Hapo Wa Kwanza Da'Vinci , Wa Pili Ni Vicent Van Vogh Na Wa Tatu Ni Michelangelo Na Wengine Wameendelea.

Hao Wawili( Da'vinci Na Miche') Nawajua ( Shukrani Kwako ), Ila Van Gogh Sikujuwa Namjua Na Nilishangaa Kumkuta Akiwa #2.

Hivyo Ikabidi Nianze Kumsoma Kichaa Huyu Japo Nahisi Bado Sijammaliza Ipasavyo Na Niombe Radhi Kwa Kukopi ' Kimakala ' Cha Wikipedia Ambacho Hakija Mtendea Haki Vicent Van Gogh!

Kwa Heshima Ya Jukwaa, Nakuomba Mkuu Humble African Uje Na Nondo Iliyoshiba Juu Ya Huyu Jamaa, Wengine Kwenye Ile List Nitakuletea Pia Upate Kutujuza Kuhusu Waasisi Hawa Wa Sanaa Ya Kisasa!

Ahsante!
 
Mkuu binafsi Nina imani bado na wewe maana najua kwa sasa unakusanya nondo juu yake Van Gogh.

Naomba ujichallenge kwa kuileta makala murua kuhusu jamaa iliyoshiba zaidi maana unamsoma vizuri.

Ukitaka kumfahamu zaidi sikiliza huu wimbo theme song kutoka kwa Julio iglesias baba yake na Enrique iglesias ambae wataalamu wa muziki wana mconsider kama the best Spanish Singer of all time. Alimuimba Vincent Van Gogh kwenye wimbo unaoitwa starry starry night ambao ni mchoro maarufu wa Van Gogh but at the same time wimbo huwa wanauita Vincent. Huu hapa https://www.google.com/url?sa=t&sou...DfsQtwIIJTAB&usg=AOvVaw0esaxLii1HcGys-6PzGd5A

Alijitahidi kumuelezea kwenye hii nyimbo very soothing, relaxing and powerful.
 
Mkuu Humble,
Nimepokea Challenge Na Nitajaribu Kumleta Huyu Mtu Kwa Mapana Yake Mungu Akijaalia.

Na Wengine Waliobaki Pia Nitatumia Mwanya Huo Kujijenga Zaidi Kwenye Intelijensia Ya Manguli Wa Sanaa Wa Nyakati Hizo.



Iyegu.
 
Mkuu Humble,
Nimepokea Challenge Na Nitajaribu Kumleta Huyu Mtu Kwa Mapana Yake Mungu Akijaalia.

Na Wengine Waliobaki Pia Nitatumia Mwanya Huo Kujijenga Zaidi Kwenye Intelijensia Ya Manguli Wa Sanaa Wa Nyakati Hizo.



Iyegu.
Shukrani mkuu! Tunasubiri makala murua kutoka kwako.

Kila la kheri!
 
Shukrani mkuu! Tunasubiri makala murua kutoka kwako.

Kila la kheri!
Ahsante Mkuu Humble,

Changamoto Yako Itanifanya Kuwa Imara Zaidi Kwenye Ulingo Huu Wa Jamii Intelligence!

Iyegu
 
Ahsante Mkuu Humble,

Changamoto Yako Itanifanya Kuwa Imara Zaidi Kwenye Ulingo Huu Wa Jamii Intelligence!

Iyegu
Salute Chief Iyegu.
Umejitahidi mkuu kumuelezea nami nimemfahamu.
Endelea kujisomea ugundue mengi yaliyofichwa.
 
Salute Humble Afric..
Kama kawaida yako hujawahi kuniangusha kwenye Article zako. Sometimes natamani ningekua wewe yaani you so talented in writting and Describing. Kama ningekua nauwezo kama wako ningeandika mengi sana humu JF basi tu.
 
Msisahau Kuni-tag huo uzi ukitoka,...any of you mwenye atakuwa tayari kumuelezea Vincent

Baada ya kusoma baadhi ya article za Humble African hapa kwanza ile ya Michelangelo aligusia humo ndani uyu jamaa

Nipo interested sana na uyu jamaa nasubiri Humble African afanye yake tumjue uyu 'Crazy Genius'
 
Salute Humble Afric..
Kama kawaida yako hujawahi kuniangusha kwenye Article zako. Sometimes natamani ningekua wewe yaani you so talented in writting and Describing. Kama ningekua nauwezo kama wako ningeandika mengi sana humu JF basi tu.
Da'Vinci hata wewe unajua kuandika vizuri mkuu, ile makala yako ya Sananda na genius Da Vinci zilikuwa ni makala bora na elimishi sana.

Huwa huko makini sana ukiacha pombe za kienyeji zile...ukizirudiaga huwa unakuwa na akili kama za Baba swalehe.
 
Salute Chief Iyegu.
Umejitahidi mkuu kumuelezea nami nimemfahamu.
Endelea kujisomea ugundue mengi yaliyofichwa.
Shukrani.

Ngoja Nijiandae Kumueleza Huyu Chizi, Van Gogh!
 
Sawa Mchokozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…