Mkuu umejitahidi kumuelezea jamaa lakini hujamtendea haki Vincent Van Gogh...kumueelezea huyu genius mgonjwa wa akili aliekuwa na uwezo hadi wa kuchora upepo unaovuma na kuuweka kwenye mchoro na muhasisi wa sketch za kuchora kwa rangi za mafuta na ajabu zaidi alifanya kazi zake zote kubwa akiwa na matatizo ya akili (ukichaa) kwenye asylum home yaani kama Mirembe vile, ambapo Dunia imekiri kwamba anaqualify kuingia Kwenye kundi la magenius watano wa uchoraji Duniani wa muda wote akiwemo Leonardo Da Vinci, Michelangelo, Vincent Van Gogh, Raphael, Pablo Picasso.
Sikia hii kwamba sketch yake ya Dr Gatchet ndio mchoro uliouzwa kwa bei kubwa zaidi Duniani wa zaidi ya dola $149m kwa mchoro mmoja tu na ana michoro kibao mingi ikiwemo ule maarufu zaidi wa Starry starry night ambao Bill gate amekubali kuubandika pale nyuma ya Laptop yake huku akiacha nembo yake ya kibiashara ikifunikwa na kufichwa na mchoro wa jamaa...hii ni heshima kubwa sana!
Pia Van Gogh aliwahi kuuza picha moja tu katika maisha yake yote kwa dola 80 kama laki na kitu tu...then sasa hivi mchoro wake mmoja ni trillion za pesa? Nadhani akifufuka anaweza kufa tena kwa mshtuko maana hiyo bei hakuwahi labda hata kuiwaza kama kazi zake zinaweza kuwa na thamani hiyo.
Kihualisia maisha yake yanasikitisha sana na kutoa mafunzo mengi kuhusu maisha. Aliishi katika upweke uliotopea na kaka yake waliopendana kwa dhati hadi kufa wakafa siku zikifuatana na kuzikwa karibu kabisa maana waliacha hayo maelekezo.
Mkuu huyu ana mengi sana...ila hongera kwa kujaribu kumuelezea.