Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Naomba ku-declare interest kuwa mimi ni mdau wa safari (abiria) wa mara kwa mara 75% nikiwa natumia bus.
Niliwahi kuandika kuhusu "uhuni" wa kile kinachoitwa ving'amuzi kwenye mabasi.
Leo hii mabasi mengi yaliyosajiliwa kuanzia 2020 hayajafungwa ving'amuzi au vipo na havifanyi kazi! Mabasi ambayo hizo speed limit zinafanya kazi ni yale ya maskini tu.
Kwa mfano, ajali ya bus la kampuni ya Frester, hakuna popote pale taarifa inayoonyesha mwendo aliokua anaendesha dereva. Narudia HAKUNA!
Wiki iliyopita nilielekea maeneo ya Nzega, nilirekodi speed ya mabasi kadhaa ikiwa ni above 90km/hr hadi 130km/hr. December 2022 mara tano kwa mwezi huo nilisafiri kwenda Tanga kutoka Dar, mara mbili kwa gari binafsi na mara tatu kwa bus.
Hakuna bus hata moja, yote yanatoka Mbezi asubuhi kupitia Bagamoyo Road, hakuna bus lililokua linatembea chin ya speed 100km/hr.
Sasa unajiuliza, hivi ving'amuzi vililetwa kwa ajili ya akina nani? Kama tumeshindwa kusimamia basi tuseme kwa uwazi.
Muda huu ni 01:20 usiku, basi nililopo lina speed governor (yale ya zamani), kuna mabasi kadhaa yametupita utadhani tumesimama!
Mamlaka husika zitoe tamko rasmi la kuondoshwa kwa speed limit ili wachache wasiwe waathirika.