Vinyago/midoli vina roho

Kuna huu mdori umecheza film unaitwa CHUCKY, unaukumbuka?



Sasa kuna mwingine amefahamika anaitwa Black Chucky.... Anabamiza watoto si kawaida.




Chucky anaishi hapa kwangu na ukimuona hutoweza kumjua maana kajichubua mno!
 
NDIO MAANA.

Aliyewaumba amewatahadharisha, MSICHONGE SANAMAMU INAYOFANANA NA KITU CHOCHOTE HALAFU MKAITUMIKIA NA KUISUJUDIA.
Unakuta ndani na nje ya Kanisa kuna Sanamu nyingi kila kona hadi nje.
Wajamani wajameni mnamjua aliyezichonga hizo sanamu zote kama ni mtu wa aina gani ?
Mimi ni hapo tu ninapotofautiana na kanisa langu la Roman Catholiki na lazima niwe mkweli.
Sanamu zimenikwaza na siwezi kusujudu ili hali mbele kuna Rundo la Masanamu.
Nadhani watabadilika hapo baadae.
Karibu Sanamu zote zina roho chafu.
Kwa wale wataalamu wa VILINGE kama mleta mada, Shetani anawaelekeza sanamu za kuweka madhabahuni, anawaelekeza hadi Sura za sanamu hizo, na alama za kuweka.
Ukimwuliza mtumishi huyo wa mambo ya giza anakuelekeza kila sanamu kwa jina lake.
Utasikia huyu ni Belzebuli, huyu ni Lusifer, huyu ni mzimu wa makaburini, huyu ni malkia wa marine (marine spirit) nk.
Anawaita kama watu hai na chakula anawapa cha kufukiza kwenye chetezo, na damu.

Ni mambo makubwa wandugu wapendwa, nina mengi ya kuwaeleza.

Achaneni kabisa na Sanamu, au Midoli au chochote kinachofanana na hivyo.

MUACHE PIA KUCHORA TATOO, MWILINI
NI ALAMA (Chapa) ZA SHETANI. Mungu pia amezikataza.

ASANTE SANA mshana jr, Leo umefanya kazi kubwa ya Uinjirishaji.

Nimeeleza hivyo kwa sababu ya mapenzi yangu ya dhati kwenu na jamaa zenu muwaeleze pia.

Mwenye masikio na amesikia.
 
[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda kuna ukweli,maana mimi mathalani huwa naviogopa sana, naviogopa tu hata sijui kwa nini!!! Niikiingia kwenye nyumba au ofisi ambayo sofa zina midoli hata sikai kabisa, unless niwaombe waliondoe. Anyway, labda nina matatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu roho yako kupitia jicho la tatu inaona na nafsi inashindwa kuhimili
Ogopa sana vinyago kwenye ofisi za matajiri ama vinyago vyenye vyombo vya usafiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi TBS au BASATA wako wapi mpaka hizi vitu inauzwa bila ukaguzi wao? Hata Zimamoto, TRA, Intelijensia, Polisi jamii, na SSIT, TFDA, Mkemia mkuu na wengine nani sijui! Kweli ndio maana kina omera wanatuona sis kama misukule. "Hakuna mkate mgumu bele ya kiroba"!!!!
 
Hawaamini katika mambo ya kiroho ofisini lakini mitaani ni waumini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeiona hii mada iko hewani sasa
 
Mdoli hata uwe umepambwaje huwa nautazama Mara mbili mbili, hata nguo yenye mchoro sitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…