Vinywaji na vyakula vinavyochangia kuporomoka kwa kinga ya mwili:

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993
Habari zenu wakuu.

Najaribu kutengeneza orodha ya vyakula na vinywaji ambavyo kwa namna moja ama nyingine huchangia kuporomoka ama kushuka kwa kinga yetu ya mwili dhidi ya magonjwa kiasi cha kupelekea upungufu wa kinga mwilini.

Mimi navifahamu hivi vifuatavyo mpaka sasa, tafadhari tupia na wewe vingine hapo chini ili mwishowe tupate orodha iliyo kamili.

Vinywaji na vyakula vinavyochangia kuporomoka kinga ya mwili ni pamoja na:


  1. Alkoholi/Pombe za aina zote
  2. Madawa ya kulevya aina zote
  3. Soda aina zote
  4. Juisi za viwandani aina zote
  5. Sigara/bangi/tumbaku za aina zote
  6. Chai ya rangi na kahawa
  7. Ugali mweupe/sembe

Tafadhari wanajamvi naombeni nitupieni na vingine ambavyo nanyi mnavifahamu ambavyo mimi sijaviweka hapa.

Shukrani.
 
Namba 7 lete ufafanuzi, sababu ugali unakwenda na mboga mboga.
 
mleta mada usichanganye mambo. JIPANGE UPYA
 
Hizi ndiyo kamba za kutafutia soko la bidhaa zako za forever living nini mzee? Nikuambie kitu, Wazungu na waarabu wanapiga gahawa na chai 24/7 na CD4 zao hazishuki wala haziendi mshazari.
 
Nasikia hata "chakula cha usiku" kina shusha kinga za mwili..teh teh teh kaazi kweli kweli........
 
kwahiyo tusitumie chai mbona tumezoea tangia utoto wetu vp apo tutumie nn xaxa kama kifungua kinywa?
 
Mtume Paulo ALITABIRI kuwa siku za mwisho mafundisho kama haya yatashika kasi, mara unaambiwa usile hichi, kula hichi, usinywe soda ina madhara! na kadhalika! lakini haya mafundisho ni ya kishetani!
 
Mtume Paulo ALITABIRI kuwa siku za mwisho mafundisho kama haya yatashika kasi, mara unaambiwa usile hichi, kula hichi, usinywe soda ina madhara! na kadhalika! lakini haya mafundisho ni ya kishetani!

kaka soma bible vizuri wakina daniel walikuwa wanakula nini afu ulinganishe na unachokula wewe utaona utofauti ukizingatia kwamba watu wa zamani walikuwa wanamaisha marefu kuliko sisi.
 
weweeee bangi haina shida bana shee, mtutue.
 
Mkuu, chemsha maji yako kama kawaida ila badala ya kuweka yale majani meusi we weka ama mudalasini au tangawizi au mchaichai au ndimu fresh. hapo utakuwa umeepuka madhara ya majani hayo na utabaki na afya na kinga ya mwili itazidi kuimarika, hii hasa ni kwa wale ambao kinga zao za miili zimeshaanza kuleta mabalaa. lakini nitakuja kuelezea zaidi, inshallah.

kwahiyo tusitumie chai mbona tumezoea tangia utoto wetu vp apo tutumie nn xaxa kama kifungua kinywa?
 
Chai hatari,Bhange hatari,Biere hatari,vyoda hatari,ugali. Hatari,mbege hatari+ sukari hatari,chumvi hatari,ngono hatari,Dr ndodi kasema hata maji ni hatari ukinywa ukiwa umesimama,Kaaazi kweli kweli.
 
Mkuu,
Kwahiyo ukamdharau dr. Ndodi?, unadhani aliamka tu siku 1 akawa tayari anaitwa dr. Ndodi? kama ulivyoamka wewe siku 1 tu ukajiunga jf ukajiita imani ernest badala ya Imani Ernest?.

Ni kweli kama ulivyosema dr. Ndodi amesema kunywa maji ukiwa umesimama ni hatari. Ni hivi: "Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama".

Soma maelezo mengine HAPA

Chai hatari,Bhange hatari,Biere hatari,vyoda hatari,ugali. Hatari,mbege hatari+ sukari hatari,chumvi hatari,ngono hatari,Dr ndodi kasema hata maji ni hatari ukinywa ukiwa umesimama,Kaaazi kweli kweli.
 

We nawe haitwi dr. Ndodi ni Dr. Ndodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…