VIOJA Bungeni No.1

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Haya ndo baadhi ya maoni ya baadhi ya hawa wabunge wa Bunge maalumu la katiba. Michango ni mibovu na mingine haina umuhimu kabisa, lugha mbaya na wakati mwingine bila staha, lakini wao wanasema wana kazi muhimu sana!

"...Mheshimiwa mwenyekiti, nchi zote hizo zilizotolewa mfano kwamba ni za kidemokrasia zinaruhsu ushoga na usagaji, hatutakubali kuiga watuwanofanya mambo kama hayo ruksa!!"

"…Mheshimiwa mwenyekiti kuruhusu kura ya siri ni sawa na mtu anayeingia kichakani kujisaidia, macho anageuzia barabarani kwenye watu, ------ anayageuzia porini kwenye simba!!!"

"...Mheshimiwa mwenyekiti huyu Sendeka hajui Kiingereza…. Arudi akajifunze upya."

"...Mheshimiwa mwenyekiti, wanawake wa kiislam wakiwa kwenye zile siku zao mbaya dini inawakataza kushika msahafu, hivyo tunaomba basi iwekwe namna ya kuwaapisha bila kushika msahafu!!... na wanaume wa kiislamu lazima wawe na udhu …"

"...Mheshimiwa mwenyekiti .... na tuendelee kudai ongezeko la posho mpaka kieleweke ...."

"...Mheshimiwa mwenyekiti sisi vijana lazima tusimame imara na kwa uwazi kwa kupiga kura ya wazi kwa sababu katiba inayotengenezwa ni yetu sisi vijana, nyie mazee wote mtakuwa mmeshakufa!!"
 
Mizigo at work. Hivi ulishajaribu kufikiria kuwa kodi kubwa kubwa tunazolipa kwenye umeme, mafuta, gas, PAYE, n.k ndo zinazotumika kuwalipa hawa mizigo?
 
Mkuu Mchunguzi hiyo ya mwisho ni siriaz au unatania?ni kijana gani huyo?
 
"...Mheshimiwa mwenyekiti, wanawake wa kiislam wakiwa kwenye zile siku zao mbaya dini inawakataza kushika msahafu, hivyo tunaomba basi iwekwe namna ya kuwaapisha bila kushika msahafu!!... na wanaume wa kiislamu lazima wawe na udhu …"
mkuu hii nani aliitapika!
 
Nadhani hii nchi inahitaji mtawala dictator kama Joseph Stalin ili awachinje mataahira wote. Wananchi wengine wanaobaki wanolewe kwa uzalendo na maadili. Tofauti na hapo ni upunguani mtupu!
 
hilo c bunge ni sawa na kikundi cha mipasho.
 
Nadhani Busara alikufa na kuzikwa nayo Mwalimu Nyerere na rafiki yake Kawawa maana hata Kingunge ni wale wale.
 
Naweza kukwambia hizo kauli zimetolewa na watu toka chama gani hata kama sifuatilii bunge!
 
Wacha wajidai ndo wakati wao huu wakula bata na kumalizia nyumba zao!!
 
hata waliochaguliwa wakionekana ni wenye hoja wamekuwa mamaluki wa ccm kwa kutekwa na hoja nyepesi ya Nape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…