Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Nilitoka nae nje mida ya usiku alipouna mwezi akasema Baba nataka ileeee (mwezi)alilia usiku kucha
 
Anataka kukojoa, akienda harudi. Nimeipenda

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Ina maana hata paper hakufanya kisa 20k/-?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Wakwangu ana miaka 4 ila me nikifika hom Dogo anakua na jeuri kama walikua wanaangalia movie na Dada wa kazi basi nikisha ingia anajiamini ye ndo anachagua movie ya kuweka kama NI katuni lkn nikiwa spo anakua mtulivu utamsikia mama ake anamwambia we ukishamuona baba ako unakua msumbufu coz UA naumia nikimuona anapgwa nampenda sana chalii yangu maana nlimpata kwenye vurugu za ujana na yy anajua
 
Ajui kwamba mamake ni mkeo
 
Mimi ka bint kangu karembo sana kana timiza mwaka keshokutwa, toka mama ake alipokuwa mja mzito nilikuwa nikimwambia unaenda kuni zalia GENIUS akawa anacheka ,ilikuwa tukiwa tumekaa tuna watch movie namlalia miguuni af namshika tumbo naongea na mtoto namwambia " hv unajua ww ni GENIUS ? " mke wangu anacheka af ananiambia nimeshamwandalia karai la maparachichi atakuwa anauza basi ananicheka maana mm nakasirika namwambia mwanangu ni Genius, sasa nilikuwa natamani sana mtoto wa kike na kweli nashukuru Mungu akanipa wa kike (GENIUS) basi akazalia sasa ni mjanja kiasi flani sijui nani kamfundisha ila akiwa na miezi nane mwishoni hapa alipoanza kusimamia kwenye kochi au kitandani ,ukimpa kalama anashika kabisa kama anataka kuandika ,siku moja nikamuuliza mama ake huyu akaniambia ww siulishamwambiaga yy ni GENIUS toka akiwa tumboni? Basi nafurai sana akisema vile ,mtoto huyu nimeanza kumuona anatumia ma left kila nikimpa kitu ashike mkono wa kulia anaamishia wakushoto ,namnyang, anya namuhamishia wakulia ananipiga anarudisha wakushoto, sasa sijui nimwache tu atumie ma left, kingine akiniona natoka ananililia anajua ni safari anampungia mama ake anamwambia "aiiii" akimaanisha baii ,anajua kuita baba ,mama na pia sasa ameanza kurusha hatua moja moja .anapenda remot sana na simu ,akiona naongea na simu yy anachukua remote anaweka sikiona anapiga kelele kama anaongea na mtu ila umuelewi, akinikitu nimekaa na laptop anachukua mouse yan anashika kama vile inavyoshikwaga vizuri kabisa na anaizungusha anafurahi akiona kale kamshale ka mouse ila ku click hawezi maana kimkono kidogo, nikimpokonya anaamia kwenye keybord anabofya na kakidole kamoja sasa nikimtoa hapo ni vita, nampenda sana mwanangu, nikiwa namkiss mama ake au namnong, oneza af yy alikuwa anacheza ataacha af atanikata jicho ilo kaah mpka naacha ,af nakauliza nini wewe unaniangalia. Af anacheka. Anapenda kunyonya na kunyonya kwake kama vile vita maana ananyonya kwa sarakasi atulii atabinuka hv kama amelala ananyonya ataweka mguu juu mara abinuke mara hv ukimshika atulie analia yani kama uko karibu utakanyagwa utawekewa miguu mpka basi ,nakumbuka siku mama ake ananiambia mja mzito nilitaka kukimbia maana mtoto wa soja umempa ujauzito ilikuwa kasheshe ila nashukuru nilijikaza kiume nikajitoa na hakika watoto ni Baraka sana kwa Mungu na hata kama ulikuwa huna kitu utashangaa tu pesa ujui zinatoka wapi yani unaona tu vitu vinatirirka kama vile ww tajiri kumbe tu mtoto kaja na baraka zake nampenda mke wangu kwakuniletea sweet baby girl. Nawashauri jamani usikatae mimba kama ni yako uwezi jua huyo mtoto atakuwa nani,.


Kikubwa nafurahi kwamba nina video za HD na still picha nikimaanisha documentary za toka mama yake alipokuwa na ujauzito na mpka dogo kazaliwa mpka sasa hv kila mara huwa nashuti video zake nakumuhifadhia so akikuwa ntazi edit nakufanya iwe documentary toka mama yake akiwa mja mzito mpaka hapo zitakapofikia ,huwa nikiwa mbali nao nafungua naanza kuziangalia nakuona kwamba hili jambo nililopitia mpka hapa ni Mungu huwa naenjoy sana nnapo kaa kuona hzo video vituko nk .
 
Mm wa kwangu alikuwa analilia kwenda shule kila siku, alipofikisha miaka miwili na miezi tisa nikamuanzisha shule, alienda siku mbili, siku ya tatu namuamsha anakataa anasema imetosha.[emoji23][emoji23]
Hahahahaaaa duh na ada ulikua ushalipa?watoto hawa jamani
 
Hakika wewe huna watoto, maana ukiwa mzazi unajua kwa uhakika mdomo unaumba haswa ukimsemea mwanao mambo ya ovyo ovyo kama unavyo dai wewe!
Mtoto ni hazina kutoka kwa MAULANA MOLA WETU, kwa nini nimnenee mambo ya ovyo! Naomba soma Zaburi ya 1 yote!
 
Mwenye Enzi Mungu bariki watoto wa Nchi yangu Tanzania milele yote!
 
Yaani sisi wenye watoto wakubwa zaidi ya hapo mmetutenga, au tusimulie tu vioja vyo vya zamani!?
 
Kuna siku nimerudi home nimekuta Rungu la mgambo mezani sebureni, nikauliza hili rungu la nani na limefikaje? Akanijibu langu, mmh nikamuuliza umelitoa wapi? Akajibu st Mary's, umepewa? Hapana nimelichukua nimekuta mlinzi kalala nimelibeba akiamka nitampa, nikachukua Rungu hadi St Mary's maana niniapoishi nyumba inaangaliana na hiyo shule nikamkuta mlinzi anahangaika kuitafuta silaha yake ya jadi, nikamwambia leo umechukuliwa Rungu kesho atasepa na mkwasa kuwa makini...kweli kesho yake nimemkuta tena dogo yupo na mlinzi mwingine nje ya geti anamuuliza hiyo bunduki gani? Unapiga? Inauwa jambazi? Naomba nione? Nikaona sasa huyu dogo anakoelekea sio kuzuri, maana mkiwa mnatazama movie ikiwa na ngumi utaulizwa maswali hadi kero, baba, yule ndo steering? Utajibu wee na muda mwingine na challenge namwambia hapa yule ni Audi, anasema wewe baba unazeeka vibaya yule sio adui yule ni stering bada unanidanganya, akiona bunduki anastuka kabisa utamsikia enheee hili ni bonge la muvi mi ndo napendaga, dogo anazingua nilichoamua nimempeleka kijijini akake huko japo miezi kazaa ili akirudi awe na akili zingine.....na huko kwa bibiyake alipo ni kesi za utundu tuu...chakula anapenda mrenda na ugali, na Tambi, ila ni mjinga akiwa na usingizi anakuwa kama kiteja flani hivi, hapendi kulala mchana. Ana miaka mi 3 na miezi 10, nimemuanzisha chokechea, ila ilibidi nimuhamishe maana anasema mwalimu wake hamfundishi vizuri na akifanya mazoezi yake mwalimu anamkataza...mtoto wangu mazoezi pekee anayojua yeye ni push ups..na wakati huyu bingwa anaanza kutembea kipindi ana mwaka amenitia hasara sana, alikuwa anakojolea simu na ktk fridge, yaani simu inaweza kuwa kitandani akahangaika akapanda akaishusha chini akaikojolea, Keisha akaitelekeza hapo akasepa zake, na ktk fridge ukiweka chakula unaweza kula mikojo anafungua anakojolea kisha anafunga anasepa....Namshukuru mungu sasa amekua na ninateseka na mdogo wake ambae yeye ni mabundi halali usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…