Mi wa kwangu balaa natamani akue kidogo labda nitapata zuri la kueleza, leo ni wiki ya tatu sijalala nakesha, dogo analala mchana wakati mimi nipo job, usiku halali na akilala mikononi ukimuweka kitandani tuu yani kabla hata hujakiacha kitanda kishaamka na kelele nyingi, kingine asee usikae karibu na mamaake ugomvi wake c mdogo atalia hapo hadi utashangaa, kingine tangu wiki iliyopita hajacheka sijui ndo kutabasamu hakuna. Ana miezi 4. Hataki kulazwa kama watoto wengine anapokuwa macho, yeye anataka kukaa na anakaa...huyo ni mdogo, kakayake yeye anapenda ngumi, anajua bunduki zote kwa majina, hili nimejaribu kumuonya mamayake asiwe akimuwekea movie za mapigano zaidi ya cartoon lakini sijui huyu kijana anajifunzia wapi maana hakawii kukwambia anataka awe mwanajeshi sababu hapendi majambazi, huyo Ana miaka mi 4, anajua kikorea, kajifunza wapi mi sijui...ila ana shida moja anapenda tambi tuu, vyakula vingine kula mpaka mpigizane kelele sana na husingizia anataka kukojoa akienda harudi..ana huruma sana na mamayake, mjanja mjanja sana ukikasiririka atajua jinsi ya kukufanya ucheke tuu, shida usimuache na mdogo wake peke yao, unaweza kuta mtoto analishwa ugali.